Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 29 August 2014

TAMKO LA MWENYEKITI WA CHADEMA ARUMERU ALIYEKIMBILIA ACT-TANZANIA


TAMKO LA NDUGU ERNEST E. SHESHE ALYEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA ARUMERU MAGHALIBI 26 AGOST 2014

Ninaitwa Ernest Sheshe. Nilikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA katika Jimbo la Arumeru Magharibi kuanzia mwaka 2009 hadi tarehe 25 Agosti 2014.
1. Niligombea nafasi ya uenyekiti tena katika uchaguzi wa chama unaoendelea. Nilishindwa kwa hila na Ndugu Gibson. Hila zenyewe ni pamoja na Mhe. Godless Lema kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo shilingi 30,000/= kila moja na kisha kuwaficha hadi siku ya uchaguzi. Aidha, wajumbe walipelekewa chakula mafichoni kilichobebwa kwenye gari ya mgombea mwenzangu, yote haya ikiwa ni kinyume na kanuni za uchaguzi ndani ya chama na Waraka Na.6 uliotolewa na Katibu Mkuu. Waraka huu, pamoja na mambo mengine, unapiga marufuku matumizi ya hongo ya aina yeyote katika chaguzi.
2. Siku moja kabla ya uchaguzi, Mhe. Godbless Lema aliwatangazia wanachama kwamba Mwenyekiti wao ni Gibson na ndiye atakayekuwa mgombea ubunge. Wagombea wengine wanaojipitisha ni mamluki na ni wasaliti wa chama na wananchi wa Arumeru.
3. Baada ya kutoridhika na matokeo ya uchaguzi kutokana na matukio ya hapo juu, nilikata rufaa kwa kuandika barua kwenye ngazi ya mkoa kama utaratibu unavyosema. Hata hivyo barua yangu ya rufaa ilipelekwa kwa Katibu wa Kanda Ndugu Amani Golugwa, ambaye ndiye aliyesimamia uchaguzi. Ndugu Golugwa ametamka wazi kwamba hakuna cha rufaa wala nini na kwamba yeye hajishughulishi na wasaliti na kwamba hiyo imetoka!
4. Mambo mengine yanayoendelea ndani ya chama katika Kanda ya Kaskazini ni:
a. Uongozi wa kanda hauko kikatiba na unafanya kazi kwa kuvunja katiba ya CDM
b. Mjumbe wa kamati kuu Godbless Lema ametengeneza chama ndani ya chama. Yeyote asiyekubaliana naye na asiye na hela hana thamani ndani ya chama. Nguvu yote hii ya Lema anaipata kutoka kwa mwenyekiti wa CDM taifa Freeman Mbowe kutokana na kwamba ni kabila lake.
c. Mhe. Godbless Lema ndiye anayepanga nani awe Kiongozi ndani ya chama na ndiye mwenye mamlaka ya kuamua nani atagombea ubunge katika uchaguzi ujao kwa majimbo ya Mkoa wa Arusha.
d. Katibu wa kanda Aman Gulugwa ni tatizo kubwa ndani ya CDM,anapenda kuburuza watu,hafuati katiba wala kanuni za uendeshaji wa chama.
5. Baada ya kutafakari hali ya mambo inavyoendelea ndani ya CDM, na kujiridhisha kwamba chama hiki kimetekwa na viongozi wachache na kuachana kabisa na misingi tuliokuwa tunaijenga, na kutokana na ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea, nimeamua rasmi kujiunga na chama kipya kinachoitwa ACT_Tanzania ambacho viongozi wake ni waadilifu na baadhi yao pia wamedhulumiwa haki zao ndani ya CDM. Kunzia tarehe tarehe 26 Agosti 2014 siku ya Jumanne mimi sio mwanachama na kiongozi wa CDM tena. Ninajiunga na wazalendo wa ACT-Tanzania.
6. Pamoja nami, tupo na wazalendo wengine 14 kutoka kata 14 za Jimbo la Arumeru Magharibi. Kuanzia kesho kutwa tutaanza kukisimika chama cha ACT-Tanzania katika kata zote za Arumeru Magharibi na tutashiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa kadri utakavyopangwa.

Ndimi Ernest E. Sheshe,
Mwanachama wa ACT-Tanzania,
Arumeru Magharibi.

No comments:

Post a Comment