Kocha mkuu wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi (katikati) akiongea na Hassan Mwasapili (kushoto) na Richard Peter (Kulia)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976
DUNIA imepandwa na `mzuka bab kubwa` wa kutaka kujua nini timu nyingine ya Amerika (Argentina) itafanya katika mchezo wa leo wa nusu fainali ya pili ya kombe la dunia dhidi ya Uholanzi ya Van Gaal.
Argentina ikiwa na Lionel Messi inatarajiwa kufuta machozi ya Waamerika baada ya wenyeji Brazil kutandikwa kipigo cha kihistoria cha mabao 7-1 na Ujerumani.
Wakati kila mtu akiisubiri mechi hiyo kwa hamu, klabu ya Mbeya City fc iliyoleta ushindani mkubwa wa ligi kuu inatakiwa kufanya mambo muhimu kwa ajili ya kuendeleza mafanikio yake.
Msimu uliopita Mbeya city chini ya kocha bora wa Msimu, Juma Mwambusi ilishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 49 na kuiacha Simba katika nafasi ya nne.
Yanga walishika nafasi ya tatu na Azam fc walitwaa ndoo kwa mara ya kwanza katika historia yake.
Nafasi ya tatu kwa klabu changa kama Mbeya City yalikuwa mafanikio. Ugeni wa wachezaji katika michuano ya ligi kuu uliathiri kwa baadhi ya mechi kubwa kama ile dhidi ya Yanga, Simba na Azam fc.
Ligi kuu iligeuka kuwa maarufu zaidi kutokana na ujio wa Mbeya City fc.
Sasa timu hii inaelekea kucheza msimu wake wa pili. Miaka ya 80, Tukuyu Stars walipanda ligi kuu na kutwaa ubingwa, lakini msimu uliofuata walishuka daraja.
Baadhi ya watu wanadiriki kuwatabiria Mbeya City hali hii. Lakini ni mapema kusema yanaweza kutokea.
Mpaka sasa klabu hii inayomilikiwa na Halmashauri ya jiji haijaanza mazoezi rasmi. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba wanatarajia kuanza maandalizi julai 15 mwaka huu.
Beki wa Mbeya City fc, Hassan Mwasapili akichuana na Erasto Nyoni wa Azam fc msimu uliopita katika dimba la Sokoine.
Hawajafanya usajili mkubwa kwasababu sera yao haiwaelekezi kusajili wachezaji wengi wakongwe, wanajali soka lao la vijana. Wamemnasa mshambuliaji, Them Felix `Mnyama` kutoka kwa `wanankulukumbi ` Kagera Sugar.
Juma Mwambusi amebainisha kuwa kwasasa anaangalia uwezekano wa kusajili viungo wa ukabaji ili kuimarisha kikosi chake.
Mbeya City ni moja ya klabu niliyotarajia iingie kambini mapema kama walivyofanya Azam fc, na Ruvu Shooting.
Kusoma zaidi makala hii bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment