ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY (ACT – TANZANIA)
PRESS RELEASE,TAREHE 19 AGOST 2014
Ndugu
waandishi wa habari, awali ya yote napenda kuwashukuru kwa majukumu
yenu ya kila siku ya kuuhabarisha umma wa watanzania juu ya mambo mbali
mbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi yetu.
Ninyi
ni wadau muhimu katika suala zima la upashanaji habari na mmekuwa
mkitekeleza majukumu yenu pasipo upendeleo wala kuhofu jambo lolote,
zaidi ya kuongozwa na maadili yanayowaongoza kwa hili sisi ACT-Tanzania
tunawapongeza sana.
Ndugu
zangu wanahabari kama mnavyojua,ACT-Tanzania ni chama kinachojipambanua
katika misingi ya ukweli, uwazi uadilifu na uzalendo kwa ajili ya Taifa
letu adhimu la Tanzania na kwa misingi hiyo ndiyo maana leo tumewaiteni
kuwajulisha kile tunachorajia kufanya katika ujenzi wa chama hiki kwa
ajili ya kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Ndugu
wanahabari kuanzia kesho mwenyezi mungu akitujaalia uzima chama Cha
ACT-Tanzania kitaanza ziara kwa ajili ya kueneza na kukijenga chama hadi
katika ngazi za chini, katika azma hii tutafika katika majimbo 65
kwenye mikoa 15 ya Tanzania bara na ziara yote itatumia siku 27.
Ndugu
wanahabari katika ziara hii kutakuwa na makundi matatu yatakayogawanya
katika mikoa 15 ambapo kundi la kwanza litaongozwa na mwenyekiti wa muda
wa ACT-Tanzania Lukas Kadawi Limbu akisaidiwa na mjumbe wa Halmashauri
kuu Athuman Balozi na litatumia siku 17 kufika katika majimbo 22 kwenye
mikoa mitano
Mikoa
hiyo ni Shinyanga Geita,Mwanza Mara na Simiyu na huko watafanya
mikutano ya ndani na baadhi ya maeneo watafanya mikutano ya hadhara.
Kundi
la Pili litaongozwa na Makamu mwenyekiti akisaidiwa na Naibu katibu
mkuu Taifa na litafika katika mikoa ya Tanga,Pwani,Lindi na Mtwara na
huko watafanya mikutano ya ndani na ya hadhara kwa baadhi ya maeneo
ambayo hayajazuiliwa kwa mikutano ya hadhara kundi hili litatembelea
majimbo 15.
Ndugu
wana habari kundi la tatu litaongozwa na Katibu Mkuu Samson Mwigamba
atakayeambatana na Katibu wa mawasiliano na uenezi, kundi hili litafika
katika mikoa sita yenye jumla ya majimbo 28 na litatumia siku 27
Mikoa hiyo ni Singida,Kagera,Kigoma,Rukwa, Katavi na Tabora huko napo kutafanyika mikutano ya ndani na ya hadhara kwa baadhi ya maeneo.
Ndugu
wanahabari tunafanya ziara hizi kwa lengo la kukifikisha chama chini
zaidi kwa wananchi kama mpango mkakati wetu katika shughuli zinazopaswa
kufanywa kabla ya uzinduzi rasmi wa Chama,kwa hivi sasa Chama kipo
katika ngazi ya mkoa na kwa upande wa Tanzania bara tuna uongozi wa muda
katika mikoa yote isipokuwa katika mikoa ya Rukwa na Njombe na katika
mikoa hiyo miwili tayari kuna wanachama waliojiorodhesha kwa ajili ya
kuunda uongozi wa mikoa hiyo,hivyo katika ziara hii viongozi wa kitaifa
watakapofika Rukwa wataacha uongozi wa mkoa na majimbo huku taratibu za
kuupata uongozi wa mkoa wa Njombe zikiwa zinaendelea
Ndugu
wanahabari katika ziara hii tutahakikisha kila mahali tutakapopita
tunawafunza wanachama na viongozi misingi na imani ya ACT Tanzania kwa
ajili ya taifa la leo kesho na keshokutwa.
Mwisho
kabisa ACT-Tanzania tunawashukuru wanahabari kwa kutenga muda wenu na
kufika kusikiliza kile tulichowaitia,tunawatakia uwajibikaji mwema kwa
ajili ya Tanzania iliyo bora
Imetolewa leo na
Idara ya Mawasiliano na Uenezi
0687499466.
0687499466.
No comments:
Post a Comment