Rais Barack Obama wa Marekani amesema mapigano yanayoendelea nchini Ukraine si matokeo ya kukua kwa maasi nchini humo bali ni uchochezi wa Urusi.
Amesema waandamaji nchini Ukraine wamekuwa wakifanya vitendo hivyo kutokana na uchochezi wa Urusi ambapo anadai kuwa nchi hiyo inahusika katika kuwasaidia silaha na gharama za fedha waasi hao.
Hata hivyo Rais Obama hajatoa mrejesho wa moja kwa moja kwa kile ambacho NATO wamekiita umuhimu wa kuongeza majeshi ya Urusi nchini Ukraine.
Obama pia ameionya Urusi kwamba kwa kufanya hivyo itakuwa gharama kubwa kwao na pia yaweza kuwasababishia hasara.
BBC
No comments:
Post a Comment