Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 15 August 2014

MCHUNGAJI MSIGWA AENGULIWA KUGOMBEA UENYEKITI WA CHADEMA WILAYA KWA KUKOSA SIFA

Mbunge Msigwa kulia akiwa na mbunge Chiku 
    Mchungaji Msigwa kushoto akiwa na Chiku Abwao katika moja ya  vikao  vya Baraza la Madiwani Manispaa ya Iringa 
Na Francis GodwingaBlog
 
KAMATI ya uchaguzi  wa mkuu wa  wilaya ya Iringa mjini  kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemuengua katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa wilaya hiyo mbunge wa  jimbo la Iringa mjini  mchungaji Peter Msigwa ambae ndie alikuwa wenyekiti anayemaliza muda wake kwa  kukosa sifa ya kutetea tena nafasi hiyo.
 
Hatua  hiyo ya  kuenguliwa kwa Msigwa  imekuja baada ya  wajumbe  kulalamikia hatua ya chama kushindwa kulipa kodi ya ofisi ya kata na ile ya wilaya pia ugomvi mkubwa uliopo kati ya mbunge Msigwa na mbunge mwenzake wa  viti maalum mkoa Chiku Abwao aliyekuwa akigombea nafasi ya kiti mkoa wa Iringa nafasi ambayo msigwa pia alitangaza kugombea .
 
Hivyo  kutokana na mvutano huo kamati  hiyo  iliyoketi usiku wa  leo  ukumbi wa Sambala mjini hapa ililazimika  kuchukua uamuzi mgumu wa kufyeka majina ya wabunge hao kugombea nafasi hizo ili  kunusuru  chama.
 
Mmoja kati ya makada wa  ambae alishiriki kikao hicho cha kumuengua Msigwa na Chiku alisema kuwa chanzo cha msigwa kuenguliwa ni kutokana na kuendekeza kukuza makundi ndani ya chama na kuwa mbali na chama zaidi ya kufanya chama  kuendelea kukosa heshima.
 
Makundi hayo yanaelezwa kukiwekwa rehani chama hicho wakati kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
 
Pamoja na Mchungaji Msigwa, taarifa hizo zimesema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) naye ameenguliwa kuwani nafasi yoyote ya uongozi katika chama hicho mkoani hapa.
 
Hivikaribuni Abwao alinukuliwa akitangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa chama hicho unaotarajia kufanyika Jumapili keshokutwa.
 
Kuenguliwa kwa Msigwa katika uchaguzi huo kumeacha kampuni wagombea wawili wanaomenyana katika nafasi hiyo itakayosaidia kutoa picha ya jinsi mambo yatakavyokuwa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea ubunge jimbo la Iringa Mjini mwaka 2015.
 
Wagombea hao ni Frank Nyalusi anayeelezwa kuwa ni mfuasi wa kufa na kupona wa Mchungaji Peter Msigwa na Mohamed Makuke ambaye ni mfuasi wa kundi la wengi linalodaiwa kumpinga Mchunngaji Msigwa.
 
Kundi linalojiita la wengi katika chama hicho limesikika likisema mara kwa mra kwamba tabia ya Mchungaji Msigwa ndani ya chama hicho inawaweka katika wakati mgumu wa kutetea nafasi ya ubunge mwaka 2015.
 
Mchungaji Msigwa ni kiongozi asiyeambilika, anayejua kila kitu, mbishi, kaidi, mwenye kiburi, asiyependa watu, mwenye visasi, majivuno na asiyetaka ushirikiano toka kwa wenzake, asiye na mikakati ya kujenga chama huku akiamini siasa za kitaifa pekee anazopenda zaidi zinaweza kulinusuru jimbo hili katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
 
Wakati Mchungaji Msigwa akirushiwa lawama zote hizo, taarifa za uhakika zimedai kwamba ofisi ya wilaya ya chama hicho imefungwa na wameamuliwa kuondoka baada ya uongozi wa mbunge huyo unaomaliza muda wake kushindwa kulipa kodi ya pango. Mchungaji Msigwa ndiye Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Iringa Mjini anayemaliza muda wake hii leo.
 
Wanachama wa chama hicho wamechukizwa kwa hatua ya mbunge wao kuridhia kupoteza ofisi pekee ya chama hicho mjini Iringa kwasababu ya kushindwa kulipa Sh 540,000 walizokuwa wakidaiwa.
 
Kwa upande  wake  mbunge Msigwa alinukuliwa na mwandishi wa habari  hizi akimrushia maneno  mmoja kati ya  viongozi wa  chama  hicho  kuwa  watu  wanamchafua kwa suala la ofisi na  kuwa  ni ruksa kwa  wanachama ambao  wanapenda vyama vyenye ofisi  kuhama chadema na  kujiunga na vyama  hivyo .
 
Huku mbunge Chiku Abwao amethibitisha kuenguliwa  kwao katika  nafasi hizo japo amedai  kwa  upande  wake kaonewa na ataendelea  kutumia vikao kuomba  kurejeshwa kwa  jina lake.

No comments:

Post a Comment