Timu mbili za mwisho za Afrika katika kombe la dunia zimendoka dimbani baada ya kushindwa katika awamu ya timu bora kumi na sita.
Nigeria walicharazwa na Ufaransa mbili bila huku Algeria ikiangushwa na Ujerumani mabao mawili kwa moja katika muda wa ziada.
Algeria na Nigeria walijitahidi kadri ya uwezo wao kuingia katika awamu ya robo fainali ingawa mambo yalikuwa magumu.Ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika kwa timu mbili kufika awamu ya kumi na sita bora katika kombe la dunia.
Timu hizo mbili zilionyeshwa mlango baada ya kutofanya vyema. Algeria waliwapa wakati mgumu wachezaji wa Ujerumani ingawa mabao ndiyo yalikataa kuingia.
Katika muda wa ziada walichapwa mabo mawili ingawa walifanikiwa kuingiza bao moja kabla ya muda kumalizika. Matumaini ya kusonga mbele yakaisha.
Katika mechi yao, mabingwa wa Afrika, Nigeria walikula kichapo cha mabao mawili bila dhidi ya Ufaransa na baada ya mechi kumalizika, kocha wa timu yao Stephen Keshi akajiuzulu.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment