Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 18 August 2014

TAASISI, MASHIRIKA NA WADAU WATAKIWA KUWEZESHA WAJANE NA YATIMA


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog


Arusha: TAASISI na mashirika  mbalimbali nchini pamoja na jamii zimehamasishwa kuhakikisha kuwa zinawawezesha  wajane na yatima katika kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili waweze kujikwamua na hali ngumu ya maisha inayowakabili.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa asasi ya wajane na yatima Tanzania (TOWA) ,Frida Silayo wakati akizungumzia kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili huku wakikosa mitaji kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.
Alisema kuwa,jamii imekuwa ikiwasahau sana wajane na yatima ambao wamekuwa wakiishia kuomba tu kutokana na kukosa mitaji na watu wa kuwawezesha katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha na hivyo wengi wao kuishia kuwa omba omba tu.
Frida alisema kuwa,wao kama wajane wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi sana za kimaisha ikiwemo kudhulumiwa haki zao za msingi huku wakikosa mtetezi na hivyo wengi wao kuishia kuishi maisha ya kuomba omba tu.
"Sasa kutokana na hali hiyo tulifikia hatua  ya kuanzisha asasi yetu ambayo itakuwa ikishughulikia haki zote za wajane na yatima katika shida zao ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuomba wafadhili  na wadau mbalimbali katika kuwawezesha na hatimaye kutatua changamoto zao," alisema Frida.
Alisema kuwa, asasi hiyo imekuwa ikilenga zaidi kuwapa wajane na yatima matumaini, kuwapa elimu ya kujua haki zao za kisheria, na kuwawezesha kwa njia ya miradi ili hatma yake wajitegemee wenyewe na kuweza kuendesha miradi yao wenyewe na kuziendeleza familia zao.
Naye Katibu wa asasi hiyo Fatuma Ramadhani alisema kuwa, kupitia asasi hiyo  kutawezesha kabisa kutokuwepo kwa wajane na yatima ambao watakuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kulingana na mwitikio wa wadau na taasisi katika kuwasaidia na kuwawezesha kupitia asasi yetu.
Fatuma aliwataka wadau mbalimbali  kujitokeza kwa wingi kuwasaidia wajane na yatima ili waweze kuondokana na changamoto hizo kimaisha kwani hawana msaada wowote.

No comments:

Post a Comment