Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu
ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi
na ufaulu leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa
Eustella Bhalasesa.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Thursday, 31 October 2013
WAZIRI NAHODHA AONGOZA MAZISHI YA LUTENI MILIMA
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha
akitia saini kitabu cha mahudhurio, alipohudhuria kuuaga mwili wa marehemu
Luteni Rajabu Mlima kwenye kambi ya Jeshi la Ulinzia la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Wednesday, 30 October 2013
WAKALA WA NYUMBA BORA ULIVYOJIZATITI
Mkuu wa
Kitengo cha Mbinu za Ujenzi toka Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na
Vifaa vya Ujenzi(UNHBRA) Mhandisi Amri Juma akieleza kwa waandishi wa
habari(hawapo pichani) namna wakala hao unavyosaidia kutoa elimu ya ujenzi wa
nyumba bora,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Habari na Masoko toka Wakala hao Bw. Frimin Lyakurwa. Picha na Fatma
Salum-MAELEZO
KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI CHAINGIA SIKU YA PILI
Kamishna
wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga (kulia) akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya jeshi hilo katika Kikao cha Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kinachoendelea katika Hoteli ya
Paradise jijini Mbeya. Wa pili kulia (waliokaa) ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo,
Mbarak Abdulwakil. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi
la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. Wa pili kushoto ni Venance
Ntiyalundura, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Tuesday, 29 October 2013
RAIS KIKWETE AENDA LONDON KUHUDHURIA MKUTANO WA SERIKALI UWAZI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa
Swissport katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere wakati
akielekea kwenye ndege jioni ya jana, Jumatatu,
Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne
ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa
Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na Meneja wa Shirika la ndege
la Emirates uwanjani hapo Bw. Aboubakar Jumaa. (PICHA NA IKULU)
BALOZI MULAMULA AZUNGUMZIA UTATUZI WA MIGOGORO CHUO KIKUU SALISBURY, MARYLAND MAREKANI
KEYNOTE SPEECH ON CONFLICT RESOLUTION AND ORGANIZATION
DEVELOPMENT, SALISBURY UNIVERSITY, MARYLAND
Courtesies
I feel honoured to
join you for this panel discussion on conflict resolution and organizational
development. I feel privileged to be among the learned. I, for
sure, am not an academician rather a
diplomat. I don’t study conflict, I live them. As I
live them, I am compelled to learn to manage them. I come
from Tanzania, a country that has played extraordinary role in conflict
resolution in the Great Lakes Region and beyond. Therefore, my career path has
exposed me to organizational conflicts, as well as interstate and intra state
conflict.
NHC YAJIZATITI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA MAKAZI
Meneja Huduma kwa Jamii toka Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) Bw.Muungano Saguya akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani)kuhusu hatua zinazochukuliwa na Shirika hilo kutatua tatizo la makazi
hapa nchini ikiwa ni pamoja na mkakati wa miaka 5 wa utakaohusisha ujenzi wa
nyumba 15,000,wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)
Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bw. Frank
Mvungi.
MAKAMANDA WA AL-SHABAAB WAUAWA
KOMBORA lililorushwa kusini mwa Somalia limewaua makamanda wawili wa kundi la Kiislamu la al-Sahaab, wakazi wa eneo hilo wameiambia BBC.
ASKARI MWINGINE WA JWTZ AUAWA CONGO, M23 WAKIMBIA
Vikosi vya jeshi la Congo DR vikishangilia huko Rumangabo baada ya kuutwaa mji huo, jana Jumatatu Oktoba 28.
ASKARI mwingine wa JWTZ aliyeko katika vikosi vya kulinda amani nchini DR Congo, anadaiwa kuuawa juzi Jumapili, katika mapambano na waasi wa M23.
Habari kutoka mashariki mwa nchi hiyo zinaelezwa kwamba, askari huyo alikufa wakati akiwalinda raia katika mji wa Kiwanja.
Monday, 28 October 2013
NTAGAZWA KIDEDEA KORTINI
Arcado Ntagazwa
Na Happiness KatabaziMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru Waziri wa zamani, Arcado Ntagazwa na wenzake waliokuwa na kesi na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu zenye thamani ya sh milioni 74.9, baada ya kuwaona hawana hatia na hawakutenda kosa hilo.
Sambamba na hilo, mahakama hiyo imemshauri mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Noel Severe kufungua kesi ya madai kama walivyofanya hivi karibuni, ambapo walifungua kesi ya madai dhidi ya Ntagazwa.
Sambamba na hilo, mahakama hiyo imemshauri mlalamikaji katika kesi hiyo ambaye ni Noel Severe kufungua kesi ya madai kama walivyofanya hivi karibuni, ambapo walifungua kesi ya madai dhidi ya Ntagazwa.
NJELU KASAKA: NYERERE ALITAMANI SERIKALI TATU
Njelu Edward Mlugale Kasaka
Na Josephat Isango na Shehe SemtawaKADA mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye ni muasisi wa kundi la wabunge waliokuwa wakishinikiza hoja ya Serikali ya Tanganyika, maarufu kama G55, Njelu Kasaka, ameibuka na kuwashangaa wabunge wa chama hicho kupinga hoja ya muundo wa serikali tatu wakati ni yao tangu awali ya kudai mabadiliko ya muundo wa Muungano.
Kasaka aliongeza kuwa hata Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliona umuhimu wa muundo huo wa serikali tatu, isipokuwa alitoa tahadhari kuwa kwa aina ya uendeshaji wa serikali uliokuwa unaendekezwa kwa kuogopana na kulindana Muungano usinge dumu.
Kasaka aliongeza kuwa hata Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliona umuhimu wa muundo huo wa serikali tatu, isipokuwa alitoa tahadhari kuwa kwa aina ya uendeshaji wa serikali uliokuwa unaendekezwa kwa kuogopana na kulindana Muungano usinge dumu.
MWIGAMBA AKANUSHA KUTWANGANA NA MBOWE
Samson Mwigamba
Na Grace Macha, ArushaMWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha ambaye amesimamishwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, Samson Mwigamba, amesema kuwa hakupigana na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, kama ilivyodaiwa na baadhi ya magazeti.
TBA KUIPUNGUZIA SERIKALI MZIGO SEKTA YA UJENZI
Mtendaji
Mkuu toka Wakala wa Majengo Tanzania Bw. Elius Mwakalinga (kushoto) akieleza
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa wakala hao wa
kupunguza Matumizi ya fedha za Serikali katika sekta ya Ujenzi kwa kujenga
Ofisi za Serikali, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Bw. Erasm
Tarimo na kulia Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi. Picha na
Hassan Silayo-MAELEZO.
PROMOSHENI YA MAWAKALA YAZIDI KUCHANJA
Meneja wa Vodacom Tanzania,Chunya Mkoa wa Mbeya Bw. Elisha
Tengeni (kushoto)akimkabidhi wakala wa M-pesa wa hiyo,Bw.Damas Mtewele
hundi yake yenye thamani ya shilingi 100,000 aliyojishindia katika
Promosheni ya "Mkwanja kwa Wakala"yenye lengo la kuboresha maisha ya
mawakala wa kampuni ya Vodacom.Kampuni hiyo imetenga fedha taslimu kwa
mawakala 810 wa M-pesa ambao wamejivunia kiasi cha Shilingi Milioni 81
ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini Mchango wao kwa jamii ya
watanzania na kampuni hiyo,hadi sasa kati ya Wakala 270 wamepatikana
katika droo iliyochezeshwa leo ikiwa ni wiki ya tatu tangu kuanza kwa
promosheni hiyo.
MANISPAA YA ILALA KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Ofisa Uhusiano kutoka Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu (kulia) akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo
pichani) mafanikio yaliyopatikana katika utoaji wa huduma ya afya ikiwa ni
pamoja na kuboresha miundombinu ya afya katika manispaa hiyo, wakati wa mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dk. Asha Mahita.
RAIS KIKWETE AAPISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI NIGERIA NA MAKATIBU MBALIMBALI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Mhe Daniel Ole
Njolaay kuwa balozi leo Oktoba 28, 2013 Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi
Njolaay amepangwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria.
WIZARA: MSAFARA WA DK. NCHIMBI HAUKUPOPOLEWA MAWE
JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua
Pepe: ps@moha.go.tz
|
Dar
es Salaam
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MSAFARA WA WAZIRI NCHIMBI
HAUKUPIGWA MAWE SONGEA
Habari
iliyotolewa Oktoba 26, mwaka huu na baadhi ya magazeti na mitandao ya kijamii yenye
kichwa cha habari ‘Msafara wa Waziri Nchimbi wapigwa mawe Songea’ si
za kweli bali zimetengenezwa na walizituma kwa nia ya kupotosha jamii.
CUF NI SACCOS YA SEIF - UVCCM
Maalim Seif Shariff Hamad
Na Mwandishi Wetu, ZanzibarJUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imesema Chama cha Wananchi (CUF) ni Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) kutokana na kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa ataendelea kuwania nafasi hiyo na kutangaza nia ya kuwania tena urais mwaka 2015.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadif Khamis Juma katika mkutano wa hadhara wa vijana wa CCM uliofanyika katika viunga vya Vuga.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadif Khamis Juma katika mkutano wa hadhara wa vijana wa CCM uliofanyika katika viunga vya Vuga.
JWTZ WACHOMA MOTO KIJIJI CHA MINZIRO
Jenerali Davis Mwamunyange na IGP Saidi Ally Mwema
Na Charles Ndagulla, MisenyiWANANCHI wa Kijiji cha Minziro, Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, wameyakimbia makazi yao baada ya kundi kubwa la askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kuvamia na kuwashambulia raia kisha kuchoma moto nyumba zao.
KAMBI YA LOWASSA YAMEGUKA
Edward Lowassa
Na Waandishi WetuMBIO za urais wa mwaka 2015 ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinazidi kuchukua sura mpya baada ya kundi linalodaiwa kumuunga mkono Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kumeguka huku baadhi ya washirika wake wa Kanda ya Ziwa wakimwibua William Ngeleja.
Ngeleja ambaye amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, ni mmoja wa wanasiasa vijana wanaotajwa kuwa wafuasi wa kundi la Lowassa, jambo ambalo linazua hofu kuwa huenda kambi hiyo ikatikisika ikiwa juhudi hizo zitafanikiwa.
Ngeleja ambaye amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, ni mmoja wa wanasiasa vijana wanaotajwa kuwa wafuasi wa kundi la Lowassa, jambo ambalo linazua hofu kuwa huenda kambi hiyo ikatikisika ikiwa juhudi hizo zitafanikiwa.
Sunday, 27 October 2013
NSA: VYOMBO VYA HABARI UJERUMANI VYASEMA MAREKANI ILIKUWA INAMCHUNGUZA MERKEL
Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel akifurahia jambo na Rais Barack Obama wa Marekani
TAARIFA mpya katika vyombo vya habari vya Ujerumani zikiegemea nyaraka zilizovuja za ujasusi za Marekani zimeendelea kubomoa na kuzua maswali mengi kuhusu harakati za ujasusi za Marekani.
BOMU LAUA WAALIKWA 18 WALIOKWENDA HARUSINI
SHAMBULIZI la bomu la pembezoni mwa barabara katika jimbo la Ghazni, kusini mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, limeua watu 18 waliokuwa wanakwenda kuhudhuria sherehe ya harusi, maofisa wameeleza.
RAIS KIKWETE MGENI RASMI JUBILEI YA MIAKA 100 YA PAROKIA YA LUGOBA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki wa Jimbo
la Morogoro Onesphory Mkude, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la
Tanga Anthony Banzi, viongozi wa mkoa wa pwani na kwaya pamoja na watoto
wa shule ya Jumapili katika Parokia ya Lugoba, wilaya ya Bagamoyo, Mkoa
wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za Jubilei ya Miaka 100
Parokia hiyo.
Rais
Jakaya Kikwete na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Morogoro
Onesphory Mkude, wakishuhudiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo
la Tanga Anthony Banzi, wakiweka jiwe la msingi katika kiwanja
kitakachojengwa jengo la vijana katika Parokia ya Lugoba, wilaya ya
Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, leo Oktoba 27, 2013 wakati wa sherehe za
Jubilei ya Miaka 100 wa Parokia hiyo.
VIGOGO WA CCM WAPATA SHAHADA CHUO KIKUU HURIA
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Idara ya Itikadi
na Uenezi CCM, Makao Makuu, Daniel Chongolo, akipongezana na Mjumbe wa
NEC ya CCM, Asha Abdallah Juma baada ya wote kutunukiwa shahada zao katika
mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), yaliyofanyika Oktoba 27, 2013 Bungo, Kibaha mkoa wa Pwani. Chongolo ametunukiwa
shahada ya kwanza ya Mawasiliano ya Umma na Asha shahada ya pili ya
Biashara. Katikati ni Kada wa CCM, Rachel Kyala ambaye pia ametunukiwa
shahada ya Mawasiliano ya Umma.(Picha na Bashir Nkoromo)
WARAKA WA SAMSON MWIGAMBA KWA WATANZANIA
Samson Mwigamba
Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wa chama.
Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.
WIZARA YA UJENZI YAKABIDHI NYUMBA 13 KWA JESHI LA POLISI MKOANI KIGOMA
Waziri wa Ujenzi (katikati) akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) na Eng. Mashaka Mgallah ambaye ni Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Kigoma, kukagua eneo lililokuwa kambi ya ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Manyovu mkoani Kigoma. Nyumba hizo zimetelekezwa kwa miaka miwili. Wengine katika picha ni Watendaji kutoka Taasisi mbali mbali za Serikali.
CCM NI VITENDO SI MANENO, ASEMA WAZIRI NCHIMBI
Mbunge
wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi akiweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Likuyufusi iliyopo
katika Kata ya Lilambo, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. Dk Nchimbi yupo
mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi
mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake. Hata hivyo, Waziri Nchimbi
aliwaambia wananchi wa eneo hilo kuwa, chama chake kimefanya makubwa kwa kujenga
barabara, shule, pamoja na Zahanati tangu alipokuwa Mbunge wa jimbo hilo.
RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA PAKISTAN ALIYEMALIZA MUDA WAKE
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Pakistan nchini Mhe
Tajammul Altac aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 26, 2013
kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi.
RAIS WA USWISI AIFUNDA TANZANIA JINSI YA KUPATA FEDHA ZA KIFISADI
Katika mahojiano maalumu na timu ya waandishi wa Mwananchi na The Citizen jana, Graf alisema kuwa Serikali ya Tanzania inapaswa kusaini mkataba wa kimataifa wa kubadilishana taarifa za masuala ya usimamizi wa fedha na kodi ili kuweza kujua ni kina nani wameweka fedha nchini kwake na kunufaika na kodi.
PINDA AONYA UUZAJI WA 'PASIPOTI' CHINA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewaonya baadhi ya Watanzania wanaokuja katika Jiji la Guangzhou nchini China kwa ajili ya kununua bidhaa mbalimbali,waache kuuza hati zao za kusafiria kwa raia wa nchi nyingine kama njia ya kujiongeza kipato.
VIONGOZI WA CHADEMA WAZIPIGA KAVUKAVU MBELE YA MBOWE
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Na Mussa Juma na Peter Saramba, Mwananchi
Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.
Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa uongozi kwa muda usiojulikana.
Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.
Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa uongozi kwa muda usiojulikana.
DK. MWAKYEMBE AILIPUA TRA
Dk. Harrison Mwakyembe
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe ameishutumu Mamlaka ya Mapato (TRA), kuwa ni kikwazo katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).
MSAFARA WA WAZIRI NCHIMBI WAPIGWA MAWE
Dk. Emmanuel Nchimbi
Na Stephano Mango, SongeaMSAFARA wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, umepigwa mawe na wananchi waliojitokeza kuzungumzia kero ya daraja la Matarawe, ambalo linadaiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya watatu mwezi Oktoba mwaka huu.
Tukio hilo limetokea jana saa 10:00 jioni hadi saa 12:00, ambapo wananchi hao wakiwa na hasira walifanya fujo wakimshinikiza Nchimbi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini awasaidie kupanua daraja hilo ambalo kwa muda mrefu limesababisha kutokea kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo.
Tukio hilo limetokea jana saa 10:00 jioni hadi saa 12:00, ambapo wananchi hao wakiwa na hasira walifanya fujo wakimshinikiza Nchimbi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini awasaidie kupanua daraja hilo ambalo kwa muda mrefu limesababisha kutokea kwa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo.
MWENYEKITI CHADEMA ARUSHA ASIMAMISHWA KWA USALITI
Samson Mwigamba
Na Ramadhan Siwayombe, Arusha
BARAZA la uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini limemsimamisha uongozi Mwenyekiti wake wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.
Uamuzi huo umefikiwa juzi katika kikao cha dharura cha baraza hilo baada ya mwenyekiti huyo akiwa ndani ya kikao kutuma ujumbe katika mtandao wa kijamii unaolenga kuwachonganisha viongozi na wanachama wa chama hicho.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana juu ya uamuzi huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni mbunge wa Karatu, Mchungaji Israeli Natse, alisema wameamua kuchukua uamuzi huo mgumu kutokana na tuhuma zinazomkabili Mwigamba na kuhitaji uchunguzi wa kina.
BARAZA la uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini limemsimamisha uongozi Mwenyekiti wake wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.
Uamuzi huo umefikiwa juzi katika kikao cha dharura cha baraza hilo baada ya mwenyekiti huyo akiwa ndani ya kikao kutuma ujumbe katika mtandao wa kijamii unaolenga kuwachonganisha viongozi na wanachama wa chama hicho.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana juu ya uamuzi huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni mbunge wa Karatu, Mchungaji Israeli Natse, alisema wameamua kuchukua uamuzi huo mgumu kutokana na tuhuma zinazomkabili Mwigamba na kuhitaji uchunguzi wa kina.
LOWASSA: NITAENDELEA KUPIGANIA SHULE ZA KATA
Edward Lowassa
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema ataendelea kuzipigania shule za sekondari za kata kwa kuwa shule hizo zimekuwa mkombozi kielimu katika familia za watu walio na kipato cha chini.
Lowassa aliyasema hayo jana wakati alipoendesha harambee iliyoandaliwa kwa pamoja na shule za sekondari 12 za Tarafa ya Mbagala, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo zilipatikana sh milioni 233 huku lengo likiwa sh milioni 400.
Alisema kuzipigania na kuwa mkereketwa mkubwa wa shule hizo, bado hilo halimfanyi kuwa mmiliki wa shule hizo, bali amefanya hivyo kwa ajili ya kutaka kuleta usawa wa kielimu katika jamii ya Kitanzania.
Saturday, 26 October 2013
WAZIRI KAGASHEKI MATATANI
Balozi Khamis Kagasheki
JESHI la Polisi mkoani Arusha, limeingia kwenye kashfa nzito baada ya kubainika kumdanganya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kwa kuwahusisha raia wawili wa kigeni na biashara ya ujangili wakati si kweli.
Hatua hiyo inakuja baada ya Waziri Kagasheki kudai kuwa watumishi wa serikali wanakwamisha juhudi za kukabiliana na majangili wa tembo, akitolea mfano wa Mkuu wa Upelelezi wa Polisi mkoani hapa (RCO), Duwan Nyanda, kwamba aliwatorosha raia wawili wa Saudia ambao walikamatwa wakiwa na meno ya tembo pamoja na silaha nzito.
JK AIKATIA TAMAA CCM
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, ameonyesha wasiwasi wa chama hicho kushindwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 iwapo watendaji wake wataendelea na vitendo vya rushwa.
Alisema kuwa kwa sasa chama hicho kikongwe kimepoteza matumaini kwa Watanzania kutokana na vitendo ambavyo siyo vya kiungwana vinavyofanywa na watendaji.
DK. NCHIMBI ALIRARUA RIPOTI YA UHALIFU
Dk. Emmanuel Nchimbi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ameirarua ripoti ya uhalifu na kusema kuwa waliofanya kazi hiyo wana lao jambo. Mbali na hilo, Dk. Nchimbi, amesema kuwa anashangazwa na utafiti huo ambao umeilenga Tanzania pekee ambayo lengo lake ni kutaka kuua biashara ya utalii, kwa kujenga hofu miongoni mwa jamii na taasisi za kimataifa.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Taasisi ya Utafiti kuhusu kuondoa Umasikini (REPOA), kutangaza matokeo ya uhalifu, ambapo walibaini kuwa Tanzania ni kinara wa matukio ya kihalifu katika nchi za Afrika.
WAFUGAJI WAPIGANA DODOMA
VURUGU zimetokea katika Kijiji cha Zajilwa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, huku baadhi ya wanakijiji wakichomewa nyumba zao. Vurugu hizo zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, zimewahusisha Wagogo na wafugaji wa jamii ya Kimasai, ambao chanzo chake ni ugomvi wa kugombania maji ya mifugo. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Elizabeth Kaganda, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na bado wanaendelea kuwasaka wahalifu wengine.
TANZANIA YASAINI MIKATABA SABA NA CHINA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Na Mwandishi Maalumu, Guangzhou
SERIKALI ya Tanzania imeingia mikataba saba na kampuni sita za China yenye thamani ya Sh trilioni 2.72, zitakazowekezwa katika ujenzi wa miradi ya umeme na nyumba za makazi na biashara. Makubaliano ya uwekezaji huo yameingiwa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mawaziri wengine wa Serikali baada ya kusainiwa kwa mikataba saba ya uwekezaji katika sekta hizo muhimu kwa uchumi wa nchi.
MAALIM SEIF ATANGAZA KUWANIA URAIS 2015
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema atagombea urais hadi nguvu zitakapomuishia katika maisha yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)