TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU MADAI YA TUME YA OPEREHSNI TOKOMEZA "KUKWAMA"
Gazeti la Mtanzania TOleo Na. 7547 la Jumatano taerhe 13 Agosti, 2014 ukurasa wa tano (5) liliandika habari iliyobeba kichwa cha habari "TUME YA OPERESHENI TOKOMEZA YAKWAMA". Kwenye ufafanuzi wa habari hiyo chanzo cha "kukwama" huko ni kutokana na kutokupatiwa fedha.
Tume inafafanua na kujulisha umma wa Tanzania kuwa habari hiyo haina ukweli wowote.
Taarifa sahihi ni kuwa Tume ilianza kazi mara tu baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya M. Kikwete na Serikali iliipatia ofisi rasilimali watu na rasilimali fedha.
Kwa mujibu wa mpango kazi, Tume imegawanya majukumu yake katika sehemu kuu mbili, kazi za ndani na kazi za nje ya Ofisi.
Kwa sasa Tumeinaendelea na kazi za ndani. Kwa hiyo sio kweli kwamba "imekwama" kama ilivyodiwa kwenye habari hiyo ya gazeti la Mtanzania.
Pindi kazi za ndani zitakapokamilika, Tume itaendelea na kazi za nje na hatimaye za ndani kwa mujibu wa mpango kazi wake.
Imetolewa na;
Frederick K. Manyanda
KATIBU WA TUME
13 Agosti, 2014
No comments:
Post a Comment