Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla (kulia), akipata maerlezo kutoka kwa kiongozi wa Mafundi wa
Kampuni ya CDM Smith, John Donoherth, kuhusu ujenzi wa kisima kilichopo
Mkwalia Mkuranga ambacho ni moja kati ya visima 8 vinavyofanyiwa utafiti
maji wilayani humo. Makalla alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji
wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo. Pia alikagua mradi wa kisima cha
maji cha Nyamato chenye uwezo wa kutoa maji lita 26,000 kwa saa
kitakachohudumia wakazi wa vijiji vya Mvuleni, Nyamato na Kilimahewa.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Waziri Makalla akiangalia mradi wa kisima cha Mkwalia ambacho kinafanyiwa utafiti
Maji yakitiririka kwenye kisima hicho
Makalaa akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kisima hicho,John Donoherth
Naibu
Waziri Makalla akielezea namna Kisima kipya cha Nyamato kikianza
kufanya kazi kuwa kitakuwa kinatoa lita 26,000 za maji kwa saa na
kuhudumia sehemu kubwa ya wananchi wilayani Mkuranga, Pwani. Atakizindua
kisima hicho mwanzoni mwezi ujao kitakapowekwa pampu iliyoagizwa Afrika
Kusini. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamage, Abdallah
Kiyewehe ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maji kijijini hapo.
Mama
mkazi wa Kijiji cha Mvuleni, wilayani Mkuranga akielezea mbele ya
waziri jinsi wanawake wa eneo wanavyopata taabu ya kuata maji karibu
umbali wa Km 5, na kuonesha furaha ya kupata kisima hicho
kitakachowaondolea adha waliyokuwa wanaipata.
Eneo la Kisima cha Nyamato kilichogauliwa. Kisimamhicho kinasubiri pampu tu ili kianze kufanya kazi.
Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mvuleni baada ya
kukagua kisima cha maji cha Nyamato, wakati wa ziara yake wilayani
Mkuranga leo.
Sehemu
ya umati mkubwa wa wananchi ukimsikiliza Makalla akihutubia kwa
kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwaboreshea wananchi sekta ya maji.,
ambapo zimetengwa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya wilaya hiyo.
Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makalla
Katibu wa Kamati ya Maji ya Mradi
wa Nyamato, Ali Salum akielezea jinsi mradi wa Nyamato unavyosuasua
kuzinduliwa, akidai anayesababisha hivyo ni Mkandarasi wa mradi huyo
ambaye hatoi taarifa yoyote juu ya ucheleweshwaji huo.
Mkandarasi wa mradi wa maji wa
Nyamato, Jamila Chibwana wa Kampuni ya Mac Consultant akitoa majibu ya
ucheleweshwaji wa mradi huo, ambapo alisema moja ya sababu
zilizosababishwa ni kutopewa fedga za ujenzi kwa wakati na uagizaji wa
pampu kutoka Afrika Kusini.
Makalla akiagana na wananchi baada ya mkutano kumalizika.
Credit Source: Fullshangweblog
No comments:
Post a Comment