Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot
ARUSHA: IMEELEZWA kuwa endapo kama nchi ya Tanzania itaendelea kujikita katika majibizano ya kisiasa zaidi basi nchi uchumi wa nchi utaendelea kuyumba hali ambayo itasababisha pia maendeleo kuwa duni.
Kwa sasa katika vyombo vya habari kitu kikubwa kinachosikika ni majibizano ya kisiasa na wala sio ya maendeleo sasa kama nchi itaendelea hivi baada ya miaka michache ni wazi kuwa bado umaskini utatawala sana.
Kauli hiyo imetolewa na askofu wa kanisa la International Evangelism Dkt Eliud Isangya,lililopo Sakila wilayani Meru wakati akiongea na wanafunzi, walimu na walezi wa chuo hicho kwenye maafali ya 63 ya chuo hicho yaliyofanyika jumamosi iliyopita.
Dkt Isangya alisema kuwa haipendezi sana kuona kuwa nchi inajibizana kwenye siasa na kuacha masuala ya msingi ambayo yanagusa tija za wananchi na hivyo sasa wana siasa wanatakiwa kujiangalia kwenye hilo.
"Unakuta wakati mwingine muda wa majibizano ya kisiasa ni makubwa sana kuliko yale ya maendeleo sasa hali hiin inatupa wakati mgumu sana sisi kama viongozi wa dini hawa wanasiasa wanatakiwa kubadilika na kuachana na hilo," aliongeza Dkt Isangya.
Pia alisema kuwa Nchi ya Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kubwa sana kwani asilimia kubwa ya mahitaji yake bado hayajaweza kutekelezwa hivyo wanasiasa wanatakiwa kutumia muda huo huo katika kutafuta ufumbuzi wa hayo yote.
Alisisitiza kuwa kama watafanya hivyo basi hata uchumi wa nchi ya Tanzania utaweza kubadilika kwa kiwango cha juu sana tofauti na sasa ambapo nguvu kubwa sana imeelekezwa kwenye majibizano lakini hata bajeti kubwa kwa ajili ya kujibu hoja za kisiasa tofauti na hoja zile za maendeleo ya wananchi.
Nao wahitimu wa chuo hicho walisema kuwa pamoja na kuwa wameweza kupata elimu bora lakini kuna umuhimu mkubwa sana wa Serikali kuangalia changamoto ambazo wanazipata hasa za miundo mbinu kwani wakati mwingine zinasababisha mvutano mkubwa sana.
"pamoja na kuwa hapa tumepewa elimu bure kabisa na hata elimu za kijamii lakini kama barabara kutoka kikatiti ingekuwa nzuri basi tungefurai zaidi kwa sasa hii barabara inatupa wakati mgumu sana na sisi tungepata elimu wengi zaidi basi nchi ingekuwa na mabadiliko ya kutosha"waliongeza wahitimu hao.
No comments:
Post a Comment