Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 19 April 2015

YANGA, ETOILE KUMALIZANA TUNISIA


NA FAUSTINE FELICIANE
Etoile du Sahel ya Tunisia jana ilififisha matumaini ya Yanga ya kusonga mbele kwa kuilazimisha sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya timu 16 bora ya Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika, kwenye Uwanja wa Taifa.


Etoile ilipata bao la kusawazisha dakika moja tangu kuanza kwa kipindi cha pili, baada ya shuti la chinichini la Ben Amor Med Amine kutoka nje ya eneo la hatari kupita kwa namna ya ajabu chini ya mwili wa kipa Ally Mustafa aliyechupa kuudaka kirahisi.

Amisi Tambwe wa Yanga alifanikiwa kutumbukiza mpira wavuni dakika mbili kabla ya filimbi ya mwisho lakini 'goli' lake lilikataliwa kwa kuwa aliotea.

Kwa matokeo hayo, Yanga inalazimika kwenda kupata ama ushindi ama sare ya zaidi ya 1-1 katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo ili kuwa timu ya kwanza ya Bara kufuzu kucheza ligi ya robo-fainali ya Kombe la Shirikisho.

Bao la Yanga lilikuja baada ya sekunde 120 kwa njia ya penalti iliyofungwa na nahodha Nadir Haroub ambaye shuti lake kali lilifanikiwa kumpita langoni Mathlouthi Laymen licha ya kipa huyo wa Etoile kulifuata.

Penalti hiyo ilitolewa na muamuzi Samuel Chirindza wa Msumbiji baada ya Laymen kumuangusha Simon Msuva kwenye eneo la hatari, akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga kutokana na pasi ya Tambwe.

Haroub aliumia mwishoni mwa kipindi cha kwanza na nafasi yake kimchezo kuchukuliwa na kiraka Mbuyu Twite baada ya mapumziko, ingawa Said Juma ndiye aliyeingia uwanjani kuziba pengo hilo.

Mbali na goli la kuotea, Yanga na Etoile kila moja ilipoteza nafasi nyingi nzuri za kufunga katika kipindi cha pili lakini ni wageni ambao inaelekea hawatachukizwa na udhaifu huo, wakitaraji kwenda kumaliza kazi Tunisia wiki mbili baadaye.

Mara tatu katika kipindi cha kwanza ambacho wenyeji walifunikwa kabisa kimchezo kutokana na kasi na pasi fupifupi za wageni, Yanga iliponea chupuchupu kutota.

Kelvin Yondani aliondoa mpira kwenye chaki dakika saba tangu timu yake ipate bao la kuongoza na kipa Mustapah alionyesha ushujaa kwa kupangua mashuti mawili likiwamo la mshambuliaji wa Etoile, Mouihb Youssef lililokuwa likienda wavuni baada ya nusu saa ya mchezo.

Kufikia kukabiliana na Etoile katika mchezo wa kwanza jana, Yanga iliziondoa kwenye mashindano BDF XI ya Botswana na Platinum ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao 9-3.

YANGA: Ally Mustafa, Juma Abdul (Rajab Zahir dk.82), Oscar Joshua, Nadir Haroub (Said Juma dk.45), Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga (Kpah Sherman dk.77), Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Mrisho Ngassa, Simon Msuva.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment