Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 18 August 2014

TANZANIA INA UHABA WA WAHANDISI

Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

Arusha: TANZANIA inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa wahandisi jambo ambalo kwa sasa linatakiwa kuchukuliwa kama changamoto na kisha kutatuliwa ili kuweza kuharakisha maendeleo hasa ngazi za Halmashauri.
Hata hivyo, endapo kama nchi itakuwa na wahandisi wa kutosha basi itaweza kuchangia kwa kiwango kikubwa sana matatizo hasa katika ujenzi kutatuliwa tofauti na sasa idadi iliopo haitoshelezi kwa mahitaji halisi.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Arusha na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akifungua mkutano wa viongozi wa Halmashauri, mikoa na wahandisi kutoka katika maeneo mbalimbali nchini.
Pinda alidai kuwa mpaka sasa mahitaji ya wahandisi ni makubwa sana kuliko idadi ya watu walioko kwenye halmashauri zote hivyo basi kama nchi ingepata wahandisi wa kutosha zaidi wangeweza kusaidia katika shuguli mbalimbli.
"Natoa changamoto kwa bodi ya wakandarasi hapa nchini kufikiria namna ambayo tunaweza kuongeza idadi ya wakandarasi takwimu zinaonesha kuwa kwa sasa tuna wakandarasi kama 300 mahitaji ni mengi sana," aliongeza Pinda.
Wakati huo huo aliwataka wakandarasi hasa wa bodi za barabara kwenye ngazi za halmashauri kujiwekea utaratibu wa kusimamia maadili kwani wakati mwingine ukosefu wa maadili ya kutosha unasababisha hasara kwa serikali.
Nao wadau hao wa barabara walisema kuwa wana uwezo mkubwa sana wa kufanya vizuri endapo kama watapewa mahitaji muhimu pamoja na bajeti ambayo inatosheleza kwa wakati.
Wadau hao hasa wakandarasi walisisitiza kuwa kwa sasa bajeti inayotengwa na serikali kuu bado haitoshelezi ukulinganisha na mahitaji ya wananachi hasa maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment