Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 15 August 2014

ITACHUKUA MIEZI MINGI KUIDHIBITI EBOLA

MSF inasema ni muhimu kudhibiti ugonjwa huo Liberia mwanzo
Mkuu wa shirika la madaktari wasio na mipaka la Medicins Sans Frontieres, amesema kuwa itachukua miezi sita kuweza kudhibiti janga la Ebola katika mataifa ya Afrika Magharibi.
Akizungumza mjini Geneva,mkuu huyo, Joanne Lui alisema kuwa uongozi mzuri unahitajika kutoka kwa shirika la afya duniani na kwamba kukabiliana na Ebola hasa ilikozuka mwanzo nchini liberia, ni muhimu zaidi katika kumaliza ugonjwa huo.
Bi Lui aliongeza matabibu 80 wamefariki kutokana na ugonjwa huo, huku watu wengine 170 wakiambakizwa na kwamba nyingi ya vituo vya afya vimefurika wagonjwa wa Ebola.Hasa amesisitiza kwamba wataalamu zaidi wenye uzoefu wa kupambana na ugonjwa hupo wanahitajika katika maeneo yaliyoathirika.
''Ikiwa hatutapambana na ugonjwa huo nchini Liberia,basi itakuwa vigumu kuudhibiti katika kanda nzima ya Afrika Magharbi,'' alisema Bi Lui.
Mifumo ya afya katika neo la Afrika Magharibi inakabiliwa na hali ngumu wakati huu wa mlipuko wa Ebola.
Ebola huambukizana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, kupitia maji maji ya mwili au damu.

Dalili kama za mafua zinaweza kusababisha mtu kuvuja damu kutoka kwenye sehemu zake za mwili kama vile masikioni, mapuani, machoni na ndani ya mwili na kusababisha viungo vya mwili kutofanya kazi.
BBC

No comments:

Post a Comment