HALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE
HALI YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA APRILI 2014 MANISPAA YA TEMEKE
Utangulizi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ina ukubwa wa kilometa za mraba 656. Ina jumla ya watu 1,368,881 kwa taarifa ya sensa ya mwaka 2012.
Manispaa ina Tarafa 3 za Mbagala, Chang’ombe na Kigamboni. Pia ina kata 30 na mitaa 180.
Kuna jumla ya Maafisa Afya 75 ambao wanafanya kazi kwenye vitengo mbalimbali na wengine wapo ngazi ya kata.
1.HALI YA USAFI WA TEMEKE
Operesheni za usafi wa mazingira
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke inaendelea kufanya operesheni za usafi wa mazingira ili kuondoa kero za uchafuzi wa mazingira kwa makusudi. Opresheni hizi zimeanza kutekelezwa tangu tarehe 20-03-2014 na zimelenga katika mambo makuu kama ifuatavyo;-
I. Kuondoa wafanya biashara ambao wanafanyia biashara zao katika maeneo yasiyo rasmi mfano
- Kandokando ya bararaba za waendao kwa miguu,
- Juu ya mifereji ya maji ya mvua
- Katikati ya barabara zinazotumiwa kwa usafiri wa magari
Upikaji.
- Katika maeneo ya wazi ya kupumzikia wananchi
II. Kuondoa watu wanaopika au kuandaa chakula katika mazingira machafu na yanayohatarisha afya za walaji
III. Kuondoa vibanda vyote vilivyojengwa katika maeneo ya pembeni mwa barabara na au katikati ya barabara bila vibali vya ujenzi
IV. Kukamata wachafuzi wa mazingira ikiwemo mifereji ya wazi, barabara kwa makusudi na kusababisha chukizo (Nuisance) kwa jamii yetu
V. Kuondoa meza zote zinzotumiwa na wafanyabiashara kandokando ya barabara hasa nyakati za usiku
VI. Kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheri ikiwemo kuwatoza faini za papo kwa papo na aidha kuwapeleka mahakamani.
VII. Kuondoa ombaomba wanaozagaa katika barabara na kusumbua wananchi nyakati mbalimbali
VIII. Kupanda miti maeneo ya bustani na maeneo ya wazi
IX. Kuhamasisha jamii kwa njia ya matangazo juu ya Afya na usafi wa mazingira,
X. Kutoa matangazo ya operesheni kwa njia ya vipaza sauti,redio na television.
Matokeo ya operesheni zinazoendelea kufanyika
Kwa kuwa halmashauri imejipanga kusimamia usafi endelevu tayari hatua zilizochukuliwa ni kama ifuatavyo;-
1. Jumla ya meza zilizovujwa 2193
2. Idadi ya mabanda yaliyovunjwa 415
3. Jumla ya watuhumiwa 172 walikamatwa na watu 92 walipewa onyo kali, ambapo waliotozwa faini za papo kwa papo ni 80 jumla ya TSHS 4,120,000/=
4. Watu 45 wamepelekwa mahakamani na kesi zao zinaendelea
5. Jumla ya ombaomba 74 walikamatwa na kurudishwa makwa
Jambo hili limeleta hamasa kwa wananchi kujua kuwa jukumu la usafi wa mazingira ni la kila mtu.
Pia barabara zetu kwa maeneo ambayo yalisongwa sana mfano pale charambe na mianzini sasa yanapitika
Nyumba na majengo ya biashara
Usafi wa nyumba za kuishi na majengo ya biashara tathmini yake inapatikana baada ya Maafisa Afya wa Kata kuendesha zoezi la ukaguzi wa nyumba hadi nyumba kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati za Afya za mitaa husika ambao wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika jukumu hili.
Dhumuni la ukaguzi ni kuangalia
• Usafi wa Mazingira kwa ujumla;
• Uzalishaji, ukusanyaji na utupaji wa taka ngumu na taka miminika;
• Hali ya vyoo ikijumuisha uwepo wa maji ya kunawia mikono, mfuniko; utumiaji sahihi wa vyoo na kukamilika kwa ujenzi wa vyoo;
Mwezi January hadi aprili 2014, jumla ya nyumba 3614 na majengo ya biashara 225 yamekaguliwa. Kwa kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu.
Kwa kawaida wahusika wote wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za Afya na Usafi wa mazingira wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
Kuwapa ilani za kisheria za marekebisho ya dosari zilizogundulika;
Kuwatoza faini za papo kwa papo
Kuwafungia na
Au kuwapeleka Mahakamani
MAMBO YANAYOCHANGIA UCHAFUZI WA MAZINGIRAUjenzi holela wa makazi na vyoo
Ukosefu wa miundombinu kwenye makazi yasiyo rasmi
Uhaba wa mabwawa ya maji machafu (Public sewer system),
Utupaji wa taka ovyo
Ufunguliaji wa maji taka nyakati za mvua kwenye mifereji ya wazi
Kuunganisha mfumo wa maji taka toka viwandani kwenye mifereji ya maji ya mvua
Ukosefu wa vyombo vya kuhifadhia taka ngumu katika maeneo maalumu.
MBINU ZINAZOTUMIKA KATIKA KUIMARISHA USAFI WA MAZINGIRAKufanya mashindano ya usafi kuanzia ngazi ya Mtaa na Kata na mshindi kupatiwa zawadi stahili.
Kufanya mikutano ya pamoja ya wadau na kuwataka kuwasilisha taarifa zao za utendaji na kuzijadili.
Kuweka mikakati ya pamoja ya utekelezaji wa shughuli za utunzaji wa usafi wa mazingira kwa kutumia mbinu shirikishi ya CLTS (Community Led Total Sanitation).
Kufungua milango kwa wadau wenye uwezo na nia ya kuchangia shughuli za Afya na usafi wa mazingira.
William J. Muhemu
AFISA AFYA WA MANISPAA YA TEMEKE
KNY; MKURUGENZI WA MANISPAA YA TEMEKE
No comments:
Post a Comment