Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akitoka kwenye Banda la Wizara yake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin Rutageruka na kulia ni Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christina Mwangosi. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo kuangalia hali ya usalama. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(TanTrade), Jacquline Maleko akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (wapili kushoto), Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu (kushoto) na Kamishna wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) jinsi Mamlaka hiyo kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi walivyojipanga kuimarisha usalama katika
Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (aliyevaa tai) akiongozwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soko la Ndani, Edwin Rutageruka (watatu kulia) kuelekea kuangalia usalama katika sehemu mbalimbali ya Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba). Nyuma ya Waziri Chikawe upande wa kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (wapili kulia). Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo.
Msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
wakizunguka katika viwanja vya Sabasaba katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya
Biashara yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Waziri Chikawe
na Maafisa wa Jeshi la Polisi wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam, kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili
kulia) akikiangalia cheti cha usajili wa vyama katika Banda la Wizara yake
wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea
Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu. Waziri Chikawe na Maafisa wa Jeshi la Polisi
wametembelea viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam,
kuangalia hali ya usalama katika viwanja hivyo. Kushoto ni Afisa Sheria, Flora
Mlope ambaye alikuwa akitoa maelezo ya usajili wa vyama. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment