Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya
saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha,
ambapo watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la Polisi limewakamata
watuhumiwa 25 kwa uchunguzi.
Kufuatia uchunguzi huo kati yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa
watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni: SHAABAN MUSSA MMASA @
JAMAL, Umri miaka 26 Kabila, Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo
kwenye mgahawa huo.
Wengine ni ATHUMAN HUSSEIN
MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese
uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio na MOHAMED NURU @
MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese
jirani na eneo la tukio.
Mwingine ni JAFFAR
HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet
Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha.
Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
Wengine
ni ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba;umri wa miaka 31, Mmanyema wa
Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha, SAIDI MICHAEL TEMBA;umri
wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha. Aidha tarehe 21/07/2014
majira ya saa 20.00 usiku maeneo ya Sombetini walikamatwa YUSUFU HUSSEIN
ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA ,
kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa
walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi sita za shortgun,
mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi
moja. #
Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini
mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote
jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
Uchunguzi
wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya milipuko unaendelea, ikiwa
ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi na
kuwakamata watakao bainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa matokeo
ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila
mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo
la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya
ulipuaji mabomu nchini.
Zawadi nono itatolewa
kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu
huyu. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa
wanaoutoa.
IMETOLEWA NA ISAYA MNGULU-CP
MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA
No comments:
Post a Comment