BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
MCHAKATO WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
1.0 MAANDALIZI YA UTOAJI MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitangaza mwongozo na vigezo
vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 kupitia magazeti na
tovuti yake mnamo wezi Aprili 2014. Mwongozo huo, pamoja na mambo
mengine, uliainisha sifa za waombaji mikopo na ruzuku, vipengele vya
Mikopo, programu za vipaumbele kwa waombaji wa shahada ya kwanza,
shahada za uzamili na uzamivu waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya
juu zinazotambulika. Maombi ya mikopo kwa waombaji wapya yalifanyika kwa
njia ya mtandao kwa anuani yahttp://olas.heslb.go.tz au kupitia anuani ya tovuti ya Bodi ya Mikopo ambayo ni:www.heslb.go.tz.
Kulingana na Mwongozo wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa mwaka wa masomo 2014/2015, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilifungua maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS) kuanzia Aprili 23, 2014 na kuendelea kupokea maombi hayo hadi Julai 31, 2014.
Kulingana na Mwongozo wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa mwaka wa masomo 2014/2015, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilifungua maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS) kuanzia Aprili 23, 2014 na kuendelea kupokea maombi hayo hadi Julai 31, 2014.
Mabadiliko
machache yamefanyika, kubwa likiwa ni kwa wanufaika wanaoendelea na
masomo, tofauti na ilivyokuwa miaka iliyopita, hawakutakiwa kujaza tena
fomu kuthibitisha uhitaji wao wa mikopo kwa mwaka unaofuatia, isipokuwa
kwa wale ambao waliopenda kusitisha kuendelea kupokea mkopo kutoka Bodi.
Wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo wataendelea kupata mikopo
yao kulingana na viwango walivyopangiwa awali.
1.1 Maombi yaliyopokelewa
Jumla
ya maombi 58,037 yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia tarehe 31 Julai,
2014. Kati ya maombi hayo, jumla ya maombi 37,689 ni ya waombaji wa
kiume na maombi 19,592 ni ya waombaji wa kike. Uchambuzi zaidi wa
waombaji wa mikopo unaonyesha kuwa Waombaji wa kundi la diploma ya
ualimu wa sayansi ni 480 (Me – 324, Ke – 156), Waombaji wa shahada ya
uzamili/uzamivu (kwa vyuo vya ndani ya nchi) ni 276 (Me – 194, Ke – 82),
Waombaji wa shahada ya kwanza (kwa vyuo vya ndani ya nchi) ni 56,922
(Me – 37,460, Ke – 19,462), Waombaji wa shahada ya uzamili/uzamivu (nje
ya nchi) ni 126 (Me- 88, Ke – 38) na Waombaji wa shahada ya kwanza (nje
ya nchi) ni 233 (Me – 141, Ke – 92).
1.2 Uchambuzi wa MaombiBaada
ya kufungwa rasmi kwa kipindi cha kupokea maombi ya mikopo, hatua
inayoendelea kwa sasa ni uhakiki (verification) wa taarifa za waombaji,
kwa kuzipitia nyaraka mbalimbali zilizoambatanishwa na waombaji mikopo
ambazo ni cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma, vielelezo vya mdhamini,
saini ya mwombaji na mdhamini wake na ushuhuda wa Mwanasheria au Hakimu
kwamba vivuli vya nyaraka zilizowasilishwa kwenye Bodi ni halisi.
1.3 Upangaji wa mikopoMchakato
wa uchambuzi na upangaji wa mikopo utakamilika baada ya majina ya
wanafunzi waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kujiunga na
vyuo mbalimbali yanapowasilishwa rasmi kwenye Bodi ya Mikopo. Udahili wa
wanafunzi unafanywa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa mfumo wa pamoja wa
udahili (CAS) unaotumiwa na vyuo takribani vyote vya elimu ya juu
nchini. Kwa vyuo ambavyo havimo katika mfumo wa pamoja wa udahili (CAS)
hutuma TCU majina ya wanafunzi ambao vimewadahili ili waweze
kuthibitishwa kabla ya kupatiwa mikopo. Taarifa za udahili ni muhimu
katika zoezi la upangaji wa mikopo kwa kuwa zinatoa mwongozo wa gharama
halisi za programu za mafunzo. Wanafunzi wanaostahili na waliotimiza
masharti na vigezo vya ukopeshaji ndio hupangiwa mikopo kulingana na
bajeti iliyotengwa na Serikali.
1.4 Kutangazwa kwa majina ya wanafunzi waliopata mikopoMajina
ya wanafunzi waliopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye
tovuti ya Bodi na taarifa hiyo pia itatangazwa katika vyombo vya habari
ili kuwataarifu wadau wote ikiwa ni pamoja na wanafunzi, vyuo vya elimu
ya juu, wazazi na umma kwa ujumla. Nakala za majina ya wanafunzi
waliopangiwa mikopo zitatumwa kwenye vyuo husika.
2.0 WANAFUNZI WA MASOMO YA STASHAHADA YA UALIMU
Kwa kutambua umuhimu wa masomo ya Sayansi na kukabiliana na upungufu
wa walimu wa masomo hayo katika ngazi ya shule za Msingi na Sekondari, mwaka huu serikali imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya Stashahada maalum ya Ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
wa walimu wa masomo hayo katika ngazi ya shule za Msingi na Sekondari, mwaka huu serikali imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya Stashahada maalum ya Ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Wanafunzi
wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na Stashahada hii maalum katika
Chuo Kikuu cha Dodoma na wote watanufaika na mikopo ya wanafunzi wa
elimu ya juu.
3.0 HITIMISHO
Kwa
Taarifa hii, Bodi inapenda kuwataarifu wadau wote kuwa mchakato wa
utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 unaendelea vema.
Aidha,
Bodi inawasisitizia waombaji wa Mikopo, wazazi/walezi na umma kwa
ujumla kutambua kuwa Mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu ya
utekelezaji wa Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya juu na hivyo iwapo kuna
waombaji wanaoweza kujigharamia, wasiombe mikopo ili kutoa nafasi kwa
wahitaji wengi zaidi kunufaika.
Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
No comments:
Post a Comment