Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar) Salum Mwalimu akisisitiza jambo wakati akiongea na viongozi wa Vijiji na Mitaa wa chama hicho katika semina ya kuwajengea uwezo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Libori mjini Sumbawanga leo hii.
Viongozi wa Vijiji na Mitaa wa Chadema wakiunga mkono hoja kwenye mkutano huo.
Silinde yuko makini akisikiliza, hajalala.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, China wa China.
Viongozi wa Chadema wakisikiliza maelezo ya viongozi wa vijiji mkoani Rukwa leo hii.
Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde naye 'akimwaga sumu'.
Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Frank Mwaisumbe.
Na Mwandishi Wetu, Sumbawanga
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepoteza baraka za Mungu ndiyo maana mpaka sasa hawajajua nani atakayemrithi Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa mwaka huu.
Chadema imesema kwamba, CCM inaandamwa na laana ya damu nyingi za Watanzania zilizomwagika bila hatia, hali ambayo inakifanya chama hicho kishindwe kujua nani atakiwakilisha katika uchaguzi wa mwaka huu, likiwa ni jambo la ajabu kutokea katika historia yake.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya viongozi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa wa chama hicho katika ukumbi wa Libori mjini hapa leo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu,
amesema viongozi hao wapaswa kuwa tayari
kusimamia haki kwa gharama zozote, kukataa rushwa na kupunguza kero kwa
wananchi, na kuonya wasije wakaufanya utawala Chadema kuwa kama wa CCM ambayo
inayumba.
“Damu ya Watanzania iliyomwagwa na CCM malipo yake yanalipwa
na Mungu… tuna miezi mitatu imesalia tuanze kampeni, lakini mpaka sasa CCM
haijamjua mgombea wake, lini imewahi kutokea? Mungu amewachanganya kama wajenzi
wa karavati,” alisema Mwalimu.
Alisema viongozi wanaotokana na Chadema wasikubali utawala wao
ukakosa baraka za Mungu na njia pekee ni kuwatumikia kwa haki Watanzania.
Mwalimu alionyesha kushangazwa na baadhi ya wafuasi wa
Chadema kujiunga na chama cha ACT – Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe na
akakiita kuwa ni chama msimu ambacho kitapotea baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Alisema Chadema haiwezi kumkataza mtu kujiunga na ACT lakini
ni vema wananchi wakaelewa kwamba kile si chama chenye malengo ya kuleta ukombozi
kwa Watanzania bali kipo kwa maslahi ya watu wachache na kitadumu kwa muda
mfupi tu.
“WanaChadema msikubali kuyumbishwa kwani tumehangaika
kuijenga Chadema katika misingi madhubuti ambayo hata wananchi wamekikubali,”
alisema.
Awali, Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde alisema watu
walioonyesha nia kugombea nafasi za udiwani na ubunge wasitumie nafasi hiyo
kukigawa chama badala yake wawe wepesi kushirikiana na yule atakayeteuliwa ili
malengo yao ya kuwakomboa Watanzania katika lindi la umaskini yaweze
kufanikiwa.
Mbunge huyo alisema umefika wakati jimbo la Sumbawanga Mjini
lipaswa kukombolea kutoka mikononi mwa CCM ili wananchi waondokane na kero
zisizo za msingi za kudaiwa michango isiyo na ‘kichwa wala miguu’ ikiwemo ya
uandikishaji wa wanafunzi.
“Tangu Chadema ianze kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya
Momba, michango yote ikiwemo ya uandikishwaji ambayo mzazi alitozwa kati ya Sh20,000
hadi 50,000 imefutwa hali ambayo imeongeza idadi ya watoto wanaoandikishwa
darasa la kwanza kutoka 80 kwa darasa moja hadi 300,” alisema.
Naye Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa chama hicho,
Frank Mwaisumbe, alisema Rukwa ndiyo imeoongoza katika mikoa mitano ya Nyanda
za Juu Kusini kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, hivyo aliwashukuru wananchi
kwa kuiunga mkono Chadema.
“Ninawaomba mfanye hivyo kwenye uchaguzi mkuu ujao ili chama
kiweze kutwaa dola na kuwakomboa wananchi kwa kuwatoa katika hali ya ufukara
huku watu wachache wakijilimbikizia mali,” alisema.
Mwaishumbe aliongeza kuwa, viongozi waliotokana na Chadema
wanapaswa kulipa fadhila hizo kwa kutenda haki kwa wananchi na kuondoa kero
ambazo zimekuwa mzigo mkubwa kwao.
No comments:
Post a Comment