Afisa Mkuu wa Fedha wa
Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi
milioni 200, kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye
pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi kwa ajili ya kudhamini
mkutano huo. Katikati ni Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham Shamumoyo
XXXXXXXXXXXXXXX
Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 31 katika hoteli ya Kunduchi
jijijni Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Mkutano huo unaodhaminiwa na benki ya NMB
ni “Wananchi
pigia kura katiba pendekezwa kuboresha Serikali za Mitaa na maendeleo endelevu
baada ya mwaka 2015”“.
Mkutano mkuu wa 31
unafanyika pamoja na mambo makubwa mawili yafuatayo; Moja ni Sherehe za Miaka
30 ya Serikali za Mitaa na ALAT ambayo itakuwa na kongamano la kutathmini
tulikotoka, tulipo na kuangalia nini cha kufanya huko mbeleni ili kuziwezesha
Serikali za Mitaa kutoa huduma kwa ufanisi zaidi. Pili, shaerehe za tuzo za
viongozi bora wa Serikali za Mitaa (Mayors Award). Kwa mara ya kwanza ALAT
itatoa tuzo kwa viongozi wa Halmashauri ambao wanafanya vizuri katika kusimamia
Halmashauri zao. Katika mchakato wa kuwapata viongozi bora wananchi
wameshirikishwa kwa kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu kwenda namba 15440.
Kwa mwaka wa pili
mfululizo, NMB wamekuwa wakidhamini mkutano wa ALAT na kwa mwaka huu, wametudhamini
kwa shilingi milioni 200 ambapo milioni 150 ni kwaajili ya matayarisho ya
mkutano na milioni 50 kwaajili ya ununuzi wa trekta ambalo litakabidhiwa kwa
washindi wa tuzo ya uongozi bora wa Serikali za Mitaa (Mayors Award). Trekta
hili tunaimani litasaidia shughuli mbalimbali za halmashauri iliyoshinda kama
shughuli za ukandarasi ikiwemo utengenezaji wa barabara na urekebishaji wa
miundombinu ndani ya halmashauri.
Mkutano wa mwaka huu una
umuhimu wa pekee katika historia ya Serikali za Mitaa na taifa letu kwa jumla.
Mwaka huu ni mwaka wa 31 tangu kurejesha mfumo wa Serikali za Mitaa hapa nchini
mwaka 1984; pili Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania inaadhimisha miaka 31
tangu kuanzishwa kwake tarehe 13 Disemba 1984. Tatu mwaka huu nchi yetu
inapitia kwenye mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
itakayotuwekea misingi na kanununi za uendeshaji wa nchi yetu kwa miaka 50
ijayo ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo ya Serikali za Mitaa itakayo jikita
kwenye ugatuaji wa madaraka kupeleka kwa wananchi.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa
Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni: Wenyeviti na Mameya
168 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 168 wa
Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na
Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika
Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika
ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau
wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa.
Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi
zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta
Binafsi. Inatarajiwa kwamba Mkutano huu
utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (550). Mkutano Mkuu wa ALAT ndiyo
chombo cha juu kabisa cha maamuzi cha Jumuiya.
Maandalizi yote kwa ajili
ya Mkutanop yamekamilika kwa asilimia 95 na kwa namna ya pekee Kabisa
tumemwalika Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya
Mrisho Kikwete kuwa Mgeni Rasmi wa mkutano wetu Mkuu pamoja na kutoa tuzo za
kwa Mameya/wnyeviti wa Halmashauri.
Niwashukuru wadau
mbalimbali amabo wamejitokeza katika kufadhili na kusaidia Mkutano huu. Kwa
namna ya pekee kabisa niwashukuru benki ya NMB kwa kuendelea kuwa mwenza
(partner) katika Mkutano huu na tuzo za viongozi wa serikali za Mitaa.
Niwashukuru pia PSPF, MABIBO BEER & WINE, MSD, NHC, NIDA, GF TRUCKS,
PPF,TBA, TAA, LAPF, TSN, UTT.
Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji,
Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 168
zinazounganishwa na chombo hiki.
No comments:
Post a Comment