Kikao cha baraza la mawaziri cha usalama kimekaa kwa mara ya pili nchini Israel tangu miili ya vijana watatu wa Israeli ipatikane katika eneo la West Bank hapo jana.
Kabla ya kuingia kwenye kikao hicho, waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, aliapa tena kuwasaka wale waliowauwa vijana hao na kukabiliana na kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas, analolilaumu kuhusika na mauaji hayo.
"kwanza kuwafuata wale wote waliohusika katika utekeji nyara . Yeyote aliyehusika na mauaji ataadhibiwa ipasavyo. Hatutapumzika wala kutulia hadi tumpate mhusika wa mwisho na haijalishi ni wapi watajalibu kujificha'', alieleza Netanyahu.
Kundi la Hamas limekana kuhusika na mauaji hayo. Tarifa zaidi zinasema kuwa mawaziri wa Israeli walikuwa na hoja tofauti juu ya kuchukuliwa kwa hatua yoyote walipokutana jana.
Miili ya vijana watatu imezikwa katika eneo la kati la Israeli, ambapo maelfu ya raia wa Israeli walihudhuria , akiwemo Bwana Netanyahu na rais wa Israeli , Shimon Peres.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment