TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kumb: 21 / 1435 AH Ijumaa, 26th Shawwal 1435 AH 22/08/2014 CE
MATESO, UKATILI NA UNYAMA KWA WAISLAMU WANAOTUHUMIWA KWA KESI YA ‘UGAIDI’ NI KUTOKANA NA UISLAMU WAO
وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلاَّ أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ (البروج:
“Nao hawakuona baya lolote kwao ila tu kwa kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa” (TMQ 85:8)
“Nao hawakuona baya lolote kwao ila tu kwa kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa” (TMQ 85:8)
Hizb
ut-Tahrir Afrika Mashariki inalaani kwa nguvu zote mateso, unyama,
udhalilishaji na ushenzi mkubwa wanayofanyiwa ndugu zetu Waislamu
wakiwemo masheikh, maustadh na wanaharakati wa Kiislamu walioko katika
kesi inayodaiwa ya ugaidi, kama walivyoeleza wenyewe karibuni mahkamani
jijini Dar es-Salaam na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Sisi
katikaHizb tunaweka bayana kwamba: mateso, unyama, ukatili na ushenzi
wanaotendewa ndugu zetu Waislamu hao na wengineo ni kwa sababu tu ya
Uislamu wao na si vyenginevyo. Kwa sababu kimsingi sheria ya kibaguzi
inayoitwa ya ‘ugaidi’ imelazimishwa na Marekani kwa ajili ya
kuwadhulumia Waislamu. Hizb inauliza kwa kinywa kipana pale viongozi wa
kanisa akiwemo Mchungaji Mtikila ambaye mara kwa mara huwekwa
korokoroni, kuhojiwa na Polisi hadi kufungwa jela. Jee kuna siku yoyote
aliwahi kufanyiwa ushenzi, mateso na unyama kama wanaofanyiwa ndugu zetu
hao Waislamu ?
Tunasema tena, vitendo hivi
vya mateso na dhulma ambavyo hufanyiwa Waislamu na vikosi maalumu kwa
agizo la Marekani sio mwanzo Tanzania wala sio mwisho. Bali vimeenea
duniani kote kuanzia katika kambi za mateso za Marekani za Guntanamo,
Balgram, Abu Ghuraib nk.
Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.
Aidha, mateso yaliyotajwa mahkamani hapo na Waislamu hao ni machache kuliko halihalisi ilivyo. Hususan kwa ndugu zetu waliobambikiziwa kesi kama hizo wakiwemo Waislamu wenzetu wa Arusha, Mwanza, Kenya nk.
Mateso haya
hutendwa kupitia vikosi maalum vinavyosimamiwa na Marekani vinavyoitwa
ati vya kupambana na ugaidi ambavyo licha ya kukosolewa, kukashifiwa,
kufedhehewa na kulaumiwa vikali hadharani kwa uovu wao kama ilivyofunua
taarifa ya tarehe 18/08/2014 ya Mashirika ya Utetezi la Haki za binadamu
kwa kikosi cha ATPU cha kupambana ugaidi nchini Kenya.
http://hizb-eastafrica.com/ swa/index.php?option=com_ content&view=article&id=1470% 3Aje-hamuogopi-mungu- mkakomeka-na-maovu-yenu&catid= 30%3Akwa-vyombo-vya-habari& Itemid=127
http://hizb-eastafrica.com/
Pamoja
na fedheha hizo za hadharani kutoka kwa taasisi zao wenyewe, bado
vikosi hivi vinaonekana kujigubika uziwi na kuendeleza maovu, dhulma,
mateso na udhalilishaji wa wazi kwa Waislamu.
Vitendo
hivi ni miongoni mwa dalili nyingi za kudhihirisha udhaifu na fedheha
kubwa kwa mfumo wa kibepari. Kwanza, kutokuwa na muundombinu thabiti wa
ukusanyaji ushahidi, kama kuna ushahidi kamwe katika kesi na badala yake
kutegemea utesaji. Pili, dhihirisho la kukosekana uzito shauri/ kesi
husika kiasi cha vikosi hivi kumalizia chuki na ghadhabu zao kwa
watuhumiwa kwa kuwatesa. Kwa kuwa wana yakini hakuna kesi
itakayoendelea. Tatu, dhana ya kitoto na ndoto za mchana za bwana wao
Marekani na mfumo wake wa wa kikafiri wa kibepari kudhani ati kuwatesa
Waislamu kutawatisha Umma wa Kiislamu waache na waogope uwajibu wao wa
kuhubiri na kutangaza dini yao ya haki. Marekani na vikosi vyake
vinavyoitwa vya kupambana na ugaidi wanaelea katika ndoto za mchana na
kugubikwa na ujinga wa kutojua historia wakidhani kuwa Uislamu
utamalizika kwa kuteswa Waislamu. Lau ingekuwa ndoto yao hiyo ndio
uhalisia, basi Uislamu leo usingetajwa kamwe katika uso wa ulimwengu. Na
nne, ni kushindwa watetezi wa mfumo wa kibepari kutetea mfumo wao kwa
hoja na dalili. Badala yake katika kutapatapa na khofu ya kumalizika
mfumo wao huwa hawana namna ila kutesa Waislamu. Kwa kuwa kimaumbile
ubepari hauwezi na hautoweza kujitetea kwa hoja za kidini wala za
kiakili. Kimsingi umezaliwa kwa ajili ya kufa! Na punde InshaaAllah
utatupwa katika jalala la kihistoria. Kwa kuwa hauna manufaa kwa
ubinaadamu zaidi ya madhila na kushindwa juu ya kushindwa.
Umeshindwa
ubepari katika siasa ukidai kuna demokrasia kumbe ni nidhamu ya
udanganyifu na matajiri. Hudai katiba itokane na watu kumbe tayari wana
katiba yao mfukoni, umeshindwa kiuchumi kwa kuongeza msururu wa makodi
na umasikini, huku makampuni ya kibepari yakipora rasilmali kwa baraka
za wanasiasa waovu na mikataba ya udanganyifu, umeshindwa katika upande
wa kijamii kwa kupitia fikra chafu za ‘uhuru’ (freedoms) kwa kuongeza
maovu na mabalaa mbali mbali kwa mwanadamu kuanzia ulevi, zinaa, kupigia
debe vitendo viovu vya ushoga, usagaji nk.
Na vitendo hivi vya utesaji na udhalilishaji Waislamu katika mchakato wa kisheria ni kushindwa kuliko dhahiri kukosekana kinachoitwa utawala wa sheria na udhaifu katika taasisi za mahkama za kusimimia haki na sheria. Ajabu na aibu kubwa! wanashindwa hata kusimamia sheria walizozitunga kwa mikono yao ! Basi nini cha kutarajia kutoka mfumo huu zaidi ya damu na machozi !
Na vitendo hivi vya utesaji na udhalilishaji Waislamu katika mchakato wa kisheria ni kushindwa kuliko dhahiri kukosekana kinachoitwa utawala wa sheria na udhaifu katika taasisi za mahkama za kusimimia haki na sheria. Ajabu na aibu kubwa! wanashindwa hata kusimamia sheria walizozitunga kwa mikono yao ! Basi nini cha kutarajia kutoka mfumo huu zaidi ya damu na machozi !
Baada
ya yote hayo Hizb inawasisitiza Waislamu kuendelea kuulingania Uislamu
wao bila ya khofu wala woga kwa njia ya Mtume SAAW ambayo haihusishi
utumiaji wa nguvu wala mabavu. Pia wafedhehi kila aina ya vitendo vya
dhulma wanavyotendewa Waislamu, na kuachana na michakato yote ya siasa
za kikafiri za kidemokrasia , zikiwemo katiba zake na chaguzi zake. Kwa
kuwa ni haramu na zaidi ndio zinazodhamini kupatikana watawala
wanaosaidia kudhuru Waislamu.
Aidha,
tunawafariji ndugu zetu na Waislamu jumla kwa madhila haya na mengineyo.
Lakini pia tunawapa Waislamu bishara ya ushindi wa Umma wetu chini ya
kivuli cha dola tukufu ya Kiislamu ya Pili ya Khilafah Rashidah. Dola
hiyo haitosahau dhulma hata yenye ukubwa wa punje ya hardali
aliyotendewa Muislamu ila itamhukumu dhalimu. Na lau madhaalimu
wataondoka duniani kabla ya kurejea dola hiyo. Pia hawatosalimika wala
kunusurika na adhabu ya Muumba ambae kamwe hajawasahau, hasahau wala
hatosahau na dhulma yao.
وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ (إبراهيم: 42
“Na wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na yale watendayo madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao.” (TMQ 14: 42
وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ (إبراهيم: 42
“Na wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na yale watendayo madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatakapokodoka macho yao.” (TMQ 14: 42
Masoud Msellem
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Hizb-ut Tahrir Afrika Mashariki
Tovuti Rasmi ya Hizb ut- Tahrir
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info
www.hizb-ut-tahrir.org
Tovuti ya Afisi ya Habari
www.hizb-ut-tahrir.info
No comments:
Post a Comment