Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 1 August 2014

BALAA HILI, MTOTO WA RAIS KIZIMBANI KWA UFISADI


Karim Wade

Kesi ya ufisadi dhidi ya Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade imeanza kusikilizwa huko Dakar Senegal.
Hata hivyo kesi hiyo inaanza kusikilizwa mshitakiwa akiwa kizuizini katika gereza kuu la Dakar, Rebeuss kwa mwaka mmoja sasa.
Hata hivyo kiwango hicho cha fedha kinadaiwa kuwa kidogo ikilinganishwa na kile kilichosababisha kukamatwa kwake ambacho ni Euro bilioni moja.Waziri huyo wa zamani atatakiwa kuieleza mahakama vyanzo vya utajiri wake wa Euro milioni 178.
Seydou Diagne, mmoja wa wanasheria wa Karim Wade, amelalamikia mashitaka hayo na kuyaita ya kisiasa akidai kuwa kitu pekee kinachowasukuma wanao mshitaki mteja wake.
Wanasheria wake pia wamedai hata hiyo mahakama itakayotumika kuchunguza matumizi mabaya ya ofisi haina uwezo wa kuisimamia kesi hiyo.
Hii ni moja ya kesi za kuwatafuta vigogo waliozitumia vibaya ofisi zao wakati wa utawala wa Rais Abdoulaye Wade.
BBC

No comments:

Post a Comment