Katibu mkuu wa Tucta Bw. Nicolous Mgaya (Kushoto) akitoa
hoja mbele ya waandishi wa habari
Shirikisho la Vyama Vya
Wafanyakazi Tanzania(Tucta)limeitaka serikali kutoka tamko kuhusu mustakabali
wa elimu nchini baada ya kujitokeza kwa kauli mbili tofauti zinazowachanganya
wananchi
Akizungumza Jijini Dar
es Salaam,Katibu Mkuu wa Tucta,Nicolaus Mgaya alisema kuwa, kujitokeza kwa
kauli hizo mbili tofauti kunaonyesha wazi kuwa, serikali imeshindwa kujipanga
wakati wa kutekeleza majukumu yake, jambo ambalo linawafanya kutoa kauli
zinazokinzana.
“Kitendo
cha serikali kutoa kauli mbili tofauti katika suala nyeti la elimu kunaonyesha
wazi kuwa wameshindwa kujipanga,hivyo basi wanaweza kuiangamiza elimu kwa
vijana wetu,”alisema Mgaya.
Alisema
kuwa, hali ya elimu nchini ni mbaya ikilinganishwa na kipindi kilichopita,jambo
ambalo linasababisha kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaoshindwa kufanya
vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.
Alisema
kuwa,hakuna nchi yoyote duniani ambayo itatoa matokeo ya mwisho ya wananchi
bila ya kuwepo kwa waliofaulu na waliofeli,kwa sababu matokeo hayo yanaleta
changamoto kwa wanafunzi waliofanya vibaya kujituma zaidi ili waweze kufanya
vizuri kwenye mitihani inayofuata.
Kwa
mujibu wa Mgaya,kutokana na hali hiyo, serikali ilipaswa kushirikiana na wadau
mbalimbali wakiwemo wa elimu ili kujadili mustakabali wa elimu,hasa katika
Nyanja ya walipotoka na waendako, jambo ambalo lingeweza kusaidia kupata maoni
ambayo yanatoweza kuboreshwa na kuleta mabadiliko katika sekta hiyo.
Alisema
kuwa kutokana na hali hiyo, maoni hayo wangeweza kuwa mwongozo mpya ambao
ukitumiwa vizuri utaweza kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani
yao.
Alisema
kuwa kutokana na hali hiyo,wananchi wangeweza kuona utofauti wa hali halisi ya
elimu kwa vijana wao,jambo ambalo lingeweza kuleta maendeleo.
Alisema
kuwa, kutokana na hali hiyo, wanapaswa kujifunza kwa yale yaliyotokea na kuanza
mchakato wa kushirikisha wadau ili waweze kuleta mapinduzi katika sekta ya
elimu ambayo itasaidia uboreshaji wake katika Nyanja mbalimbali ya sekta hiyo.
CHANZO, PT BLOG
No comments:
Post a Comment