Afisa
Uhakiki, Neema Chilipweli (kushoto) akiihakiki familia ya Yohanna Bukuru (watatu
kulia), pamoja na mkewe na watoto wao sita kutoka Kijiji cha Kapemba, Kata
yaMishamo, wilayani MpandaVijijini, Mkoa wa Katavi, ikiwa ni hatua ya awali ya uhakiki
ili familia hiyo iweze kupewa vyeti vya uraia wa Tanzania. Zaidi ya watu 152,572
katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi
wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 n akupewa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya
wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi
la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo ambapo
wiki hii zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo nchini, linatarajiwa kukamilika. Serikaliya
Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR)
katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Na
Felix Mwagara, Mishamo
ZOEZI la ugawaji wa
vyeti vya uraia wa Tanzania kwa waliokuwa Wakimbizi wa Burundi zaidi ya 152,572
walioingia nchini mwaka 1972 linatarajiwa kumalizika wiki hii katika Makazi ya
Mishamo mkoani Katavi.
Wakimbizi hao ambao
waliomba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi mwaka 2010, sasa watakuwa raia halali wa Tanzania kwa kuwa na uwezo wa
kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za Udiwani
na Ubunge.
Akizungumza wakati wa
ugawaji wa vyeti hivyo, Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile alisema
ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24 mwaka jana, katika Makazi ya Katumba yaliyopo
mkoani Katavi, ambapo watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye zoezi la
ugawaji likahamia katika Makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, ambapo watu 43,453
tayari wamepewa vyeti hivyo.
Nisajile alisema katika
makazi yake ya Mishamo ambapo ugawaji wa vyeti hivyo unaendelea na unatarajiwa
kumalizika ifikapo Aprili 30 mwaka huu, ambapo katika makazi hayo zaidi ya raia
wapya 52,565 wanatarajiwa kupewa vyeti vyao.
“Mpaka leo hii (jana)
katika makazi haya ya Mishamo kama unavyoshuhudia ndugu mwandishi umati wa watu
wakizidi kuingia katika kituo hiki, mpaka sasa tayari tumegawa vyeti 131,351
kwa raia hawa wapya, na tunatarajia ifikapo wiki ijayo Aprili 30 tutakuwa
tumemaliza ugawaji wa vyeti hivi katika vijiji vyote, na zaidi ya raia wapya
152,572 katika Makazi ya Katumba, Ulyankulu na Mishamo watakuwa wamepewa vyeti
hivi na zoezi litakuwa limekamilika” alisema Nisajile.
Alisema Serikali ndiyo
inatoa vyeti hivyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia
Wakimbizi (UNHCR), ambapo wote kwa pamoja wamejipanga kikamilifu ili ugawaji
huo unamalizika salama na kwa umakini wa hali ya juu.
Hata hivyo, Nisajile
alisema kuwa, makazi yake ya Mishamo yana vijiji 16, hivyo kabla ya kuanza
kugawa vyeti hivyo, huwa wanatoa elimu kwa kuwahamasisha wakazi wa kijiji
ambacho kinatarajia siku ya pili yake kwenda kugawiwa vyeti hivyo.Alisema katika
uhamasishaji huo, yeye Mkuu wa Makazi anaambatana na Maafisa Uhamiaji na UNHCR
ili waweze kuhamasisha mambo mbalimbali kuhusiana na umuhimu wa vyeti hivyo.
Aliongeza kuwa, vyeti
hivyo vinatolewa kwa mtu mmoja mmoja ambapo raia mpya anatakiwa aje na karatasi
ya uthibitisho wa picha za wanafamilia ili kuiwezesha Serikali na UNHCR
kutambua kabla ya kutoa cheti kwa wahusika hao na kila anayepewa cheti hicho anatakiwa
kusaini.
Zoezi la ugawaji wa
vyeti vya uraia kwa raia hao wapya lilikuwa la miezi mitano, ambapo lilianza
Novemba 24 mwaka 2014, na Aprili 30 wiki hii,
linatarajiwa kukamilika.
No comments:
Post a Comment