Bila
ya shaka kila mmoja wetu ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania
ameshtushwa kwa kiasi kikubwa baada ya kupata taarifa ya kunyanyaswa
vikali pamoja na kufanyiwa matendo ya kulawitiwa viongozi wa Jumuia ya
Uamsho Zanzibar.
Matendo
haya katika hali ya kiubinadamu hayafai kabisa na nidhahir kwa kila
mmoja wetu kuyapiga vita ili jamii na mataifa kwa ujumla wazisikie sauti
zetu juu ya viongozi hawa wakubwa wa Dini ya Kiislamu.
Tukiwa
kama taasisi kubwa ya hapa Tanzania Chama cha Wananchi CUF tunalaani
vikali ukatili na ushenzi uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya
viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na wenzao 19.
Kwa mujibu wa walivyoeleza watuhumiwa hao wakiwa Mahakama ya kisutu Shekh Farid Had
Ahmed na wenzake Jeshi la polisi limewafanyia ukatili wa hali ya juu usiostahili kwa binadamu.
Mahabusu
hao wanaozuliwa huko Daresalam wanadai kuhojiwa wakiwa uchi wa mnyama,
kulawitiwa na askari wa Jeshi la polisi, kuwekewa vitu vyenye ncha kali
kwenye sehemu za haja kubwa na mateso mengine mengi ikiwa ni pamoja na
kupigwa hadi kuumizwa.
Hata
kama ni wakosaji matendo haya ni kinyume na haki za binadamu hayapaswi
kufanyiwa binadamu kama hawa tena raia halali wa Nchi hii.
Tunauliza
ipo wapi haki ya kisheria ya mwananchi wan chi hii ikiwa jeshi la
polisi ndio wanaovunja sheria baada ya kulinda sheria?
Inashangaza
kuona vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Makaburu dhidi ya Watu weusi wa
Afrika Kusini sasa Vinafanywa na Vijana wa Kitanzania dhidi ya
Watanzania wenzao kwa kisingizio cha Ugaidi.
Sisi
CUF hatuoni mantiki ya uvunjaji wa Haki za Binadamu kwa kiasi hiki kwa
watu wanaotuhumiwa kwa kile kinachoitwa kujishirikisha na Matendo ya
Kigaidi.
Hata
kama watuhumiwa hao watatiwa hatiani kwa makosa hayo, bado hukumu yao
haitakua kulawitiwa kama ilivyoelezwa na mmoja kati ya Watuhumiwa hao
mbele ya Mahakama.
Polisi
mnapaswa kujua kwamba mnaowafanyia matendo hayo bado ni watuhumiwa tu
wa matendo ya ugaidi je wakishinda kesi na kuonekana hawana hatia na
nyinyi mchukuliwe hatua za kisheria?
Ikiwa
matendo hayo yanafanywa kwa makusudi na Jeshi la Polisi dhidi ya
Viongozi wa Dini ya kiislamu tena yenye asilimia 99 ya wakaazi wa
Zanzibar hivi munataka wafuasi wao na Familia zao wafanye nini ?
CUF-Chama
cha Wananchi kutokana na kauli mbiu yake ya ‘’haki sawa kwa wote’’
tunamtaka Rais kutoa kauli na Msimamo wa Serikali dhidi ya unyanyasaji
na udhalilishaji huu uliofanywa na Jeshi la Polisi ili Wananchi wapate
kujua hatua zitakazo chukuliwa na Serikali sambamba na kukubali Ombi la
Watuhumiwa la kufanyiwa uchunguzi wa Afya zao kama lilivyo wasilishwa
kwenye Mahakama inayosikiliza Kesi hiyo.
Tunatoa
wito kwa Taasisi za kimataifa na kitaifa zinazoshughulikia mambo ya
Uvunjwaji wa Haki za Binaadamu kufuatilia kwa Karibu suala hili na
kuchukua hatua zinazostahili vingenevyo siku moja wanaweza kushuhudia
maiti ikipelekwa mahakamani kama walivyodai watuhumiwa hao mbele ya
Mahakama ya kisutu.
Tumeshuhudia
malalamiko ya watuhumiwa hao kupitia vyombo vya habari wanasema kwamba
mpaka hivi sasa wale waliojeruhiwa bado wanaugulia maumivu na hawajapewa
matibabu yoyote yale licha ya kufanyia matendo makubwa ya kishenzi
wanaendelea kusota ndani tu hivi hamuoni kama hii ni hatari zaidi kwa
watuhumiwa hawa?
Tukiwa
kama wadau wakubwa wa Chama cha siasa hapa Nchini tuna imani kwamba
taarifa yetu hii itafanyiwa kazi na hatua za kisheria kuchukuliwa haraka
sana iwezekanovyo ili kuepusha majanga zaidi ndania ya Nchi yetu.
Chama
cha Wananachi CUF kinawaomba ndugu na jamaa pamoja na waislamu wote
Nchini kuendelea kuwa na subra tukiamini kwamba sheria itachukuliwa
dhidhi ya viongozi hawa.
Imetolewa na
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi CUF.
No comments:
Post a Comment