Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
VIONGOZI waliopo madaakani wameshauriwa kuweka tofauti zao za itikadi ya vyama vyao, ili waweze kukaa pamoja kwa ajili ya kuwezesha Watanzania kupata katiba mpya yenye tija kwa taifa.
Hayo aliyasema jana na Padre Ephrem Ruwa'ichi, wakati alipokuwa akihubiri katika misa ya tatu iliofanyika Kansia la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, mkoani Arusha.
“Mimi Napata wasiwasi kw ajinsi hali ilivyo sasa viongozi wetu kama wana nia ya dhati kusaidia wananchi, kwani hakuna kinachofanyika hata ukiangalia suala la mabomu pia hadi leo kimya,” alisema.
Alisema kuwa kwa sasa taifa inapita katika mchakato w akatiba lakini wananchi wanaona hali ilivyo kila mmoja upande wake, lakini kuna suala la mabomu pia watu walijeruhiwa kanisani wakaumizwa vibaya na kulazwa hospitalini mbambali nchini huku baadhi yao wakipoteza maisha lakini hakuna kinachoendelea.
Padre Ruwa'ichi alisema ni vema viongozi wakakaa meza moja ili kuhakikisha wanaleta katiba itakayoleta umoja na sio kujenga chuki na mgawanyiko.
“Kinachotakiwa viongozi wetu wafuate nyayo za bwana yesu ili waweze kuwa na upendo na kila mtu na wakiwa hivyo watawza kuweka maslahi yao pembeni na kutanguliza maslahi ya wananchi,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa ni muhimu katika suala kubwa la katiba viongozi wakaacha maslahi ya watu wachache pembeni na kutanguliza maslahi ya wengi mbele.
No comments:
Post a Comment