Klabu ya soka ya Manchester United imepiga marufuku uingizwaji wa tabiti au (Tablets) na komputa za Laptop kwa watakaokuwa wanaingia katika uwanja wake.
Klabu hiyo inasema imechukua hatua hiyo,kuambatana na taarifa za kijasusi ikiongeza kwamba kikwazo hicho kinaambatana pia na mikakakti mipya ya ukaguzi wa vifaa vya elektroini katika viwanja vya ndege.
Ilisema kuwa kinyume na hali ilivyo katika viwanja vya ndege, haitawezekana kuhakikisha ikiwa vifaa vinavyoletwa na mashabiki ikiwa ni ghushi kwa kutaka waviwashe.
Polisi hata hivyo wamesema hawajahusika na hatua ya kupiga marufuku vifaa hivyo.
Taarifa kwenye mtandao wa klabu hiyo, imesema marufuku hiyo itahusisha tabiti kubwa na ndogo, pamoja na vifaa vingine vikubwa vya elektroniki.
Lakini Smartphones zinaruhusiwa ila kwa masharti fulani.
Msemaji wa klabu hiyo, aliambia BBC kwamba imechukua hatua hiyo baada ya kupokea ushauri lakini hakusema ushauri huo unatoka kwa nani.
Aliongeza kwamba wasiwasi kuwa klabu hiyo haitaki mashabiki kurekodi video za mechi zinapokuwa zinaendelea na kuwazuia mashabiki wengine kutizama mechi, hauna msingi.
Msemamji wa ligi ya uingereza naye amesema kwamba wao hawajahusika kivyovyote na marufuku hiyo.
BBC/SWAHILI-MICHEZO
No comments:
Post a Comment