Sheikh Mkuu ,Mufti Shabaan bin Simba
SIKU chache baada ya Sheikh Mkuu ,Mufti Shabaan bin Simba kutangaza
uongozi mpya wa msikiti wa Ijumaa na msikiti wa Quba iliyopo jijini
hapa ,sheikh wa msikiti wa Qiblatan ,Sood Ally Sood(37)uliopo
Kilombero jijini hapa,amelipuliwa na bomu la kurushwa kwa mkono
nyumbani kwake wakati akila daku na kujeruhi vibaya.
Aidha mbali na Sheikh huyo,mtu mwingine aliyekuwa nyumbani
kwake,aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini
Dar es salaam naye amejeruhiwa vibaya na wote wamelazwa katika
hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya matibabu.
Sheikh alijeruhiwa upande wa miguu yake yote miwili na mapajani huku
Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole
vya miguu yote miwili.
Akizungumza hospitalini hapo sheikh,Sood alisema tukio hilo lilitokea
nyumbani kwake eneo la majengo ya chini ,usiku wa kuamkia jana majira
ya saa 5 wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula
sebuleni .
Alisema alishangaa kusikia mlio mkubwa ulioambatana na vyuma
mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ,ambapo bomu hilo linaelezwa
kuwa ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu
wasiofahamika kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumbani katika
nyumba hiyo .
‘’hawa watu kimsingi wanafahamika maana walishawahi kunitishia kupitia
waraka wa maandishi pamoja na kunifyatulia risasi ‘’alisema
Alisema kuwa siku tatu kabla ta tukio hilo alikoswakoswa kwa kupigwa
risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na kutoa taarifa
katika kituo kikuu cha polisi jijiji hapa juu ya tukio hilo,hata
hivyo kuna baadhi ya vijana anawatuhumu juu ya matukio hayo.
Sood ambaye ni kiongozi Alswasun kanda ya kaskazini amekuwa
akitofautiana na waamini wenzake kutokana na msimamo wake mkali wa
kutokukubaliana na makundi ya kigaidi yanayojiita jihadi ,yanayotokana
na vijana wenye msimamo mkali yaliyopo ndani ya msikiti huo.
Akizungumzaia tukio hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo
alikemea matukio mbalimbali yanayotokana na ulipuaji wa mabomu na
kueleza kuwa viashirio vya matukio haya yanatoka ndani ya mkoa wa
Arusha hasa mahusiano mabaya ya waumini na viongozi wa misikiti.
Mulongo alisema matukio ya mabomu yanayoendelea jijini hapa,jeshi la
polisi linawashikilia baadhi ya watuhumiwa ,hivyo wale ambao
hawajakamatwa ndio hasa wanaoendelea na matukio haya na jeshi la
polisi linawasaka kwa udi na uvumba ili watafikishwa kwenye vyombo vya
sheria.
Naye kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatusi Sabasi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa hali za majeruhi bado
wanaendelea na matibabu huku polisi wakifanya uchunguzi juu ya tukio
hilo, alitoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili
kuwabaini wahalifu.
Kwa upande waka mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,alitaka jeshi la
polisi kurejesha amani jijini hapa kwa kulichukuliwa kwa umakini suala
hili ili wananchi waondoe hofu walionayo kutokana na majaribu
yanayojitokeza na kugarimu maisha ya wananchi wasio na hatia.
Aliongeza kwa kuwataka wananchi wajikite zaidi kwenye maombi na
waondoe tama mbalimbali za kutaka madaraka .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment