Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza mwamlima akionesha eneo ambalo linagawiwa kwa vijana na kujihakikishia zoezi linafanikiwa
Wazazi wa watoto waliogawiwa ardhi wakiwa katika picha ya pamoja wakinyosha mikono juu na kupongezi zoezi hilo.
(Picha zote na Kibada wa Kibada –Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mpanda)
………………………………………………………..
Na Kibada Kibada, Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima amezindua zoezi la ugawaji ardhi kwa vijana wasiokuwa na ardhi Wilayani humo ili iweze kuwasaidia katika shughuli za uzalishaji kuliko kukaa kijiweni na kufanya shughuli zizokuwa na tija na kujiingiza katika vitengo vya uhalifu.
Uzinduzi huo umefanyika kwenye kitongoji cha Sijonga kilichoko Kijiji cha Kabungu Tarafa ya Kabungu wilayani Mpanda na ni zoezi litakaloendelea katika maeneo yote ya Wilaya ya Mpanda ili kuhakikisha vijana wasiokuwa na ardhi wanapatiwa ardhi na wazazi wao .
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa jumla ya vijana ni 262 kutoka katika Kata za Mwesevijana 42, Mpanda ndogo vijana 50, Karema vijana 82, na Kata ya Kabungu wapo vijana 90.
Katika ugawaji huo kila kijana atapatiwa kuanzia ekari tatu na kuendelea kulingana na eneo alilokuwa anamiliki mzazi wake na limekaa tu bila kutumiwa.
Akifafanua zaidi alieleza kuwa Mkoa wa Katavi ni moja ya Mikoa iliyojaliwa kuwa na fursa za kila aina, ardhi ya kutosha yenye rutuba, madini,maziwa, misitu minene, mbuga ya wanyama lakini ni Mkoa ambao wananchi wake ni masikini sana wakati kuna kila kitu cha kuwawezesha kuwa matajiri.
“Hakuna sababu yeyote ya Mwananchi wa Mpanda na Mkoa wa Katavi kuwa masikini, ardhi nzuri tunayo, tuitumie. Tunapokuwa masikini wakati ardhi tunayo mungu anachukia”. Alisema Mkuu wa Wilaya Mwamlima.
Awali Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kagwira Zamda Mheka ambaye pia ni Afisa Ugani wa kijiji hicho alieleza kuwa katika kijiji chake vijana 90 wamegawiwa mashamba kutoka katika vitongoji vinavyounda kijiji cha Kabungu na Kitongoji cha Sijonga.
Hata hivyo pamoja na kufanikiwa kwa zoezi hilo zipo changamoto kadha zilizojitokeza kutoka kwa baaadhi ya wazazi kusema kuwa kugawa ardhi wakati bado wako hai na ni sawa na kujitangazia kifo .
CHANZO,FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment