Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 2 May 2014

RATIBA KUTATIZA KOMBE LA AFRIKA 2015


Shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa vilabu havitashurutishwa kuwaachilia wachezaji wao ili washiriki mechi za kufuzu kwa michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2015.


Hii ni kwa sababu tarehe ya kufanyika kwa michuano hiyo iko nje ya tariba ya shirikisho hilo ya michuano ya kimataifa.

Hii huenda ikasababisha mgongano kati ya vilabu na nchi hasa ikizingatiwa mechi za ufunguzi zinazogongana na mechi za vilabu barani Afrika.

Mechi za taifa bingwa Afrika, shirikisho na kombe la klabu bingwa Ulaya itafanyika kati ya tarehe 16-17.

Mechi hizo hazipo kwenye ratiba ya FIFA na kwa hivyo haitakuwa lazima wachezaji wa vilabu kuruhusiwa kuondoka.

Hata hivyo, michuano ya makundi itakayoshirikisha Ghana, Nigeria na Cameroon, zitakuwa katika tarehe iliyoidhinishwa na FIFA , ikimaanisha kuwa vilabu vya soka kote duniani lazima viwaruhusu wachezaji wao kushiriki mechi hizo.

Wachezaji kama Edward Sadomba, wataathiriwa na mgongano wa tarehe zilizo kati ya mechi za kufuzu zitakazofanyika 2015 na michuano ya vilabu.

Sadomba atahitajika kwa wakati mmoja na klabu yake ya Al Ahli Benghazi pamoja na timu yake ya taifa Zimbabwe.

Ni hali sawa kwa mchezaji wa Zamalek kutoka Mauritania Dominque da Silva pamoja na mtanzania Mbwana Samatta, anayechezea TP Mazembe ya DR Congo.

Maafisa wa kombe la mashirikisho wamesema kuwa wataviandikia barua vilabu vyenye wasiwasi wakitaka wachezaji kuruhusiwa kuwakilisha nchi zao kwa sababu ya changamoto zinazotokana na ratiba.
Lakini FIFA imeambia BBC kuwa wachezaji wanaweza tu kuondoka ikiwa maafisa wa vilabu na mashirikisho ya nchi husika wanaweza kukubaliana.

CHANZO, BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment