Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 25 August 2014

WATUHUMIWA WA UJANGILI WAOMBA KUFIKISHWA MAHAKAMANI


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

ARUSHA: Watuhumiwa wa kesi ya ujangili waliokamatwa  katika zoezi la Oparesheni Tokomeza wameiomba Serikali kuwafikisha mahakamani kwani mpaka sasa wameshatumia kiasi cha Milioni  80 wanatumikia kifungo cha nje
Watuhumiwa hao zaidi ya 20 wanatokea katika Wilaya za Meru, Longido, na Simanjiro na mpaka sasa baadhi ya shuguli za maendeleo ya jamii zimesimama huku pia wakiwa wanaishi kwa mashaka sana kwa kuwa hata silaha zao zimesimama.
Wakizungumza kwa niaba ya watuhumiwa hao Mwenyekiti wa Kijiji cha Orobomba Ndionona Ngeresa alisema kuwa walikamatwa toka mwaka jana mwezi wa kumi kwenye oparesheni tokomeza lakini kitu cha ajabu ni kuwa mpaka sasa hawajafikishwa mahakamani.
Alidai kuwa wanalazimika kutumia gharama kubwa sana kwa ajili ya kuripoti katika kikosi dhidi ya ujangili kwa kanda ya kaskazini (KDU) kwa kuwa Serikali imewataka waweze kuripoti kila baada ya wiki mbili kwa kuwa wanatumikia kifungo cha nje jambo ambalo sasa Serikali inatakiwa kuwangalia na kwa kuwa wanaonekana kuwa wanamakosa basi wafikishwe mahakamani.
Ngeresa alisema kuwa hapo awali walikuwa wanalazimika kutumikia kifungo cha nje ambapo walikuwa wanalazimika kuripoti katika kikosi dhidi ya ujangili Arusha kila baada ya siku mbili  jambo ambalo liliwasababishia hasara kubwa sana kwa kuwa wengi wao wanatokea katika Wilaya za Meru, Longido na Simanjiro.
Kutokana na hilo alisema kuwa baadaye viongozi wa kikosi hicho walilazimika kubadilisha utaratibu huo baada ya kuona kuwa wanateseka na ndipo walipolazimika kuwaambia kuwa wanatakiwa kuripoti katika
kikosi hicho kila baada ya wiki mbili kuisha hali ambayo nayo imesababisha hasara kubwa sana kwa wananchi ambao wanategemea huduma za viongozi wa kata, ibada, na hata familia.
"Sisi tumechoka sana na hii hali kwani tutaisha hivi mpaka lini alafu wale viongozi wa ngazi ya taifa waliokuwa kwenye oparesheni hii wameshashugulikiwa na serikali sasa kama sisi ni majangili basi tufikishwe mahakamani tukajibu mashitaka ambayo yanatukabili kuliko kupoteza kiasi kikubwa cha fedha," aliongeza Ngeresa.
Naye Mchungaji kiongozi wa kanisa la Apostolic Assembly kutoka Simanjiro, Mchungaji Allen Mweta ambaye pia ameshikiliwa katika oparresheni hiyo  alisema kuwa zoezi hilo la opareshini tokomeza
limekuwa na hasara kubwa  kwa kuwa mpaka sasa shuguli za kanisa lake zinayumba tofauti na hapo awali.
"Kanisa langu kule Simanjiro lina mambo mengi sana ya kuweza kuwasaidia wananchi mbali na huduma za kiroho lakini sasa nani ataweza kusimamia ilihali mimi kila mara nipo huku Arusha mimi ninachoomba
Serikali kupitia Wizara ya mali asili na utalii iweze kuangalia hili tunateseka sana na kama ni mahakamani basi tupelekwe tukaelezewe mashtaka yetu kwani hatujakutwa na chochote kile bali tumeonewa tu," aliongeza Mchungaji huyo.
Hata hivyo, Mkuu wa Kikosi Dhidi ya Ujangili Kanda ya Kaskazini, Pascal Mrina alisema kuwa malalamiko ya watuhumiwa hao 20 wa ujangili bado yanaendelea kufanyiwa kazi na kwa sasa kikosi hicho hakiwezi kuaamuru watuhumiwa hao wasiripoti kwa kuwa zoezi hilo la oparesheni tokomeza lilifanywa na ngazi za juu za Serikali.
Mrina alisema kuwa watuhumiwa wote hao walikamatwa katika opareheni hiyo na kwa sasa uchunguzi bado unaendelea na utakapokamilika kuanzia ngazi za juu basi sheria itaanza kuchukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment