Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 28 April 2015

MAANDAMANO YACHACHA BURUNDI

Waandamanaji nchini Burundi
Maandamano yanaendelea kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura kwa siku ya tatu kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.

Watu wanachoma magurudumu ya magari na kuweka vizuizi huku nao polisi wakirusha vitoa machozi.
Maandamano hayo kwa mara ya kwanza, yamesambaa kwenda nje ya mji mkuu. Polisi wamezuia wanafunzi wa chuo kikuu kwenye mji ulio kati kati mwa nchi wa Gitega waliojaribu kuandamana kwenda mjini.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu watu 25,000 wamekimbia nchi hiyo ndani ya majuma mawili yaliyopita, wakihofia kuongezeka kwa ghasia kabla ya uchaguzi mkuu unaokuja.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment