KWA mara ya kwanza dunia itashuhudia fainali ya kwanza ya UEFA mei 24 mwaka huu mjini Lisbon, Ureno, itayozikutanisha timu mbili zinazotoka mji mmoja yaani Madrid.
Hii ni baada ya Atletico Madrid kufuzu fainali usiku huu kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Mechi ya kwanza nchini Hispania katika uwanja wa Vicente Calderon, timu hizi zilitoka suluhu, lakini leo Chelsea wameachia na kutolewa kwa wastani wa mabao 3-1 katika mechi zote mbili za nusu fainali.
Katika mchezo wa leo, Fernando Torres alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 36 kwa pasi ya Azpilicueta baada ya kazi nzuri ya Willian.
Dakika 8 baadaye, Adrian Lopez akaisawazishia Atletico kwa pasi ya Juanfran.
Diego Costa katika dakika ya 61 alifunga bao la pili kwa penalti iliyosababishwa na Samuel Eto`o.
Wakati Chelsea wakihaha kusawazisha bao hilo, dakika ya 72, Arda Turan alipiga kidude cha tatu na jahazi la Chelsea kutota kabisa.
Mouringo katika dakika ya 54 alimtoa beki wake, Ashley Cole na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji, raia wa Cameroon, Samuel Eto`o ambaye alisababisha penati iliyowapoteza Chelsea.
CHANZO,FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment