TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Demokrasia bila mipaka ni ukichaa na demokrasia bila nidhamu ni uwendawazimu” Mwl Jk Nyerere
Ndugu
zangu Watanzania, naomba mfahamu kuwa miongoni mwa wajumbe wote wa
bunge la katiba takriban 600, wajumbe waliofanya maamuzi haramu ya
kugomea ni 79 ambao ni pungufu ya asilimia 15% ya wajumbe wote, na sio
kweli kuwa wao pekee ndio wenye tafsir sahihi ya rasimu. Wajumbe wa
makundi mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa vyama vyote vya siasa
takriban 18 kati ya 22 bado wamo kwenye bunge, kati ya wajumbe wa kundi
la 201 walioasi ni 15 ambapo bara ni 9 na zanzibar 6 lakini pia katika
wanaojiita UKAWA wapo wabunge ambao wameendelea kurudi bungeni kwa
kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
Takwimu
hizi zinatuthibitishia kuwa UKAWA ni kikundi kidogo cha watu
waliojipanga kuvuruga AMANI ya nchi, watu ambao hawataki KATIBA wala
hawataki MUUNGANO.
Ndugu zangu watanzania,
naomba leo niwape picha na kilichopo nyuma ya pazia ya kikundi hiki
kiitwacho ukawa ambacho kinaratibiwa na viongozi wachache na maslahi
yake kujulikana kwa wachache zaidi tena yaliyojikita katika misingi ya
kibinafsi.
Mfano, ndoa ya CUF na CHADEMA
inayopelekea NCCR mageuzi kuwa bendera fuata upepo imejengwa katika
misingi ya kuvunja muungano, kwa makubaliano kuwa CUF kubaki na Zanzibar
na CHADEMA kubaki na Tanganyika. CUF inataka inufaike na mkakati
dhalimu wa kunyonya rasilimali za wazanzibar yakiwemo mafuta bila
kushurutishwa na sheria za muungano kwani wakiamini kubaki na muungano
imara CUF na viongozi hao wachache katika chama hicho wanakosa fursa za
kupora rasilimali za wazanzibar. Ikubumbukwe Muungano ndio unalinda
mipaka na usalama wa raia katika kujiendeleza na kujinufaisha bila
ubaguzi wa kikundi cha watu wachache ambacho kinaenda kinyume na utawala
wa sheria.
Ikumbukwe kuwa rasimu ya CUF
walioipeleka kwa Mhe. Raisi mwaka 2011, mapendekezo yao ni tofauti na
madai yao sasa ya serikali 3, hapa inatosha kutupa picha kuwa nia yao ni
kuvunja muungano ili watuache katika mfarakano kama nchi nyingine
zinazoteseka kwa sababu ya wanasiasa uchwara.
Ifahamike
ajenda ya CHADEMA ni kuvunja muungano ndio maana CHADEMA hawahangaiki
kuimarisha chama Zanzibar, nia yao ni kubaki na Tanganyika ili waigawe
Tanganyika katika vipande vipande kwa lugha ya majimbo ili adhima yao ya
ukanda na ukabila itimie. Moja ya kanda yao ambayo wametangaza katika
kanda 8 walizo nazo ni Kilimanjaro, tanga, arusha na manyara. CHADEMA
ina amini kanda hii inajitosheleza kwani ina bandari,bunga za
wanyama,madini, milima . Na hii imepelekea mbunge mmoja wapo wa CHADEMA
kulazimika kusema kaskazini ni nchi huru huku mwenyekiti wao Mbowe
akiendelea kudai mapato ya mlima Kilimanjaro yabaki Kilimanjaro.
Katika
kipindi hiki ambacho wenzetu wamegomea bunge la katiba ambalo lipo
kisheria na madai yao yakibadilika kila kunapokucha tena yakiwa na
upotoshaji mkubwa kwa kufanya siasa chafu ili mradi watimize azma ya
kuisambaratisha Tanzania wakiwa makuwadi wazuri wa soko huria. Ukihoji
leo sababu iliyowafanya watoke bungeni ni tofauti kabisa na sababu
waliyoitoa siku wanatoka bungeni, eti msingi wao mkuu wao ni watetezi wa
wananchi. Lakini tumesikia katika vyombo mbalimbali wananchi hao
wakiwaasa na wakiwataka warejee bungeni ili kukamilisha kazi ya kisheria
na tumaini la watanzania la kuwapatia katiba mpya.
UKAWA
hawa bila haya wamekataa. Swali..? wanamtumikia nani. Mpaka sasa
imepelekea wananchi hao wanaosema wanawawakilisha wameamua wenyewe kuja
Dodoma kuendelea kusema kero zao na shida zao ili katiba hii iweze kutoa
majawabu, mfano tumeshuhudia makundi ya wakulima, jukwaa la wahariri wa
vyombo vya habari, wafugaji na makundi kadha wa kadha yameendelea
kutiririka Dodoma. Hii ni picha tosha kuwa UKAWA hawawatumikii
watanzania na wameamua kuwahadaa watanzania kwa mgongo wa kuwatetea huku
ajenda yao ikiwa maslahi binafsi.
Ndugu zangu
watanzania tunapowaunga mkono watu wanaoendelea kuligomea bunge la
katiba wakati tunajua nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria, na wao ndio
wamevunja sheria, tujue kabisa kuwa tunaenda kinyume na utawala bora,
ambao umejengwa kwenye msingi wa sheria na demokrasia. Msingi wa
demokrasia sio kususa baada ya kushindwa hoja, UKAWA hawataki hoja za
wengine na wanalazimisha hoja zao pekee ndizo zikubalike kinyume na
msingi wa demokrasia. Na bila haya watu hao wasiojua demokrasia
wameendelea kuwashawishi watanzania waingie barabarani huku wakijua kuwa
Katiba haipatikani barabarani kama wanahoja kwanini wanaikimbia
Dodoma..? Mchakato huu ulianza kisheria na utahitimishwa kisheria, sio
matamko ya makuwadi wa soko huria.
Miongoni mwa
madai yao matatu, (i) Rais avunje bunge (2) kinachojadiliwa Dodoma sio
rasimu ya warioba (3) Serikali tatu ndio maendeleo
Kwa
ujumla wake, UKAWA wanajua mamlaka ya Rais kwa mujibu wa sheria ya
mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011, sura namba 83 imempa Rais mamlaka ya
kuunda tume, kuchagua wajumbe 201, kutangaza na kuitisha bunge na
kuzindua bunge la katiba, kupokea katiba inayopendekezwa na kuitangaza
kwenye gazeti la serikali.,kwanini wanataka kumlazimisha Rais kuvunja
Sheria kwani hayo niliyoyataja ndio ambayo Rais anayo mamlaka ya
kisheria kuyafanya katika mchakato huu wa Bunge la Katiba, na ndio maana
hata wale wajumbe aliowateua ambao wamegomea Rais hajawatengua.
,kinachojadiliwa
bungeni ni Rasimu ya jaji warioba na kiko wazi, kwa sababu msingi mkuu
wa majadiliano ni Rasimu inayotokana na tume tena kwa mujibu wa Sura
namba 83 kifungu cha sheria namba 25/26 na kwa mujibu wa kanuni za bunge
kifungu namba 33 (8). Wanajua mamlaka ya bunge na waliohusika
kutengeneza sheria hizi pamoja na kanuni waache kuwahadaa watanzania.
Jambo
la mwisho lenye kusikitisha zaidi ni kung’ang’ania Serikali tatu kana
kwamba ndio kilio kikubwa cha watanzania, naomba niulize swali kati ya
Muungano na migogoro ya ardhi ni jambo lipi limepoteza maisha ya
watanzania wengi na ambalo tunatakiwa kulifanyia kazi ili watanzania
wasiendelee kumwaga damu. Kati ya tatizo la ajira na muungano, kati ya
afya na muungano, kati ya maji salama na safi na muungano, kati ya elimu
bora na muungano, kati ya haki za binadamu na muungano eti watu hawa
wanaojiita ukawa kwao muhimu muungano kuliko chochote kile.Watanzania
naomba tupime kama ni kweli kuwa hawa ni watetezi wetu au ni makuwadi wa
soko huria.
Kwa niaba ya watanzania wazalendo,
napenda kuiomba serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama
kuwatupia UKAWA jicho la pekee katika kuangalia na kufuatilia kwa
ukaribu zaidi nyendo za UKAWA na hata kutuambia ni nani wako nyuma yao
kiasi cha kuwa na kiburi cha kupindukia. Wito wa watanzania kwa vyombo
vya ulinzi na usalama ni kuwa amani, umoja na uhai wa nchi hii uko
mikononi mwao, kwani nia ya UKAWA sio nzuri kwa mustakabali wa taifa
hili na lazima wakumbuke USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA na pia MAJUTO NI
MJUKUU NA HUJA BAADAE. UKAWA wanataka kutengeneza Misri, Afrika ya Kati,
Libya, Syria, Sudani Kusini nyingine hapa Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
PAUL MAKONDA
Katibu, Idara ya Hamasa na Chipukizi
Jumuia ya Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
No comments:
Post a Comment