Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 27 April 2015

MVUA KUNYESHA NA KUSABABISHA WATU KUKOSA MAKAZI


Na Hastin Liumba, SikongeMVUA inayoendelea kunyesha sehemu mbalimbali hapa Nchini Imesababisha maafa na uharibifu mkubwa wa kaya 27 zenye watu 135 kukosa makazi katika Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora.


Akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali jana,Mkuu wa Wilaya hiyo Hanifa Seregu alisema kuwa Mvua hiyo ilianza kunyesha mwezi April 5 hadi 10 mwaka huu majira ya saa Tano usiku.

Seregu alisema kuwa mvua hiyo ilinyesha katika wilaya ya Sikonge na kusababisha maafa katika kitongoji cha Makingi kijiji cha Mwanamkata kata ya usunga Wilayani humo.

Alisema kuwa familia zilizoathirika na mvua hiyo ni kaya 27 zenye watu 135 ambao waliokuwa wakiishi mabondeni katika kitongoji hicho na kusababishia watu hao kukosa makazi.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Sikonge Amewataka wananchi wanaoishi mabondeni wahame mara moja wahamie kwenye mwinuko ili kujiepushia athari zingine zinazoweza kutokea katika kipindi hichi cha mvua kunyesha.

Nae Diwani wa kata ya Usunga Mariamu Ukongo,alisema kuwa Familia hizo zilizoathirika na mvua hiyo ni kaya 27 zilizopo katika kijiji cha Mwamkata Wilayani Sikonge.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu wanaoshughulikia Maafa Gerad Mwagalazi,alisema kuwa mpaka sasa Wilaya hiyo,Imepokea Msaada wa maturubai matano na mtaalamu wa kuyafunga amekwishafika katika eneo hilo kutoka Jeshi la wananchi wa Tanzania TPDF.

Mwagalazi alisema kuwa maturubai hayo yametolewa kwa ajili ya watu hao waliokosa makazi ili kuwahifadhia katika shule ya msingi ya Mwanamkata Wilayani humo.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Jitihada za kuwatafutia waathirika hao Magodoro, Mashuka na Mabranket zinafanyika ili kuwasaidia katika kipindi hichi cha Mvua Zinazoendelea kunyesha hapa Nchini.

No comments:

Post a Comment