JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TANGAZO KWA UMMA
MAPENDEKEZO YA MABORESHO YA MICHEPUO NA TAHASUSI ZA KIDATO CHA KWANZA MPAKA CHA NNE NA KIDATO CHA TANO NA SITA
Elimu ya sekondari katika ngazi ya Kidato cha Kwanza hadi cha Nne imekuwa ikiongozwa na michepuo ya ama ya Sanaa, Sayansi, Ufundi na Biashara. Halika dhalika, masomo ya sekondari Kidato cha Tano na Sita yamekuwa ya kifundishwa kwa kutumia Tahasusi mbalimbali kulinga na mahitaji ya nchi ambazo kwa sasa ni PCM, PCB, PGM, CBG, EGM, CBA, CBG, CBN kwa Sayansi, na HGL, HGK, HKL, KLF, ECA, HGE kwa Sanaa.
Mafanikio
mbalimbali yamepatikana kwa kutumia mfumo huu tangu ulipoanza hadi
sasa. Hata hivyo, kutokana na (a) nia ya nchi kupiga hatua zaidi katika
maeneo mbalimbali ya maendeleo ya nchi kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025, (b) mabadiliko ya mahitaji ya ulimwengu wa ajira na kazi
na (c) kuendelea kukua kwa ugunduzi na ubunifu pamoja na matumizi ya
Sayansi na Teknolojia katika maeneo mbalimbali, Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi imeona kuna umuhimu wa kupitia upya Michepuo na
Tahasusi zilizopo ili ufundishaji uweze kwenda na wakati. Michepuo na
Tahasusi hizo mpya zinatarajiwa kuanza kutumika katika mwaka wa masomo
2015/2016.
Ili
kufanikisha maboresho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
inakaribisha wadau wote wa Elimu na Mafunzo kutoa mapendekezo ya jinsi
gani Michepuo na Tahasusi za elimu ya sekondari ziundwe au kuanzishwa
katika madarasa ya kidato cha Kwanza hadi Nne na Tano hadi Sita. Mwisho
wa kutuma mapendekezo ni tarehe 31/10/2014. Wadau wote mnahamasishwa
kutoa maoni yenu kupitia njia mbalimbali ikiwemo vikao ama kwa
kuwasiliana moja kwa moja na wizara. Majumuisho ya mapendekezo ya
tawekwa kwenye magazeti na tovuti kwa maoni na hatua za mwisho katika
kukamilisha maboresho haya.
Mapendekezo ya Michepuo naTahasusi mpya yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
7 Mtaa wa Magogoni,
11479 DAR ES SALAAM.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
7 Mtaa wa Magogoni,
11479 DAR ES SALAAM.
Elimu Bora Inawezekana; Timiza Wajibu Wako
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
No comments:
Post a Comment