Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 29 August 2014

HIZI NDIZO NJIA TANO ZA KUEPUKA VIRUSI VYA EBOLA!

Njia za kuepuka kuambukizwa Ebola
Ebola:Njia tano za kujiepusha virusi hatari vya homa ya Ebola
Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.
1. Sabuni na majiMadaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi:
Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha.
Hili huwa jambo gumu kwa wanaoishi kwenye makazi duni, na walio vijijini ambako aghalabu maji safi hayapatikani moja kwa moja- lakini ni mbinu iliyothibitishwa ya kuua virusi vya Ebola.
Osha mikono kwa sabuni na Maji
Unachohitaji tu ni sabuni ya kawaida.
Kusalimiana kwa mikono kunafaa kuepukwa kwa ujumla, daktari Unnis Krishnan wa Plan International aliarifu BBC, kwani Ebola husambazwa haraka watu wanapowasiliana ana kwa ana na maji maji ya kimwili ya waliougua.
Dalili ya ugonjwa huu huchukuwa muda kabla ya kudhihirika.
Tumia njia zingine za kujuliana hali
2. Hakuna kugusana
Iwapo unashuku kuwa mtu ana Ebola, usimguse.
Inaokena kuwa si maadili mema unapoona unaowapenda wakihisi uchungu na unataka kuwakumbatia na kuwahudumia, lakini maji maji ya kimwili- mkojo na kinyesi, matapishi, kamasi, mate, machozi, na mbegu za kiume na majimaji ya uke- vyote huweza kueneza Ebola.
Dalili za mtu aliyeugua ni joto mwilini, maumivu kwa misuli na viungo, vidonda kooni, kuumwa na kichwa, na uchovu- kufuatiwa na kichefuchefu, kutapika, na kuharisha, ambapo mtu huweza kutoa damu pia.
Usimguse mtu anayeonesha dalili za ugonjwa
Tia watu hao moyo kutembelea kituo cha afya haraka iwezekanavyo.
Pia ni uamuzi mzuri usiguse nguo au malaza ya waliougua Ebola- na Medecins Sans Frontieres anashauri kuwa malazi ya waliougua yanafaa kuteketezwa.
3. Epuka miili ya wafu
Iwapo unadhani mtu amefariki baada ya kuugua Ebola, usiguse mwili wao, hata kama ni mila au desturi ya maziko.
Baada ya mtu kufa, bado unaweza kuambukizwa Ebola kutoka kwa miili yao kwani bado inatoa maji maji ya mwili ambayo huweza kuwa hatari zaidi hata kuliko ya mtu alieugua.
Fanya mipango kupata timu ya magwiji kushughulikia mwili huo haraka iwezekanavyo kwani ni hatari kuwacha mwili wa mfu kwa muda mrefu katika eneo la makazi.
Usile nyama ya porini
4. Usile nyama ya porini
Epuka kuwinda, kugusa, au kula nyama ya porini, kwa mfano popo, nyani na sokwe, kwani wanasayansi wanaamini kuwa hiyo ndiyo chanzo cha maambukizi kwa binadamu.
Hata kama mnyama fulani wa porini huliwa katika eneo lenu na nyama yake ni tamu epuka myama huyo kwani nyama yake au damu yake huweza kuwa na virusi hivyo.
Hakikisha vyakula vyote vinapikwa inavyostahili.
Usieneze uvumi kuhusu Ebola
5. Usiwe na hofu
Kueneza uvumi huongeza hofu.
Usiogope wafanyakazi wa huduma za afya- wako hapo kukusaidia na kliniki ndipo mahali mwafaka kwa mtu kuponywa- wataongezewa maji na kutulizwa maumivu.
Takriban nusu ya watu walioambukizwa Ebola kufuatia mzuko wa hivi punde wa Ebola walifariki.
Kumekuwepo na matukio ya madaktari kushambuliwa na watu kutorokwa wanaposhukiwa kuwa na Ebola- hata wakati wanaugua ugonjwa tofauti.
Kuamini matibabu ya kiasili ambayo hayajathibitishwa kutoa afueni, pia kumechangia ongezeko la kuenea kwa virusi vya Ebola.
"Kinga ndiyo jinsi bora zaidi ya kukabiliana na Ebola, hivyo basi wacha uvumi na usiwe na hofu; inawezekana kupunguza maumivu na kuokoa maisha,” daktari Krishnan asema.
Ugonjwa wa virusi vya Ebola (EVD):
Dalili za Ebola ni homa, kufuja damu na kuharibika kwa mfumo mkuu wa neva.
Epuka miili ya watu walioambukizwa Ebola
Maafa ya ugonjwa huu huweza kufika asilimia tisini- lakini mzuko wa hivi punde unasababisha maafa 55% .
Ugonjwa huo huchukua muda wa siku ishirini na moja kukomaa.

Hakuna kinga wala tibaHuduma za msaada na kudhibiti kupoteza maji mwilini kutokana na kuharisha au kutapika husaidia katika kuponaInafikiriwa kuwa popo ndo vilemea vya ugonjwa huo.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment