JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi ya Diaspora Tanzania (Tanzania Diaspora Initiative-TDI), unalenga kuwahamasisha Watanazania wanaoishi ughaibuni wenye utaalamu na mitaji kurudi nchini au kuwekeza katika shughuli mbalimbali kwa madhumuni ya kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, wenye kaulimbiu “Unganisha, Shiriki, Toa taarifa na Wekeza” (Connect, Engage, Inform and Invest) utatoa nafasi kwa washiriki kutambua vyema fursa za uwekezaji na ajira zinazopatikana Tanzania.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es salaam
13 Agosti, 2014
No comments:
Post a Comment