Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anashikiliwa akihojiwa kutokana na tuhuma za kufanya ushawishi kuhusu kesi inayochunguzwa ya matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi uliopita.
Bwana Sarkozy anashikiliwa Nanterre, karibu na mji mkuu Paris, katika tukio la aina yake dhidi ya rais huyo wa zamani wa Ufaransa.
Hali ya sasa hivi inaonekana pigo katika jaribio la Bwana Sarkozy kuwania kiti cha urais mwaka 2017.Mwanasheria wa Bwana Sarkozy, alihojiwa Jumatatu kuhusu tuhuma za kutafuta taarifa za ndani kuhusu kesi inayomkabili kiongozi huyo wa zamani.
Wachunguzi wanajaribu kutafuta iwapo Bwana Sarkozy, mwenye umri wa miaka 59, ambaye alikuwa rais wa Ufaransa kutoka mwaka 2007 hadi 2012, aliahidi kumpa wadhifa mkubwa jaji wa Monaco, Gilbert Azibert, ikiwa ni shukrani ya kupatiwa taarifa kuhusu uchunguzi unaofanyika dhidi kuhusu fedha aliyoitumia katika kampeni ya uchaguzi.
Wanachunguza madai kwamba Bwana Sarkozy alionywa simu yake ilikuwa inadukuliwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa fedha zilizotumika katika kampeni.
Bwana Azibert, mmoja wa majaji waandamizi katika mahakama ya rufaa, aliitwa kuhojiwa Jumatatu. Jaji mwingine Patrick Sassoust, naye pia alihojiwa, kama ilivyokuwa kwa mwanasheria wa Bwana Sarkozy, Thierry Herzog.
BBC
No comments:
Post a Comment