Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Thursday, 14 August 2014
DK. BILAL AWATAKA WANAFUNZI VYUO VIKUU KUFIKIRI KUJIAJIRI BADALA YA KUAJIRIWA
Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha: MAKAMU wa Rais, Dk Gharib Bilal amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuajiriwa badala yake watumie taaluma zao ili waweze kujiajiri wenyewe.
Bilal aliyasema hayo jana Jijini hapa wakati akifungua kongamano la sita la Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (TCU) kwakushirikiana naWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Alisema lengo kuu la jukwaa hilo ni kuangalia changamoto zinazozikabili vyuo vikuu nchini katika kuhakikisha zinaopatiwa ufumbuzi ili viweze kufikia viwango vikubwa zaidi katika sekta ya elimu hapa nchini.
Alisema Tanzania imepiga hatua kubwa katika malengo ya milenia yanayoishia mwaka 2015 lakini sekta ya elimu ni vyema ikapewa kipaumbele zaidi ili kuwezesha wataalam wengi kujikita kwenye taaluma zao.
“Ni lazima tutafutembinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali za elimu ikiwemo wanafunzi kuweza kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa hii itatuongezea ukuzaji wa ajira zaidi”.
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu , Profesa Awadh Mawenya alisema kuwa ni vyema kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu ili kuboresha sekta hiyo na kutoa rai kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuachana na tabia ya kusubiri kuajiriwa badala yake wabuni mbinu zitakazowawezesha kupata ajira pindi wamalizapo vyuo.
Pia alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tume ya Vyuo Vikuu itaendelea kuchukua hatua za kusimamia na kuimarisha ubora wa elimu ya juu nchini ikiwemo kufuatilia mwenendo wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki baada ya kutunukiwa hati idhini ili viendelee kuzingatia ubora unaokubalika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment