Masuala mawili hayo,
(i) Msimamo wa Zanzibar kuhusu utaratibu wa kuchagua Makamu wa Jamhuri ya Muungano, na
(ii) Zanzibar kuingia katika OIC ndiyo yaliyokuwa sababu ya ujumbe wa mara kwa mara kati yangu na Rais wa Jamhuri ya Muungano; na ndiyo Rais na mimi tulikuwa tukiyazungumza Butiama, tarehe 2 Agosti, 1993. Baada ya kuyazungumza kwa muda mrefu na kuelewana nini la kufanya, Rais akanifahamisha kwamba Waziri Mkuu kamletea habari kwamba:
(a) Wabunge 44 wamejiandikisha kupeleka bungeni hoja ya kudai Selikali ya Tanganyika;
(b) Kwa maoni yake hoja hiyo ikijadiliwa bungeni, baadhi ya mawaziri wataiunga mkono na yeye atapata tatizo la kuipinga au kuiunga mkono.
(c) Anapendekeza ifanywe semina ya wabunge wote na viongozi wa Zanzibar, ikiwamo Serikali na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, ili hoja hiyo izungumzwe na ipingwe nje ya Bunge na
(d) Rais aniombe nikubali kushiriki katika Semina hiyo. Nilimwambia Rais kwamba niko tayari kushiriki katika semina iliyopendekezwa na Waziri Mkuu;
Lakini kwa kuwa tunakubaliana kwamba hoja ya wabunge ni matokeo ya msimamo wa Zanzibar kuhusu masuala mawili hayo, itafaa “tuyamalize" kabla ya kukabiliana na wabunge.
Sikusema kuwa tusipoyamaliza vema; sitapinga hoja ya wabunge; nilisema, nadhani kwa kusisitiza, kwamba hoja hiyo kwa vyo vyote mimi nitaipinga; lakini "hali ya hewa" itakuwa ni tofauti kama hoja inapingwa baada ya Zanzibar kukubali, au kukataa kubadili msimamo wake, na Selikali ya Muungano itakuwa imeonyesha msimamo gani katika masuala hayo.
DAR ES SALAAM 5:8:1993

Kikao tulichofanya Dar es Salaam kuendeleza
mazungumzo haya tulikuwa na Rais na Makamu wake wote, na Waziri Kiongozi na
viongozi wengine wa Zanzibar, na Manaibu wa Katibu Mkuu wa CCM. Katibu Mkuu,
hakuwepo. Pamoja na kwamba mazungumzo haya yalikuwa magumu, lakini
tulikubaliana katika kikao hicho:
(i) Zanzibar itoke katika IOC;
(ii) Tukubali mapendekezo ya
Kamati ya Bomani kuhusu utaratibu mpya wa kuchagua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano;
(iii) Hoja ya Serikali Tatu
ipingwe, na mimi nisaidie kuipinga; na
(iv) Kamati Kuu iitwe ili itoe
uamuzi wake rasmi kuhusu masuala haya.
Siku hiyo baadhi ya wabunge,
viongozi wa hoja ya Serikali Tatu, waliomba kuja kuonana nami Msasani.
Tulizungumza kwa muda mrefu; na
wote walisema; wakieleza sababu zao za kudai Serikali ya Tanganyika. Nilisisitiza
kwao kwamba zote zilikuwa ni sababu za kuwataka wawadhibiti viongozi wetu na
kuwataka watuongoze kwa kufuata sheria na, Katiba ya Nchi yetu.
Hapakuwa na sababu hata moja ya
kuwafanya wadai Serikali ya Tanganyika, maana hata ukiwa na Serikali ya Tanganyika
bado viongozi wetu wanaweza kukiuka sheria na Katiba ya Nchi, na dawa haitakuwa
ni kuigawa nchi tena na kuongeza serikali.
Bali ni kuwadhibiti viongozi wahalifu. Baadaye hoja hizi nilizirudia bungeni.
Bali ni kuwadhibiti viongozi wahalifu. Baadaye hoja hizi nilizirudia bungeni.
Siku iliyofuata, tarehe 6:8:1993,
mimi niliondoka kwenda Brussels, Ubelgiji, kumwakilisha Rais katika mazishi ya
Mfalme wa nchi hiyo. Huku nyuma Kamati Kuu iliitwa. Niliporudi tarehe 9:8:1993
Kamati hiyo ilikuwa inakutana Dares Salaam. llipokwisha kufikia uamuzi wake,
viongozi waliotumiwa kuja kunieleza uamuzi huo walikuwa ni Waziri Mkuu, Katibu
Mkuu wa CCM, na Waziri Kiongozi. Msemaji wao alikuwa Katibu Mkuu.
UAMUZI WA
KAMATI KUU: 10:8:1993
(i) OIC: Zanzibar itoke;
(ii) MAKAMU WA RAIS: Mapendekezo ya
Kamati ya Bomani yakubaliwe;
(iii) HOJA YA SERIKALI TATU:
Ipingwe;
(iv) SEMINA: Isifanyike; badala
yake mazungumzo yafanyike katika kamati ya Chama ya Bunge.
Baadaye Rais alinifahamisha kwa
simu kwamba yeye sasa alikuwa hakusudii kwenda kusema na wabunge, lakini
akanitaka mimi niende. lnaelekea kuwa baadhi ya viongozi waliona kuwa Rais
akienda kusema atawazuia wabunge wenye hoja kutoa dukuduku zao bila hofu.
Kwa kuwa nilikuwa nafahamu kwamba
baadhi ya viongozi wa Chama na Selikali walikuwa na maoni hayo hayo kuhusu
kushiriki kwangu, nilimwambia Rais kwamba hata na mimi nisiende kusema bungeni.
Na kwa vyo vyote vile kushiriki kwangu kulitegemea kushiriki kwake; lakini kama
yeye haendi kusema na wabunge, mimi nitakwenda kama nani na kutafuta nini? Kwa
hiyo yafaa wote wawili tusiende. Tukakubaliana hivyo.
NYUMBANI
KWA RAIS: 13:8:1993
Baadaye Rais akanipigia simu tena
na kuniambia kuwa Waziri Mkuu alipoelezwa makubaliano yetu ya kutokwenda kusema
na wabunge amechachamaa. Nikamwomba Rais amwambie Waziri Mkuu asiondoke ili
niende wote watatu tuzungumze la kufanya. Nikaenda; tukazungumza kwa muda
mrefu. Waziri Mkuu akanisihi sana sana, niende bungeni, nikasaidie kupinga hoja
ya Serikali Tatu. Nikakubali, nikasisitiza mambo mawili:
(i) Rais awe ndiye msemaji mkuu
na mimi niwe msaidizi tu; na
(ii) Uamuzi wa Zanzibar kutoka
katika OIC; na wa kukubali utaratibu wa kuchagua Makarnu uwe umekwisha
kutangazwa.
Nilisiliitiza kwamba itafaa uamuzi
wa Zanzibar kutoka katika OIC uelezwe wazi wazi, na bila kuvungavunga, ili makali
ya wabunge, kama ikiwezekana, yawe yamepunguzwa kabla hatujapinga hoja ya
Selikali Tatu,
Tulipokwisha kukubaliana hivyo
Waziri Mkuu alifurahi sana na kusema kwa Kiingereza: "I could not take No for an answer! Nisingekubali jibu la Hapana!
Tukaachana.
BUNGENI:
14:8:1993
Kesho yake tarehe 14:8: 1993
tulikwenda bungeni.
(i) Nadhani jana yake Waziri Mkuu
alikuwa amekwisha kutanga uamuzi wa Zanzibar kutoka katika OIC, na wakubali
mapendekezo ya Kamati ya Bomani kuhusu utaratibu wa kuchagua Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano. Na kwa upande wa Zanzibar Rais wa Zanzibar alikuwa
amekwisha kufanya hivyo. Bungeni Waziri Mkuu alieleza sababu za kutuomba tuseme
na wabunge.
(ii) Rais alieleza historia ya
kisa cha OIC na uamuzi wa Zanzibar kujitoa. Akapinga hoja ya Serikali tatu.
(iii) Mimi nilieleza kwa kirefu
sana ile migogoro miwili ya awali. Pia kupinga hoja ya Serikali Tatu. Katika
kufanya hivyo nilieleza historia ya Muungano wa Serikali Mbili, badala ya
serikali moja au shirikisho la serilali tatu.
REJEA:
NYERERE, J.K.; UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA
No comments:
Post a Comment