Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 29 August 2014

RAIS KIKWETE KUHUTUBIA TAIFA JUMAPILI


Rais Jakaya Kikwete anatarajia kufanya ziara mkoani hapa ambako atazindua  miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya barabara, maji na kulihutubia Taifa kwa kuongea na wazee.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, alisema Rais ataanza ziara mwishoni mwa wiki hii  kulihutubia Taifa mwishoni mwa mwezi huu Jumapili ijayo. 

Kwa mujibu wa Nchimbi, Rais Kikwete ataanza ziara yake katika wilaya ya Kongwa ambako ataweka mawe ya msingi na kufungua miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Akiwa wilayani Kongwa, atapokea  madawati kutoka  shirika la misheni na kuyakabidhi katika shule ya msingi.

Kisha atafanya mkutano wa hadhara Kibaigwa wilayani humo,  kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Mbandee-Kongwa  inayojengwa kwa  kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 14.

Siku itakayofuata Rais Kikwete atafungua mradi wa maji katika wilaya ya Mpwapwa mradi ambao unahudumia wakazi wa kijiji cha Chunyu, kuweka jiwe la msingi katika daraja la Gulwe na kuzungumza na wananchi.

“Rais kwa mara ya kwanza atahutubia Taifa akiwa mkoani Dodoma siku ya Agosti 31 na katika Wilaya ya Dodoma mjini, atakuwa na siku mbili katika siku ya kwanza atazungumza na wazee wa Dodoma jioni,” alisema Dk. Nchimbi

Alisema Rais pia, atafungua mradi wa makazi ya Mkuu wa wilaya ya Chemba na ofisi yake katika wilaya ya Chemba na pia katika wilaya ya Kondoa ataweka jiwe la msingi katika barabara ya Mayamamaya-Kondoa, kuzindua ukumbi wa mikutano wa halmashauri na kuongea na wananchi.

Aidha alisema katika wilaya ya Dodoma mjini Rais Kikwete atafanya ziara ya siku mbili ikiwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa kuboresha huduma za maji manispaa ya Dodoma na katika wilaya ya Chamwino na Bahi na kwamba vile vile, atafanya shughuli mbalimbali za uzinduzi.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment