Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 31 July 2014

UINGEREZA KURUHUSU GARI BILA DEREVA JANUARI, BONGO TUTAWEZEA WAPI NA MIFOLENI HII!

Gari linalojiendesha
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itaziruhusu gari zisizokuwa na madereva barabarani ifikapo mwezi Januari mwakani.
Serikali hiyo pia imetoa wito miji ya Uingereza zitoe mapendekezo ya kuwania kuwa wenyeji wa moja kati ya majaribio 3 ya magari hayo.
Aidha waziri huyo ameagiza kufanywe mabadiliko ya sheria za barabarani ilikuafikiana na mabadiliko hayo ya teknolojia.
Wizara ya usafiri wa umma nchini Uingereza ilikuwa imeahidi kuruhusu majaribio ya magari hayo mwisho wa mwaka uliopita.
Katibu wa Biashara Vince Cable aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Mira,kilichoko Midlands.
"tangazo hili la leo linatoa ithibati kuwa magari pasi na madereva yatakuwa barabarani katika miezi 6 zijazo''.
Uingereza kuruhusu magari bila ya dereva katika miezi 6 ijayo
Waandisi nchini Uingereza wakishirikiana na wanavyuoni kutoka chuo kikuu cha Oxford wamekuwa wakifanya majaribio ya matumizi ya magari hayo yasiyo na madereva.
Wadau hata hivyo wamekuwa wakiibua tahadhari ya maswala ya Bima,na uhalali wa magari pasi na madereva jambo ambalo limewalazimu kutumia barabra za kibinafsi kwa majaribio yao.
''Mimi mwenyewe nilijiskia kuwa salama ndani ya gari hilo lililokuwa bila dereva''alisema bwana Cable.
Wakati huohuo Magari hayo yameruhusiwa kufanyiwa majaribio huko Marekani katika majimbo ya California, Nevada na Florida.
Nissan imeruhusiwa kujaribu magari bila ya dereva
Gari linalonadiwa na kampuni ya mtandao wa Google tayari limetumika kwa zaidi ya kilomita laki tatu hivi katika mabarabara ya umma.
Mwaka uliopita kampuni ya 2013 ilifanya majaribio ya gari lake huko Japan.
Barani Uropa kampuni ya kutengeza magari ya Volvo tayari imepata ithibati ya kujaribu magari yake mjini Gothenburg Sweden.
BBCSWAHILI/TEKNOLOJIA

LIVERPOOL YAINYUKA MAN CITY 3-1

Liverpool iliwalaza mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti timu hizo zilipokutoshana nguvu 2-2 katika muda wa kawaida katika mechi ya kirafiki ya kuwania taji la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup).
Mechi hiyo iliyovutia mashabiki elfu 50,000 katika uwanja wa yankee ulioko New York ilianza bila ya msisimko kipindi cha kwanza kikikamilika matokeo yakiwa ni suluhu bin suluhu.
Kiungo cha kati wa Liverpool ,Jordan Henderson aliisawazishia timu yake kabla ya Jovetic kuirejeshea City uongozi .Lakini katika kipindi cha pili, mabingwa hao walidhibitisha niya yao mapema kupitia bao la Stevan Jovetic.
Uongozi huo hata hivyo haukudumu kwa muda mrefu kwani Raheem alifanya mambo kuwa 2-2.
Waandalizi waliamua mechi hiyo ikamilishwe kwa kupiga matuta ya penalti.
Na hapo vijana wa Brendan Rodgers walitamba na kujikatia tikiti ya nusu fainali ambapo sasa watachuana na AC Milan ya Italia .
City sasa itakwaruzana na Olympiakos ya Ugiriki.

Mchuano huo unajumuisha timu 8 za kimataifa.

BBC

LUKAKU AMWAGA WINO EVERTON

Romelu Lukaku
Hatimaye Romelu Lukaku amebebwa rasmi na Everton kwa kitita cha pauni milioni 28.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye miaka 21 aliyefunga mabao 16 akiwa Everton kwa mkopo msimu uliopita sasa atatumika pale Goodison Park kwa miaka mitano.
Lukaku alijiunga Chelse akitokea Anderlecht kwa pauni milioni 18 mwezi August 2011 lakini aliichezea mechi 15 tu.Bosi wa Everton Roberto Martinez amsemea: "Usajili huu sio tu muhimu kwa msimu huu, ni siku muhimu katika historia ya klabu."
Baada ya kutia saini Lukaku amsema, "Nina miaka 21, ninahitaji kucheza kwenye Timu bora. Nataka kuwa mahali palipo nigusa kisahihi”

"Niliamua haraka sana nilitaka kurejea. Hapa ndipo ninapotakiwa kuwa” Aliongeza Romelu Menama Lukaku.
BBC

EBOLA YASABABISHA MECHI KUAHIRISHWA

Mechi kati ya Sierra Leone na Seychelles yatibuka kutokana na hofu ya Ebola
Mechi kati ya Sierra Leone na Seychelles ya kuwania tikiti ya kushiriki katika kombe la mabingwa barani Afrika mwakani imetibuka.
Hiyo inafuatia hatua ya maafisa wa Ushelisheli kuwanyima Sierra Leone ruhusa ya kuingia nchini humo wakihofia wanaweza kueneza Ebola.
Timu hiyo ililazimika kurejea hotelini mjini Nairobi Kenya ambako wamekuwa wakipiga kambi tangu Jumatano.Yamkini timu hiyo ilikuwa ikipania kusafiri lakini maafisa wa usafiri wa ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi wakawaarifu kuwa Ushelisheli haijaidhinisha safari yao kuingia nchini humo.
Rais wa shirikisho la soka la Sierra Leone Elvis Chetty ameiambia BBC kuwa amepokea habari kutoka kwa Wizara ya afya ya Ushelisheli kuwa angependa waiahirishe mechi hiyo kutokana na hofu ya kuenea kwa Ebola.
Barua hiyo ya Wizara ya Afya inaelezea hofu ya kisiwa hicho ya kutokea mlipuko wa homa ya Ebola.
Chetty aliendelea kusema kuwa kufuatia tahadhari iliyotangazwa leo na rais wa Sierra Leone kuwa huenda ugonjwa huo ukadhibitiwa katika kipindi cha miezi minne ijayo basi huenda mechi hiyo haitachezwa kamwe.
Hatua hiyo huenda ikasababisha Ushelisheli ikapigwa marufuku ya kushiriki mashindano hayo.
Sierra Leone, ilishinda mkondo wa kwanza mabao mawili kwa nunge .
Ebola ilivyoenea Afrika Magharibi
Mechi hiyo ilichezwa juma lililopita.
Chetty alisema kuwa kuambatana na sheria za shirikisho la soka barani Afrika CAF, mechi hiyo inasiku 3 tu za kuchezwa vinginevyo wapinzani walistahili kupewa ilani siku 10 kabla ya tarehe iliyopangiwa mechi yenyewe.
''Ninaamini kuwa tayari Mshelisheli ameamua liwe liwalo hatocheza mechi hiyo na hilo huenda likaisababishia taifa hilo marufuku ya kipindi kirefu.

''Kimsingi taifa lote lilikuwa limechangamkia mechi hii na ni jambo la kusikitisha sana''.
BBC

SHULE ZAFUNGWA LIBERIA, SIERRA LEONE YATANGAZA HALI YA HATARI

Rais Sirleaf ametangaza amri ya kufungwa kwa shule zote
Rais wa Liberia,Ellen Johson Sirleaf ametangaza amri ya kufungwa kwa shule zote nchini humo kama mpango wa taifa hilo wa kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Ebola.
Mpango huo pia unashirikisha kuzitenga baadhi ya jamii zilizokatika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Katika visa vingine wagonjwa wamelazimika kutibiwa nyumbani kutokana na ukosefu wa vituo vya kutoa matibabu.Hatua hiyo inajiri huku maafisa wa afya wakidaiwa kuzongwa na kazi katika mji mkuu wa Monrovia ambapo vyumba vya kuwatenga waathiriwa wa ugonjwa huo vimejaa.
Ebola imeua sasa watu 672 magharibi mwa Afrika
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Thomas Fessy anasema huu ni mpango huo ambao mamlaka inaamini utapunguza mtagusano baina ya jamii na hivyo basi kusitisha kuenea zaidi kwa Ugonjwa huo unaoua.
Shule zote nchini humo zimefungwa ,na tayari wafanyikazi wa mashirika na Wizara za Serikali zisizo na umuhimu mkubwa wamepewa likizo ya siku 30.
Baadhi ya jamii zimetengwa-na kupewa madawa na chakula.
Serikali inajaribu kuzuia watu kutembea kutoka eneo moja hadi jingine ikiwa na imani kwamba watu walioathirika watajulikana na kutibiwa.
Vikosi vya usalama vimeagizwa kutekeleza hatua hiyo.
Ebola huenea kwa kumgusa mtu aliyeambukizwa
Wakati huohuo baadhi ya raia wamepinga kubuniwa kwa eneo jipya la kuwatenga watu na kuwalazimu maafisa wa afya kuwatibu hadi wagonjwa 20 katika makaazi yao.
Bado haijulikani ni vipi serikali itafanikiwa kutekeleza hatua hiyo wakati ambapo kuna hofu na shauku.
Hadi kufikia sasa Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 672 katika matifa matatu ya Afrika Magharibi yaani Liberia Sierra Leone na Guinea huku mtu mmoja akifariki nchini Nigeria.
Liberia, Sierra Leone na Guinea zimeathirika pakubwa na Ebola.
Shirika la Marekani linalotoa misaada ya huduma kwa jamii (Peace Corps) limewaondoa mara moja wahudumu wao katika mataifa yaliyoathirika pakubwa Liberia, Sierra Leone na Guinea baada ya mmoja wao kupatikana ameambukizwa.
Kulingana na takwimu Ebola huua asilimia 90% ya watu walioambukizwa homa hiyo ambayo huchukua kuanzia siku 2-20 kujulikana iwapo mtu ameambukizwa.
Hiyo ndiyo sababu asilimia kubwa ya wahudumu wa afya waliokuwa wakiwatibu wagonjwa walidhania kuwa ilikuwa ni Malaria na hivyo kuambukizwa homa hiyo kali.
Ugonjwa huu ulitubuka nchini Guinea mwezi Februari.

Homa hiyo ilienea kwa haraka hadi Liberia na sasa Sierra Leone ambapo Rais wa nchi hiyo ametangaza hali ya hatari kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo.
Rais Ernest Bai Koroma ametoa agizo maeneo yaliyokuwa yakwanza kuripoti ugonjwa huo yadhibitiwe ipasavyo na kutengwa .
Rais Koroma aliagiza watu wasiruhusiwe kuingia au kutoka kwenye maeneo hayo chimbuko la mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Maafisa wa Usalama ndio waliopewa jukumu la kutekeleza maagizo hayo kwa ushirikiano na maafisa wa Afya ya umma.
Kulingana na takwimu Ebola huua asilimia 90% ya watu walioambukizwa homa hiyo ambayo huchukua kuanzia siku 2-20 kujulikana iwapo mtu ameambukizwa.
Hadi kufikia sasa Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 672 katika matifa matatu ya Afrika Magharibi yaani Liberia Sierra Leone na Guinea huku mtu mmoja akifariki nchini Nigeria.
Rais Koroma ametangaza kuwa hataenda Marekani kwa mkutano baina ya viongozi wa Afrika na rais Obama.
Chanzo: BBCSWAHILI

ISRAEL KUHARIBU NJIA ZA CHINI KWA CHINI

Israel inasema kuwa haitaondoka Gaza hadi iharibu njia za chini kwa chini
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa Israel imeamua kuyaharibu kabisa mahandaki na njia za chini ya ardhi zilizojengwa na wapiganaji wa Palestina-Hamas, katika mipaka yake huko Gaza.
Amesema uharibifu huo utatekelezwa na majeshi ya Israeli kukiwa au kutokuwa na muafaka wa kusitisha mapigano.
Mwanamke akiomboleza Gaza
Netanyahu amesema hayo huku Serikali ya Israel ikishikia kani kuwa kuwa itaendeleza mashambulizi katika eneo la Gaza licha ya shutma za kimataifa kufuatia shambulizi la shule moja ya umoja wa mataifa ambapo takriban watu 15 walipoteza maisha yao.
Msemaji wa serikali ya Israel amesema kuwa wataomba msamaha iwapo watabaini kwamba shambulizi hilo, lilitekelezwa kimakosa na wanajeshi wa Israel.
Umoja wa mataifa umesema kuwa ni wazi kwamba ni jeshi la israel ndilo lililorusha kombora hilo katika shule hiyo ambapo zaidi ya raia elfu tatu wa Palestina walikuwa wameomba hifadhi.
Licha ya malalamiko kutoka kote duniani kuhusiana na idadi kubwa ya vifo vya watu.
Njia za chini kwa chini za Hamas ambazo Israeli inalenga kuharibu
Mashambulizi ya Israel kutoka angani na nchi kavu yamerindima kwa milipuko ya mizinga na ndege za kivita.

Na sasa Israel inajiandaa kwa vita zaidi baada ya kuwaamuru wanajeshi wa akiba kujiunga na jeshi la taifa. Katika ukanda wa ngaza ni kilio na majonzi makubwa.
BBCSWAHILI

BALOZI WA NORWAY NCHINI INGUNN KLEPSVIK AMUAGA RAIS KIKWETE IKULU

D92A3955 D92A3944 D92A3951
D92A3957
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini anyemaliza muda wake Ingunn Klepsvik wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga Rais Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi (Picha na Freddy Maro)

LHRC: WANAWAKE NA WASICHANA 2,878 WABAKWA KATI YA JANUARI HADI JUNI 2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba
Mtafiti wa Tafiti mbalimbali wa LHRC, Wakili Pasience Mlowe.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leoasubuhi, wakati akitoa taarifa ya kituo hicho ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari hadi kufikia Juni 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na Mtafiti wa LHRC, Pasience Mlowe.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwachua picha za utoaji wa taarifa hiyo. Imeandaliwa na www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 
Na Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema kuwa hadi kufikia Juni 2014 wanawake na wasichana 2,878 wamebakwa nchini kutokana na vitendo vya ukatili dhidi yao.
 Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba wakati akitoa taarifa ya kipindi cha nusu mwaka kuanzia Januari na Juni mwaka huu kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo.
 “Vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya makundi hayo vilivyoripotiwa polisi kwa nchi nzima vilikuwa 3,633″ alisema Kijo -Bisimba.
 Kijo-Bisimba alisema taarifa hii inatoka na tafiti zilizofanywa na kituo hicho ili kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka kwa waangalizi wa haki za binadamu, wasaidizi wa sheria, taarifa rasmi kutoka taasisi za Serikali, Bunge, Mahakama,vyombo vya habari na asasi mbalimbali zisizo za kiserikali.
Akizungumzia kuhusu taarifa ya Sensa ya watu na makazi inaonesha idadi kubwa ya watu wanaishi vijijini huku wakiwa na huduma duni za kijamii kama za afya, maji, umeme, umeme na shule.
 Alisema takwimu zinaonesha bado vijijini kuna makazi duni ya wananchi kutokana na gharama kubwa za saruji na vifaa vya ujenzi, mfano katika suala la upatikanaji maji makazi 3,959,857 yanatumia vyanzo vya maji visivyo salama ukilinganisha na makazi 1,902,244 yanayotumia maji ya bomba nchi nzima.
 Kuhusu kilimo alisema idfadi ya wananchi wengi wapatao 11,359,090 wanategemea kilimo kama shughuli kuu ya uchumi hata hivyo wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono.
 “Uwekezaji katika mashamba makubwa wamepewa wawekezaji wakubwa mfano mashamba makubwa ya mpunga yaliyokuwa ya Shirika la NAFCO wilayani Mbarali mkoani Mbeya wamepewa wawekezaji na wakulima wazawa wametengewa yasiyofaa” alisema Kijo-Bisimba.

Credit Source: Fullshangwe

WATUHUMIWA WALIOKAMATWA KUHUSIANA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAKIHUSISHWA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI MKOANI ARUSHA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


NDUGU WANAHABARI, MTAKUMBUKA KUWA WIKI MOJA ILIYOPITA JESHI LA POLISI LILITOA TAARIFA KWA UMMA JUU YA WATUHUMIWA SITA WALIOKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA TAREHE 07/07/2014 KATIKA MGAHAWA WA VAMA ULIOPO MAENEO YA VIWANJA VYA GYMKANA JIJINI ARUSHA.
TAARIFA HIYO ILIZUNGUMZIA PIA TUKIO LA KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE BAADA YA KUPEKULIWA NYUMBANI KWAKE ALIKUTWA NA MABOMU SABA YA KURUSHA KWA MKONO, RISASI SITA ZA BUNDUKI AINA YA SHOT-GUN PAMOJA NA UNGA WA BARUTI. TULIELEZA PIA KUWA OPERESHENI YA KUKAMATA WATUHUMIWA WENGINE KUHUSIANA NA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI ILIKUWA IKIENDELEA, NA KWAMBA WATUHUMIWA KADHAA WALIKUWA CHINI YA ULINZI WA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYO.
KUTOKANA NA OPERESHENI HIYO ENDELEVU, WATUHUMIWA WENGINE KADHAA WAMEKWISHA KAMATWA NA KUHOJIWA, AMBAPO USHAHIDI ULIOKUSANYWA UMEBAINI KUWA KATI YAO WATUHUMIWA ISHIRINI NA MOJA (21) WANAHUSIKA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA ULIPUAJI MABOMU NA KUMWAGIA WATU TINDIKALI HAPA JIJINI ARUSHA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA MWAKA 2012 HADI YALE YALIYOTOKEA KATIKA KIPINDI CHA HIVI KARIBUNI. 

WATUHUMIWA HAO WANATAZAMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI TAREHE 01/08/2014 KUUNGANA NA WENZAO WALIOKWISHA TANGULIA ILI KUJIBU MASHITAKA YANAYOWAKABILI. UFAFANUZI WA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NA MATUKIO WALIYOHUSIKA NAYO NI KAMA IFUATAVYO:
I. TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU NYUMBANI KWA SHEKH ABDULKARIM JONJO TAREHE 25/10/2012WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:1. YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
2. KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNERLL
3. MUSTAPHA S/O MOHAMED KIAGO, MZIGUA, MIAKA 49, MKAZI WA KALOLENI, NI SHEKH MSIKITI MKUU WA IJUMA
4. ABDUL-AZIZ S/O MOHAMED, MCHAGA, MIAKA 49, MKAZI WA ENEO LA FAYA, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI MKUU WA IJUMAA

II. TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA ST. JOSEPH MFANYAKAZI OLASITI LA TAREHE 05/05/2013WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:1. YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO.
2. RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.
3. ABDUL S/O MOHAMED HUMUD @ WAGOBA, MMANYEMA, MIAKA 30, MKAZI WA MURIET, WAKALA WA MABASI YA MOHAMED TRANS (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
4. JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
5. SAID S/O MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
6. KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
7. ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
8. ABDULRAHAMAN S/O JUMANNE HASSAN, MBONDEI, MIAKA 41, MKAZI WA SINONI, MFANYAKAZI WA STANBIC BANK ARUSHA
9. MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
10. NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA
11. BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
12. HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA

III. TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU VIWANJA VYA SOWETO KWENYE MKUTANO WA CHADEMA TAREHE 15/06/2013
WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
1. YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
2. ABDUL S/O MOHAMED HUMUD @ WAGOBA, MMANYEMA, MIAKA 30, MKAZI WA MURIET, WAKALA WA MABASI YA MOHAMED TRANS (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
3. JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
4. SAID S/O MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
5. KASSIM S/O IDRISSA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
6. RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO
7. ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
8. ABDULRAHAMAN S/O JUMANNE HASSAN, MBONDEI, MIAKA 41, MKAZI WA SINONI, MFANYAKAZI WA STANBIC BANK ARUSHA
9. MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
10. NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA
11. BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
12. HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA

IV. TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI SHEKH SAID JUMA MAKAMBA WA MSIKITI WA KWA MOROMBO TAREHE 11/07/2013WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:1. YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
2. RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.
3. KASSIM S/O IDRISA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
4. JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)

V. TUKIO LA KUMWAGIWA TINDIKALI SHEKH MUSTAPHA KIAGO WA MSIKITI MKUU LA TAREHE 28/02/2014
WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
1. YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
2. KASSIM S/O IDRISSA RAMADHAN, MRANGI, MIAKA 34, MKAZI WA NGUSERO BANDA MBILI, DEREVA BODABODA FRIENDS CORNER
3. JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
4. HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA

VI. TUKIO LA BOMU ARUSHA NIGHT PARK (MTK) LA TAREHE 13/04/2014
WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
1. JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
2. IBRAHIM S/O LENARD @ SHEKH ABUU ISMAIL, MSUKUMA, MIAKA 37, MKAZI WA MABATINI MKOANI MWANZA.

VII. TUKIO LA BOMU NYUMBANI KWA SHEKH SUDI ALLY SUDI LA TAREHE 03/07/2014
WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
1. YAHAYA S/O TWALIB TWAHIR @ MPEMBA, MSAMBAA, MIAKA 37, MKAZI WA MTAA WA JALUO, MFANYABIASHARA YA DUKA MTAA WA BONDENI
2. IDD S/O RAMADHAN YUSUPH, MSAMBAA, MIAKA 23, MKAZI WA MTAA WA JALUO.
3. SAID S/O MICHAEL TEMBA, MCHAGA, MIAKA 42, MKAZI WA SINONI- UNGA LTD, MFANYABIASHARA SOKO LA KILOMBERO (AMEKWISHAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWAWA VAMA)
4. ANWAR S/O NASHER HAYEL, MNYAMWEZI, MIAKA 29, MKAZI WA NGULELO, MFANYABIASHARA
5. JAFAR S/O LEMA, MCHAGA, MIAKA 38, MKAZI WA NGULELO, ALIKUWA IMAMU WA MSIKITI WA QUBA (AMEKWISHA FIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHUSISHWA NA TUKIO LA BOMU MGAHAWA WA VAMA)
6. HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA
7. YUSUPH S/O ALLY RAADHAN @ SEFU, MPARE, MIAKA 23, MKAZI WA NGUSERO
8. ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
VIII. TUKIO LA KUPATIKANA NA MABOMU LA TAREHE 21/07/2014
WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
1. YUSUPH S/O HUSEIN ALLY HUTA, MRANGI, MIAKA 30, MKAZI WA NGUSERO
2. SUMAIYA W/O YUSUPH HUSEIN ALLY, MWASI, MIAKA 19, MKAZI WA NGUSERO.
3. RAMADHAN S/O HAMAD WAZIRI, MRANGI, MIAKA 28, MKAZI WA KWA MOROMBO.
4. HASSAN S/O ALLY MFINANGA, MPARE, MIAKA 57, MKAZI WA MAKAO MAPYA, BIASHARA
5. ABASHAR S/O HASSAN OMAR, MRANGI, MIAKA 24, MKAZI WA NGUSERO MWISHO WA HIACE, DEREVA BODABODA STAND KUU ARUSHA
6. KIMORO S/O ISSA MCHANA @ OMAR @ ABUU TWALIB, MRANGI, 25YRS, MKAZI WA ITOLWA KONDOA
7. HASSAN S/O ABDALLAH OMAR, MNYATURU, MIAKA 40, MKAZI WA ILONGERO MKOANI SINGIDA.
8. MORRIS S/O JOHN MUZI, MUHA, MIAKA 44, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
9. NIGANYA S/O HAMISI NIGANYA, MUHA, MIAKA 28, MKAZI WA BUSINDE UJIJI MKOANI KIGOMA
10. BARAKA S/O NTEMBO BILANGO, MUHA, MIAKA 40, MKAZI WA KALINZI MKOANI KIGOMA
IX. KOSA LA KUHAMASISHA VITENDO VYA KIGAIDI KUPITIA MTANDAO WA KIJAMII
WATAKAOFIKISHWA MAHAKAMANI:
1. IBRAHIM S/O LENARD @ SHEKH ABUU ISMAIL, MSUKUMA, MIAKA 37, MKAZI WA MABATINI MKOANI MWANZA.
2. ANWAR S/O NASHER HAYEL, MNYAMWEZI, MIAKA 29, MKAZI WA NGULELO, MFANYABIASHARA
3. YASINI S/O MOHAMED SHABAN @ YAKI, MCHAGA, MIAKA 20, MKAZI WA KALOLENI MITA 200
OPERESHENI YA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE WA MATUKIO HAYA INAENDELEA NCHI NZIMA, NA TAYARI TUNAYO MAJINA YA WATUHUMIWA KADHAA AMBAO WAMETOWEKA ARUSHA NA KUELEKEA MAENEO MBALIMBALI YA NDANI NA NJE YA NCHI. MTUHUMIWA MMOJAWAPO ANAYETAFUTWA SANA NA POLISI KUHUSIANA NA MATUKIO HAYA NI YAHAYA HASSAN HELLA @ SENSEI, KABILA NI MRANGI, MZALIWA WA KIJIJI CHA CHEMCHEM WILAYA YA KONDOA.
IMEBAINIKA KUWA MTUHUMIWA HUYO NDIYE KINARA WA MATUKIO YA MILIPUKO YA MABOMU NA TINDIKALI HAPA JIJINI ARUSHA KWA KUSHIRIKIANA NA WENZAKE WALIOKAMATWA, NA AMBAO BADO WANAENDELEA KUTAFUTWA. 
JESHI LA POLISI LINAFANYA KILA JITIHADA KUWEZA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WOTE WALIOTOROKA NA KUHAKIKISHA KUWA SHERIA INACHUKUA MKONDO WAKE.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA:-
LIBERATUS M. SABAS – SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
31/07/2014

UDA YATOA MSAADA WA SHS. 15 MILIONI KWA KANISA LA MT. RITA

St. RITA PIX 2
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase (kulia) kusaidia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita hivi karibuni. Picha na mpiga picha wetu.
St. RITA PIX 3
Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase(kulia) akionyesha hundi ya shilingi milioni 15 zilizotolewa na  Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mchango huo wa kampuni ulitolewa kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri kanisani hapo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija. Picha na mpiga picha wetu
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu   
MAENDELEO ya kijamii na kiuchumi yataweza kupatikana endapo tu kila mtu ataweza kutoa mchango wake kuwasaidia wale wanaohitaji msaada ili kubadilisha maisha yao na kuwa wachangiaji wakubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Simon Bulenganija wakati wa harambee ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri katika Kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, ambapo UDA ilichangia shilingi milioni 15.
“Watanzania wasisubiri mpaka makampuni makubwa yajitokeze na kutusaidia kubadilisha hali zetu za kiuchumi na mfumo wetu wa maisha. Mabadiliko yataweza kufikiwa tu endapo kila mmoja wetu ataweza kuchangia kwa nafasi yake kikamilifu. Makampuni yote makubwa na madogo na watu binafsi wenye uwezo wa kusaidia, wawashike mkono wale wanaohitaji msaada ili tuweze kuendelea pamoja,” alisema.
Bw. Simon Bulenganija alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikijihusisha na shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni jitihada madhubuti zinazolenga katika upatikanaji wa maendeleo miongoni mwa watanzania wote.
Alisema kuwa shilingi milioni 15 zilizotolewa na UDA zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga jeki maendeleo ya kanisa hilo hususani katika ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na mradi wa ujenzi wa kanisa jipya.
“Japokuwa bado kampuni yetu ni kampuni changa ya kitanzania, tumeunda programu yetu ya shughuli za kijamii katika namna ya kwamba shughuli tunazojihusisha nazo, zitasaidia katika kutekeleza ajenda yetu yenye kaulimbiu “ukuaji wa kampuni yetu uwe sambamba na ukuaji wa kiuchumi wa jamii yetu”. Hii pia ni njia pekee ya kurudisha sehemu ya pato letu kwa jamii,” alisema Bw. Bulenganija.
Naye, Bw. Frederick Msumali, Mwenyekiti wa Kigango cha Mtakatifu Rita, aliipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake na ushiriki wa Mkurugenzi wa UDA wakati wa shughuli hiyo ya harambee ambayo iliwezesha kanisa hilo kukusanya zaidi ya shilingi milioni 60 zitakazotumika katika mradi huo.
“Tungependa kwa kiasi kikubwa kutoa shukrani zetu kwa mchango uliotolewa na UDA.  Msaada huu kwa kiasi kikubwa utasaidia kupiga jeki mradi wetu wa ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na ujenzi wa kanisa jipya utakaofanyika karibu na kanisa hili la sasa.
“Lakini pia, tunaishukuru UDA kama kampuni na Bw. Bulenganija mwenyewe kwa kuwa mgeni wetu rasmi. Mfano huu unahitaji kuigwa na makampuni mengine nchini,” alisema Bw. Msumali.

Credit Source: Fullshangwe

SKYLIGHT BAND YAFUNIKA MBAYA EID MOSI NDANI YA ESCAPE ONE!

DSC_0011
Sam Mapenzi (katikati) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya fukwe za Escape One katika show maalum kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid-El Fitr huku akipewa back Vocal na Sony Masamba pamoja na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0015
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ukumbi wa Escape One.
DSC_0306
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakiachia kwenye dancing floor.
DSC_0243
Sam Mapenzi akitoa burudani adimu mashabiki wa Skylight Band katika sikukuu ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One jijini Dar.
DSC_0237
Skylight Band ni #balsaa# hebu angalia mashabiki wanaojua burudani ya muziki wa Live wanavyosebeneka.
DSC_0189
Rappa Mkongwe Joniko Flower akitunzwa wekundu wa msimbazi na mmoja wa mashabiki wa Skylight Band aliyekunwa na uimbaji wa rapa huyo.
DSC_0018
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni Mary Lucos akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani).
DSC_0466
Mary Lucos wa Skylight Band akiwaduarisha mashabiki wa bendi hiyo katika sikukuu ya Eid El Fitr ndani kiota cha Escape One.
DSC_0487
Wadada wakijipinda kuzungusha nyonga zao.
DSC_0471
DSC_0139
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiduarika.
DSC_0159
DSC_0023
Pichani juu na chini ni sehemu ya umati wa wakazi wa Dar wake kwa waume waliokusanyika ndani ya fukwe za Escape One kujipatia upepo mwanana huku wakiburudishwa na Skylight Band.
DSC_0024
DSC_0028
Mashabiki wa Skylight Band wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali huku wakisiliza burudani ya kutoka bendi ambayo kwa sasa ndio habari ya mujini.
DSC_0077
DSC_0337
Ale Mama mupe Saluti……!!! Twende kazi…..
DSC_0355
Muguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma….Yachuma chuma…!! Kikosi cha Skylight Band wakicheza sambamba na mashabiki wao katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One.
DSC_0356
DSC_0388
Burudani ikiendelea na watu wakiendelea kusebeneka.
DSC_0401
Wadada walichizikaje…!?
DSC_0514
DSC_0411
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakionyesha umahiri wao wa kucheza moja ya staili za bendi hiyo kwa wanamuziki Joniko Flower na Sony Masamba.
DSC_0420
DSC_0235
Daudi Tumba akitweta jasho kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ladha nzuri ya muziki kupitia ala za Band hiyo huku Tumba ikihusika pia kutengeneza sauti nzuri kabisa.
DSC_0274
Pichani juu na chini ni Hashim Donode a.k.a Mzee wa Viduku akifanya yake!
DSC_0310
DSC_0069
Afisa Mtendaji Mkuu wa Skylight Band, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bendi hiyo Justine Ndege wakati Skylight Band ikiendelea kutoa burudani kwenye sherehe za sikukuu ya Eid -El- Fitr ndani ya kiota cha Escape One.
DSC_0217
Blogger William Malecela a.k.a LEMUTUZ mwandaaji wa Instagram Party itakayofanyika Jumamosi hii kwenye kiota cha Escape One akishow love na Fans wake mdau Joseph Magige.
DSC_0437
Sam Mapenzi kwenye ukodak na Customer care huku akionyesha Video mpya ya “Pasua Twende” kupitia simu yake ya kiganjani.
DSC_0394
Emma Bass wa Skylight Band (kulia) akipata ukodak na swahiba wake.
DSC_0379
Joniko Flower wa Skylight Band akishow love na mdau.
DSC_0296
Mratibu wa Skylight Band Lubea akipata ukodak na Mwimbaji Mary Lucos back stage.
DSC_0002
Mkurugenzi Mtendaji wa Skylight Band na Rais wa #WANAMANYOYA# Justine Ndege (katikati) akipata Ukodak Mkuu wa Itifaki wa #WANAMANYOYA# Eddie Viede pamoja na mdau wa Skylight Band James Rock Mwakibinga.
DSC_0228
Palinogaje wewe tu umekosekana….Si haba kesho pia ni siku tukutane viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0256
DSC_0251
Aneth Kushaba AK 47 a.k.a Komando Kipensi akishow love na Tophy mpiga bass wa Skylight Band back stage.

Credit Source: Fullshangwe