Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 20 April 2015

MANJI AENDELEA KUWA BUBU MABILIONI YA JAPAN

Mbunge wa Konde Khatib Said Haji (CUF).
Wakati Mfanyabiashara Yusuf Manji akiendelea kukaa kimya bila kutoa majibu juu ya kuhusika kwake na kilio cha wafanyabiashara wa kati ambao wameingia kwenye madeni makubwa kutokana na fedha za kusaidia uagizaji wa bidhaa kutoka nje (Commodity Import Support – (CIS), wiki hii serikali inatarajia kuwasilisha kwa kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara ripoti vigogo waliokalia mabilioni ya fedha hizo kwa miaka kadhaa sasa.
 
Manji anatajwa na baadhi ya wafanyabiashara wa kati kwamba aliingia nao makubaliano ya kuwalipia asilimia 30 ya mikopo yao kutoka Japana chini ya mpango wa CIS, kisha kuchukua haki ya kuagiza bidhaa kwa kunufaika na asilimia 70 ya mkopo huo, lakini baada ya kuuza mali husika fedha hizo hakuzirejesha serikalini kwa mujibu wa mpango huo.
 
Kwa takriabani mwezi mmoja sasa Manji amekaa kimya kujibu maswali ya waandishi wa NIPASHE juu ya kadhia hii. Kila wakati katibu muhutasi wake ambaye ndiye anapokea mawasiliano yote ya kiofisi na simu ya mkononi ya mfanyabiashara huyo, kila anapoulizwa juu ya majibu hayo amekuwa akiliambia gazeti hili kwamba maswali yake hayajajibiwa.
 
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, nchi washirika wa maendeleo wa Tanzania, hususan, Japan, Canada, Norway na Sweden, zilikuwa zikikopesha wafanyabiashara wa kati wa Tanzania fedha hizo, kwa sharti la kulipia asilimia 30 ya bidhaa husika, ili wapate fursa ya kupata mkopo wa asilimia 70 ya bidhaa hizo kutoka nchi hizo. Baada ya kuagiza bidhaa na kuziuza, malipo ya mkopo huo yaani asilimia 70 walipaswa kulipa serikalini.
 
Kwa miaka kadhaa sasa wafanyabiashara wa kati wamekuwa kwenye wakati mgumu juu ya ulipaji wa madeni hayo kwani hawakunufaika na mikopo hiyo baada ya kuuza haki hizo kwa Manji ambaye naye anadaiwa kuwa hajalipa mabilioni hayo serikalini.
 
Wiki hii wafanyabiashara, kampuni na viwanda waliokopeshwa zaidi ya Sh. bilioni 328 watajikuta katika wakati mgumu zaidi serikali itakapowasilisha ripoti kwa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara ikiwa na majina ya vigogo waliokopeshwa mabilioni hayo.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Luhaga Mpina, Machi 31, mwaka huu mjini Dodoma aliiagiza serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kwamba Aprili 20, mwaka huu deni hilo liwasilishwe katika kamati hiyo likiwa limekokotolewa pamoja na riba ambayo ni asilimia 15.15.
 
Kutokana na hali hiyo, Mpina ambaye pia ni mbunge wa Kisesa alisema kuwa deni hilo litakapokokotolewa pamoja na riba litafikia zaidi ya Sh. bilioni 600.
 
Fedha hizo zilikopeshwa kwa wafanyabiashara, kampuni na viwanda zaidi 980 kwa nyakati tofauti kati ya 1992/1993, 1994/1995 na 2002/2003 na wamerejesha Sh.bilioni 95.1 tu. Manji anadaiwa kununua hati nyingi za wafanyabiashara hao kwa mlango wa nyuma.
 
Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara walipokutana na wataalam kutoka Wizara ya Fedha kujadiliana kuhusu fedha hizo walisema kuna agenda ya siri katika fedha hizo kwani inawezekano wapo watu wakubwa waliokopeshwa na ndiyo maana serikali inapata kigugumizi kukusanya deni hilo.
 
Mbunge wa Konde Khatib Said Haji (CUF), alitaja baadhi ya kampuni zilizoorodheshwa kwenye taarifa hiyo ya Serikali kuwa zinahusishwa katika deni hilo, kuwa ni pamoja na Quality Garage na Azania Industry.
 
Katika ufisadi huo, Manji anadaiwa kuwaingiza kwenye deni la kukopa fedha katika mfuko wa kusaidia uagizaji bidhaa kutoka nje (Commodity Import Support – CIS), zilizotolewa na serikali rafiki kwa Tanzania ikiwamo Japan.
 
Habari zaidi zinasema kuwa Manji alichukua jukumu la kulipa malipo ya awali ya asilimilia 30 ya mkopo (cash cover) na kuwalipa fedha hao wafanyabiashara wa kati ambayo kwa maelezo yao ilikuwa ni kati ya asilimia 20 hadi 30 ya thamani ya mkopo.
 
Hata hivyo, vyanzo vyetu vinasema kuwa makubaliano hayo yaliacha upenyo juu ya uwajibikaji wa malipo ya asilimia 70 ya mkopo ambayo ilipaswa kulipwa kwa serikali ya Tanzania ukiwa ni msaada kutoka Japan. 
 
“Sheria ya CIS na mikataba tuliosaini (wafanyabishara) zinasema wazi kwamba albaki ya asilimia 70 lazima ilipwe ndani ya siku 90 baada ya bidhaa kuagizwa,” kilisema chanzo chetu.
 
Hofu ambayo sasa inasumbua vichwa vya wafanyabiashara hao ni ukweli kwamba serikali kupitia wakala kama Mamlaka ya Kodi na wakusanya madeni inaruhusiwa kukamata na kuuza mali za wale watlioshindwa kurudisha fedha za Japan, huku mnufaika mkuu Manji akiendelea kutanua vitegauchumi vyake nchini.  
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment