Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 14 August 2014

JIJI LA ARUSHA KUKUSANYA BILIONI 11.5/=


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

Arusha: HALMASHAURI ya Jiji la Arusha inatarajia kukusanya kiasi cha TShs. 11 .5 bilioni kwa mwaka 2014-2015 kutoka kwenye vyanzo mbali mbali vya mapato ya halmashauri hiyo ,ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni moja zitatumika katika sekta ya kilimo na ufugaji.
Aidha jiji hilo ni moja ya jiji inalotegemea zaidi kilimo na ufugaji na hivyo kuamua kutenga kiasi hicho ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika ipasavyo na sekta hiyo katika kuhakikisha kuwa  kilimo kinakuwa cha biasahra zaidi badala ya kukifanya kuwa cha mazoea.
Hayo yalielezwa  na Mkurugenzi wa Jiji  la Arusha Juma Iddi alipokuwa akizungumza na blog hii kuhusiana na hali ya mapato kwa mwaka huu.
Alieleza kuwa fedha hizo wanataraja kuzikusanya katika vyanzo mbali mbali vya halimashauri hiyo huku wakihakikisha kuwa sekta ya kilimo na ufugaji inapewa kipaumbele katika bajeti hiyo.
Alisema kuwa halimashauri hiyo inawajibika ipasavyo kusimamia shughuli za kilimo ,umwagiliaji na ushirika na kwamba katikakuhakikisha kuwa wananchi wa jiji wananufaika vema na sekta hizo wameamua kutumia kiasi hicho cha bilioni mojaili kuendeleza kilimo na ufugaji
“Katika mwaka huu wa fedha tunatarajia kukusanya kiasi hicho cha bilioni 11 na kati ya hizo bilioni moja tumeona lazima itumike kwenye sekta ya kilimo na ufugaji kwani tunahitaji kilimo kiwe cha biashara zaidi na kuufanya uchumi wa jiji uzidi kukua kwa haraka zaidi,” aliongeza.
Alifafanua kuwa kiasi hicho kitawasaidia wakulima na wafugaji katika kupatiwa elimu,madawa ya mimea nay a mifugo pamoja na vitendea kazi ambavyo vitawasaidia zaidi kuinua sekta hizo.
Aidha, aliwataka wakazi wa jiji kuhakikisha kuwa wanatumia maonyesho kwa ajili ya kujifunza na kuifanya elimu wanayoipata huko kuwa ya kuboresha uzalishaji zaidi na kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni na sheria wanazopewa ili kupata matokeo makubwa katika sekta ya kilimo na ufugaji.

No comments:

Post a Comment