Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 20 August 2014

OFISI ZA SHIRIKISHO LA SOKA NIGERIA ZATEKETEA KWA MOTO

Moto wateketeza Ofisi za NFF Abuja
Moto mkubwa umetekeza makao ya shirikisho la soka la Nigeria NFF iliyoko Abuja.
Iliwachukua zaidi ya saa mbili kwa zima moto wakisaidiana na umma kuuzima moto huo mkubwa .
Katibu mkuu wa NFF bwana Musa Amadu amesema kuwa moto huo ulianzia katika afisi ya mhasibu wa shirikisho hilo.Afisa wa kuzima moto Eyo Ime ameiambia BBC kuwa wanashuku chanzo cha moto huo ulitokana na hitilafu ya umeme.
"Niliwasili kama kawaida lakini nikakatazwa kupanda ghorofa kwani tayari moshi ulikuwa unafuka ''
"Wafanyikazi wa shirikisho hilo wangeweza kuzima moto huo lakini walishindwa kuingia ofisini humo na hivyo hawangfeweza kubaini chanzo kikamilifu''
''Hata hivyo nashukuru mungu kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha yake kutokana na moto huo kwahivyo hakuna faida ya kumlaumu mtu yeyote''
Mwenyekiti wa NFF Aminu Maigari anakumbwa na tuhuma za uongozi duni
Mkasa huo wa moto ni pigo kwa shirikisho hilo ambalo tayari linakabiliwa na mvutano wa uongozi ambao umepelekea kung'olewa madarakani kwa mwenyekiti Aminu Maigari mara mbili akirejeshwa
Mabingwa hao wa Afrika hawana kocha hata kufikia sasa .
Afisi iliyoko sasa ingali haijatia sahihi makubaliano yeyote wala kandarasi na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Stephen Keshi ambaye aliiongoza timu hiyo kuenda kwenye kombe la dunia huko Brazil.

Keshi mwenyewe ameiambia BBC kuwa anatarajia kukamilisha mazungumzo kati ya saa 24 hadi 48 zijazo.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment