Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KATIBA ya Wekundu wa msimbazi Simba sc imekamilika baada ya kufanyiwa marekebisho na kukabidhi kwa uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti Ismail Aden Rage.
Katibu mkuu wa Simba sc, Ezekiel Kamwaga amezungumza na waandishi wa habari leo hii na kueleza kuwa tayari wameshakabidhiwa katiba yao kutoka serikalini na kinachofuata na kuanza kwa mchakato wa uchaguzi .
Awali uchaguzi wa Simba ulitakiwa kufanyika wiki iliyopita, lakini kutokamilika kwa katiba kulikwamisha mchakato mzima.
Kamwaga alisema baada ya zoezi la katiba kukamilika, kesho wanatarajia kukutana na kamati ya uchaguzi chini ya mwenyikiti wake, Mwanasheria Dkt. Damas Ndumbaro ili kupanga mchakato mzima.
Katibu huyo aliongeza kuwa baada ya kamati kukutana, taratibu zote zitawekwa wazi na wenye nia ya kugombea wataanza rasmi mchakato.
Aidha, Kamwaga alisema kuwa katiba yao imepitisha kuwepo kwa Kamati ya Maadili na Rufaa ambazo Mwenyekiti wa Simba SC, Ismail Aden Rage atazitangaza juma lijalo.
Pia katiba imependekeza kuwepo kwa mgombea mmoja mwanamke wa kuchaguliwa.
Kamwaga alisema, vipengele vyote vimepita katika katiba yao, isipokuwa cha ibara ya 26(4) kuhusu sifa za mgombea.
“Katiba ya sasa ni lazima katika wagombea watano wa kamati ya utendaji nafasi moja awepo mwanamke”.
“Nawaomba wanawake wanaojiona kuwa na sifa wajitokeze kwa wingi kuwania uongozi”.
“Wanaweza hata wakiwa watatu, lakini nafasi moja ni lazima,”alifafanua Kamwaga.
CHANZO MPENJA BLOG
No comments:
Post a Comment