Na Daniel Mbega
SIKU kama ya leo, yaani
Julai Mosi, mwaka 1990 Afrika ilikaribia kuvunja rekodi yake ya Kombe la Dunia
wakati wawakilishi wake, Cameroon (Simba Wasiofugika), walipocheza kwa umahiri
mkubwa mechi yao ya robo fainali dhidi ya England.
Mechi hiyo iliyofanyika
kwenye Uwanja wa San Paolo jijini Naples huko Italia mbele ya watazamaji
55,205, ilichezeshwa na mwamuzi Edgardo Codesal wa Mexico aliyesaidiwa na Vincent
A. Mauro wa Marekani na Jassim Abdulrahman Mandi wa Bahrain na ilishuhudia
kandanda safi lililoonyeshwa na Cameroon, ingawa baadaye penalty zikaiathiri
katika muda wa ziada na England kuibuka na ushindi wa 3-2.
Ndiyo mechi pekee ya robo
fainali ambayo ilikuwa na goli zaidi ya moja, kwani England ilishinda kwa mabao
3-2 baada ya dakika 120.
England ndiyo iliyoanza
kupata bao kupitia kwa David Platt katika dakika ya 25. Lakini baada ya
mapumziko mkongwe Roger Milla akaingizwa dakika ya 61 na kuubadili mchezo ndani
ya sekunde tano ambapo Cameroon walipata penalti iliyofungwa na Emmanuel Kunde.
Baadaye katika dakika ya
65, Eugene Ekeke akafunga bao la kuongoza. Waafrika wakajua wanakwenda nusu
fainali, lakini wakasababisha penalti ambayo ilifungwa na Gary Lineker katika
dakika ya 83.
Mchezo ukaingia kwenye muda
wa ziada na katikati ya muda huo wa ziada, England wakapata penalti nyingine katika
dakika ya 105 ambayo ilifungwa na Lineker na wakafuzu kwa nusu fainali.
Vikosi vya siku hiyo
vilikuwa: England: Peter Shilton, Stuart Pearce, Des Walker, Terry Butcher
(nahodha) Trevor Steven 73’,
Chris Waddle, Gary Lineker, John Barnes/Peter Beardsley 46’, Paul Parker, Mark
Wright, David Platt, na Paul Gascoigne ‘Gaza’. Kocha alikuwa mzalendo Robert Robson.
Cameroon: Thomas Nkono, Emmanuel
Kunde, Stephen Tataw (nahodha), Benjamin Massing, Bertin Ebwellé, Thomas Libiih,
Emmanuel Maboang Kessaky/Roger Milla 46’, Jean-Claude Pagal, Louis-Paul Mfédé/ Eugène
Ekéké 62’, François Omam-Biyik, na Cyril Makanaky. Kocha alikuwa Valeri
Nepomniachi wa Urusi.
Waliopewa kadi za njano kwa
Cameroon ni Benjamin Massing 28’, Thomas Nkono 104’ na Roger Milla 119’, na kwa
England ni Stuart Pearce 70’.
Mechi nyingine iliyochezwa
siku hiyo ni kati ya Ujerumani Magharibi na jirani zao Czechoslovakia ambapo Ujerumani
walishinda kwa bao 1-0 la mkwaju wa penalti wa Lothar Matthäus katika daika ya
25.
Mchezo huo ulifanyika San
Siro jijini Milan mbele ya watazamaji 73,347 na ulichezeshwa na Helmut Kohl wa Austria.
Siku kama ya leo Julai
Mosi, lakini mwaka 19950 katika fainali zilizofanyika kule Brazil, wenyeji waliibuka
na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yugoslavia katika hatua ya makundi (raundi ya
pili) wakiwa Kundi la Kwanza.
Katika mchezo huo uliofanyika
Estádio do Maracanã, jijini Rio de Janeiro na kuhudhuriwa na watazamaji 142,000
ukiwa chini ya uchezeshaji wa Benjamin Griffiths wa Wales, mabao ya washindi
yalifungwa na Admeir(Ademir Marques de Menezes) 4’ na Zizinho (Thomaz Soares
da Silva) 69’.
Siku kama ya leo mwaka 1982
kule Hispania kulikuwa na michezo miwili ya makundi ya raundi ya pili ambapo
katika Kundi A Ubelgiji ilichapwa bao 1-0 na Urusi pale Camp Nou jijini
Barcelona mbele ya watazamaji 45,000 mwamuzi akiwa Michel Vautrot wa Ufaransa. Bao
la washindi lilifungwa na Oganesian dakika ya 48.
Kwenye Kundi D, Austria na
Ireland zilifungana mabao 2-2 katika Uwanja wa Estadio Vicente Calderon jijini
Madrid mbele ya mashabiki 20,000 ambapo mwamuzi alikuwa Adolf Prokop wa
Ujerumani Mashariki.
Mabao ya Austria yalifungwa
na Pezzey 50’ na Hintermeir 68’ wakati Hamilton aliifungia Ireland mabao yote
mawili dakika za 27' na 75'.
Tarehe kama ya leo mwaka
2006 kule Ujerumani wakati wa hatua ya robo fainali, Brazil ilichapwa na
Ufaransa bao 1-0 lililofungwa na Thierry Henry katika dakika ya 57 kwenye
Uwanja wa Stadion Frankfurt mbele ya mashabiki 48,000, mwamuzi akiwa Luis
Medina Cantalejo wa Hispania.
Katika mchezo mwingine war
obo fainali siku hiyo, Ureno ilisonga mbele kwa mikwaju ya penalty dhidi ya
England baada ya matokeo ya daika 120 kuwa 0-0.
England ilipata penalty
moja tu kupitia kwa Hargreaves wakati
Lampard, Gerrard na Carragher wakikosa, na Ureno ilipata penalty tatu kupitia
kwa Simão, Postiga na Ronaldo. Waliokosa ni Viana na Petit. Mchezo huo
ulifanyika kwenye Uwanja wa Gelsenkirchen mbele ya watazamaji 52,000 na
ulichezeshwa na Horacio Elizondo wa Argentina.
No comments:
Post a Comment