Siku
ya Jumapili tarehe 10 Agosti 2014 kilifanyika kikao cha mashauriano
kuhusu Mpango Kabambe wa Uendelezaji Mji Mpya wa Kigamboni
kilichojumuisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Prof. Anna Tibaijuka (Mb), Waheshimiwa Madiwani, Maofisa Watendaji Kata,
Mbunge wa Kigamboni na wadau wengine. Mhe. Waziri alielezea kuwa lengo
la kikao hiki ni pamoja na kutoa elimu kuhusu suala la hisa na kutaka
kuwashawishi Madiwani na Mbunge kulikubali suala hili na pia kutoa
taarifa ya vikao vya “Public Hearing” alivyotaka kuanza kuvifanya kwenye
kata mbali mbali za Jimbo la Kigamboni kuanzia tarehe 24-29 Agosti,
2014.
MAELEZO YA MHESHIMIWA WAZIRI
Mhe.
Waziri alitumia muda mwingi “kutoa darasa” kuhusu suala la hisa,
umuhimu wake na jinsi wananchi wa Kigamboni “watakavyobaki kwenye ardhi
yao kupitia hisa”.
MAMBO YALIYOJITOKEZA KATIKA MJADALA HUO
Washiriki
wa kikao walionyesha kutoridhishwa na utekelezaji wa Mradi wa Mji Mpya
wa Kigamboni. Washiriki wa kikao walimweleza Mhe. Waziri kuwa wananchi
wa Kigamboni wanataabika kwa muda wa miaka sita sasa. Wananchi
hawajengi, hawakarabati, hawauzi na wala hawakopesheki. Vile vile
washiriki walionyesha wasi wasi kuhusu suala la hisa na kutaka hisa iwe
ni hiari. Washiriki wa kikao walimtahadharisha Mhe. Waziri kuhusu
kufanya mikutano kwenye kata nyingine za Jimbo la Kigamboni kabla ya
kutatua matatizo
ya Uvumba na Kifurukwe katika Kata ya Kibada kwanza. Vile vile walitaka kujua kama fedha ya kulipa fidia ipo kwa wananchi wa Uvumba na Kifurukwe ziko tayari. Mimi kama Mbunge, nilihoji uhalali wa suala la hisa kwa kuuliza maswali yafuatayo:
ya Uvumba na Kifurukwe katika Kata ya Kibada kwanza. Vile vile walitaka kujua kama fedha ya kulipa fidia ipo kwa wananchi wa Uvumba na Kifurukwe ziko tayari. Mimi kama Mbunge, nilihoji uhalali wa suala la hisa kwa kuuliza maswali yafuatayo:
1. Ni sheria ipi inayotumika kufanya suala la hisa kuwa ni lazima kwa wananchi wa Kigamboni?
2.Ni
lini wananchi waliridhia kukatwa asilimia 10 ya fedha zao za fidia kwa
ajili ya hisa? Kwa nini isiwe pungufu au zaidi ya kiwango hiki?
3.Hizo fedha watakazokatwa toka kwa wananchi zitaenda wapi?
3.Hizo fedha watakazokatwa toka kwa wananchi zitaenda wapi?
4. Chombo cha kusimamia hisa hizo kilianzishwa lini na kwa sheria ipi?
5. Usimamizi wa chombo hicho ukoje?
6. Fedha hizi zitatumikaje?
7.Masuala
ya gawio yatakuwaje? Vile vile, niliunga mkono mawazo ya Washiriki wa
kikao kuwa Wizara ijikite zaidi kwenye eneo la Kifurukwe na Uvumba kabla
ya kwenda maeneo mengine.
Aidha, nilimkumbusha Mhe. Waziri kuhusu kutekeleza maagizo mbalimbali kama yafuatayo:
1. Kurudisha mrejesho kwa Baraza la madiwani la manispaa ya Temeke juu ya hoja walizozitoa katika kikao chao cha mwisho na Mhe. Waziri
1. Kurudisha mrejesho kwa Baraza la madiwani la manispaa ya Temeke juu ya hoja walizozitoa katika kikao chao cha mwisho na Mhe. Waziri
. Jambo hili halijatekelezwa hadi hivi sasa.
2.Maagizo
ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kupitia
kwenye hotuba yake katika mkutano wa 15, kikao cha 20 cha Bunge
kilichofanyika tarehe 28 Mei 2014. Kamati ya Bunge ilitoa maagizo kwa
Wizara na kutaka maelezo ya utekelezaji ya maagizo hayo kuwasilishwa
kwenye Kamati hiyo. Maagizo haya hayajafanyiwa kazi.
3. Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati anahitimisha bajeti ya Wizara yako alisema yafuatayo:
“Mheshimiwa
Mwenyekiti, nataka niseme tu kwamba, niliposikiliza taarifa ya kamati
na kama mtaona Taarifa ya Kamati na kama mtaona ukurasa wa 22 na 23 na
zile kurasa za mwisho kwenye hitimisho, yapo mawazo ambayo nafikiri ni
mazuri sana. Kinacholeta tatizo hapa inaonekana pengine Serikali
hatujafanya kazi ya kutosha katika kuelimisha jamii juu ya mradi
wenyewe, namna utakavyosimamiwa, utakavyoendeshwa na kubwa zaidi dhana
hizi mpya za hisa, unajua ni dhana ambazo zinahitaji elimu ya kutosha.
Hata haya mambo mengine ambayo yanadaiwa hapa ya kutoshirikishwa na
kadhalika, kwa sababu yamesemwa hapa ndani ya Bunge, mimi nadhani jibu
sahihi tukubali
Tukubaliane
na aliyosema Mheshimiwa Ndugulile pamoja na Waheshimiwa Wabunge wengine
kwamba, acha Serikali jambo hili tulichukue upya, tupitie maeneo yote
ambayo Waheshimiwa Wabunge wameyasema, tutashirikisha Wabunge wenyewe na
zile Wizara zote ambazo zinahusika,
Kubwa ni Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Temeke, maana eneo hili mpende msipende, ni eneo ambalo lipo chini ya Manispaa hiyo. Tulichofanya ni kuchukua eneo kwa madhumuni ya uendelezaji, lakini hatuwezi kuacha lile Baraza bila kulielimisha kiasi cha Kutosha (Makofi). Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nikuhakikishie, na niwaombe wenzangu kwamba, Serikali acha ilipe uzito unaotakiwa, naamini tutafikia mahali pazuri tu bila tatizo kubwa (Makofi)"
Kubwa ni Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Temeke, maana eneo hili mpende msipende, ni eneo ambalo lipo chini ya Manispaa hiyo. Tulichofanya ni kuchukua eneo kwa madhumuni ya uendelezaji, lakini hatuwezi kuacha lile Baraza bila kulielimisha kiasi cha Kutosha (Makofi). Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nikuhakikishie, na niwaombe wenzangu kwamba, Serikali acha ilipe uzito unaotakiwa, naamini tutafikia mahali pazuri tu bila tatizo kubwa (Makofi)"
Nilimhoji
Mhe. Waziri kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya Bunge na
maagizo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu yamefikia wapi? Ni lini yatatekelezwa?
Kwani kuendelea hatua nyingine za utekelezaji wa Mradi pasipo
kutekeleza maagizo ya Kamati ya Bunge na Waziri ni kuonyesha dharau kwa
mamlaka ya Taasisi ya Bunge na Ofisi ya Waziri Mkuu.
MAJIBU YA WAZIRI
1.Mhe.
Waziri alikubali kuwa suala la hisa litakuwa ni hiari. Alikiri kuwa
hadi sasa hakuna chombo cha kusimamia hisa za wananchi na kwamba suala
hili litajulikana baada ya wataalam washauri wa Wizara wakakapomaliza
kazi ya kuandaa prospectus”.
2. Mhe. Waziri alikubali kusitisha mikutano kwenye kata nyingine na kujikita zaidi kwenye mitaa ya Uvumba na Kifurukwe.
3.
Waziri alikiri kuwa kwa sasa hana fedha ya kutosha kuwalipa wananchi
wote waliokubali kufanya uthamini kwenye mitaa ya Kifurukwe na Uvumba.
Ikumbukwe kiasi cha Tsh 32 Billioni kinahitajika kulipa wananchi 228
ambao ni sehemu ya wananchi zaidi 2000 waliokubali kufanya tathmini.
Wizara hadi sasa ina kiasi cha Billioni 9 tu.
MAKUBALIANO
1.
Suala la hisa liwe ni la hiari. Wananchi waelimishwe na waamue kujiunga
kwenye mfumo wa hisa kwa hiari yao. Kusiwepo na masharti ya kulazimisha
ukataji wa hisa kabla ya kupokea fidia.
2.
Mikutano ya Public Hearing isitishwe na badala yake nguvu za Wizara
zielekezwe kwenye eneo la Uvumba na Kifurukwe ili mafanikio ya maeneo
haya yatoe hamasa kwa wananchi wa Kata nyingine.
3. Utelekezaji wa maazimio haya uende sambamba na utekelezaji wa maelekezo ya Kamati ya Bunge na maagizo ya Waziri Mkuu.
HITIMISHO
Nawaomba
wananchi wa Kigamboni, hususan Uvumba na Kifurukwe kuendelea kuwa
wavumilivu wakati tunaendelea kufanyia kazi makubaliano haya na maagizo
mengine yaliyowahi kutolewa na vyombo vingine ambayo hayajatekelezwa na
Wizara hadi hivi sasa.
Dkt Faustine Ndugulile (MB)
JIMBO LA KIGAMBONI
No comments:
Post a Comment